Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, November 6, 2012

Lucy Aongea na Ohayoda: Baada ya kufanya vizuri Redds Miss Tanzania 2012,

Mara baada ya kumalizika kwa shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2012 na Brigitte kuibuka mshindi, Ohayoda ilipata fursa ya kufanya mahojiano na Lucy Stephano ambaye alikuwa akiuwakilisha mkoa wa Manyara na Kanda ya Kaskazini.
Lucy ambaye awali alishinda taji la mrembo mwenye haiba zaidi nchini (Miss Photogenic 2012) na kuwa mshiriki wa kwanza kuingia katika hatua ya 15 bora, amejinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 1 na laki mbili, japo hakuweza kuingia katika hatua ya tano bora, lakini ni mmoja kati ya washiriki waliopata mafanikio makubwa katika nshindano hilo.
Lucy Stephano akiogopa kumshika nyoka, Meserani Snake Park
Ohayoda iliongea na Lucy kwa njia ya simu mara baada ya kutoka kambini jana na alieleza furaha aliyonayo kwa hatua aliyofikia na mafanikio aliyoyapata na kueleza malengo yake ya mbeleni. 
"Kwanza ninamshukuru Mungu, familia yangu, marafiki na watu wote walionisapoti hadi hapa nilipofikia" 
"Nimefurahi sana na sikutarajia kufikia hatua hii, nilitiwa moyo na sapoti kubwa sana niliyoipata kwa watu wote wa Mkoa wa Manyara, wengi walikuwa wakinipigia simu na kunitia moyo, kutokana na hayo nilipata moyo na kufikia hapa nilipo" alisema Lucy kwa furaha
Aidha Ohayoda ilitaka kujua amepokeaje matokea hasa kwa kushindwa kuingia tano bora, alisema ameridhishwa na matokea na hawezi kulalamika.
Lucy Stephano (No4) wa kwanza kulia katika shindano la Redds Miss Tanzania 2012, Ubungo Plazza 3/11/2012
"Naamini majaji walifanya kazi yao bila upendeleo na aliyeshinda hakupendelewa kwani alistahili" alisema Lucy
Lucy ambaye atarejea Haydom wiki ijayo kutoka jijini Dar es Salaam ambapo atapitia Babati kisha kabla ya kufika Haydom, anatarajia kuendelea na mipango yake ya maisha baada hasa ndoto yake ya kuwa mtaalamu wa Maabara
"Mpaka sasa mipango yangu haijabadilika, nitarejea Haydom na mwakani mwezi Januari nitaenda chuo cha Maabara kusoma"
"Kwa sasa sijui kama nitaendelea katika tasnia ye urembo ila kama ikitokea opportunity ya kufanya kazi na makampuni yatakayonihitaji nitakuwa tayari ila kwa sasa lengo langi ni kuwa mtaalamu wa maabara" aliongeza Lucy aliyekuwa akiongea kwa kujiamini tofauti na awali.
Lucy alieleza kuwa anaamini mafanikio aliyoyapata yatafungua milango kwa wasichana wengi kuingia katika tasnia hiyo na kujipatia ajira kama ilivyo sanaa nyingine kwani yeye binafsi amefanikiwa kusoma masomo ya Kumpyuta katika chuo kikuu huria na pia ameongeza upeo (exposure) tofauti na alivyokuwa kabla. 
Je ni kweli Lucy atarejea na kuishi kama awali Haydom? au ndo ashakuwa matawi ya Juu? Yetu macho


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda