Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, November 19, 2012

LOWASA ACHANGISHA MILIONI 134 BABATI, GESSO BAJUTA ACHANGIA 1,000,000/=


Na Mary Margwe,
Babati
Aliyekuwa Waziri  Mkuu Mh. Edward Lowassa apokelewa kwa kishindo kikubwa  ambapo amewaachia simulizi  midomoni mwa wananchi wa Mkoa wa Manyara, amechangisha Harambee ya ujenzi unaoendelea wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri  Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini  kati usharika wa Mjini Babati ambapo amefanikiwa kuvuka lengo lililokusudiwa la sh.mil.120, na kuchangisha  jumla ya sh. Mil.134, 295, 058/=
Akiongea katika harambee hiyo iliyofanyika  jana katika kanisa hilo, Lowassa alisema kuwa vipo baadhi ya vyombo vya habari vinavyomtafrisi  kuwa ana fedha nyingi, jambo ambalo yeye amekama tuhuma hizo na kusema  kuwa huwa huwa anafanya kazi ya kuhamasisha marafiki zake, na hatimaye kufanikisha shughuli za harambee mbalimbali.
Lowassa alitoa jumla ya sh.mil.7 kuchangia harambee hiyo, alisema yeye bado hajafilisika katika kumtolea Mungu sadaka, ambapo anazidi kumuomba mwenyezi Mungu ili aweze kumsaidia katika kufanikiwa  shughuli mbalimbali za kimaendeleo husuani kwa upande wa kumtolea Mungu sadaka.
“Mimi sina hela nyingi kama vinavyonizungumzia vyombo mbalimbali vya habari, huwa nahamasisha marafiki zangu  na kunisaidia kunichangia harambee zote ninachochangisha, na sivyo hivyo wasemavyo watu ama vyombo vya habari” alisema Lowassa.
Aidha Bw.Lowassa alifanikiwa kuchangisha jumla ya sh. Mil.134,295,058, huku fedha taslimu zikiwa sh. Mil.86,540,480.058 wakati ahadi ikiwa ni sh.mil.47,754,950,
Harambee hiyo ilishirikisha viongozi mbalimbali wa chama na Serikali akiwepo Mbunge wa Jimbo la Babati Mijini Bw.Kisieri Warema Chambili aliyechangia jumla ya sh. Mil.2,500,000, Mbunge wa Babati Vijijini, Bw.Jitu Urajlal Soni aliyechangia kiasi cha sh.mil. 2,000,000, mbunge wa viti maalum kupitia tiketi ya CHADEMA Bi.Paulina Gekul  alichangia sh. Mil 2,400,000 Bw.Gesso Bajuta sh.1,000,000 mkurugenzi wa NSSF Mkoani Manyara Bw.Shedrack Kitomari aliyechangia sh.mil 2,300,000
Wengine ni Bi.Anna ufoo Ulomi (mfanyabiashara maarufu Mjini Babati) aliyechangia sh.mil.1,600,000, Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Bw.Willfred Mushi sh.900,000 Bw.Gamaliel Ndosi aliyechangia kiasi cha sh. 812,000 katibu wa ujenzi wa jengo Bw.Walter Ulotu aliyechangia sh.609,000 Bw.Frank Lwenge sh.813,000 Bw.Isack Mush sh.800,000 Familia ya Bw.Elias Koka sh.700,000 Bw.John Mboya sh.400,000 Bi.Miriam  Lechipya sh.312,000 Bw.Josson Begashe sh.300,000 Bw.Saul Lema sh.200,000 Bi.Anande Nassari  sh.104,000.
Naye Mkuu wa  kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya kaskazini kati Dkt.Thomas Laiser alisema Lowassa ana jina kubwa kwani hata kwenye maandiko matakatifu inaeleza hivyo, ambapo alisema ni mahiri katika utendaji wake wa kazi kama Mbunge wa Monduli  hususani katika utendaji wake  akiwa  Waziri  katika kuendeleza shughuli za kimaendeleo ya wananchi, za kikanisa.
Alisema kuwa wakati walipomuomba Lowassa  kuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo walitumia muda wa mwaka mmoja na hatimaye kupata majibu ya kukubaliwa hiyo ilitokana na shughuli mbalimbali alizokua akizifanya, ambapo walifurahia kwa kiasi kikubwa baada ya kukubaliwa hasa ikizingatiwa kuwa Babati sio jimbo lake la uchaguzi  lakini bila kujali amefanikiwa kuja.
“Tulikua na mashaka makubwa sana juu ya ujio wako kwani tunatambua kuwa una shughuli nyingi sana ikiwa ni ndani na nje ya nchi, hivyo ilikua ni vigumu kukupata kwa urahisi kwa lini kwa mapenzi yake Mungu leo tunashukuru sana kuwa wote katika shughuli hii kubwa iliyo mbele yako na tunadizi kukuombea ili mwenyezi mubgu azidi kukupa maisha marefu ili uweze kufanya kazi ya Mungu”alisema Laiser.
Hata hivyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuhakikisha kuwa wanaendeleza hali umoja ,upendo namshikamano  katika kuliendeleza neno la mungu  ili kuweza kuepukana na matatizo ya vurugu zilizotokea hapo awali baina ya dini na dini.
“Wapo watu wachache Tanzania wanaotaka kutuvurugia amani yetu tuliyonayo hapa Tanzania, kumbukeni tupende tusipende waislamu wataendelea kuwepo na tupende tusipende wakristo wataendelea kuwepo sasa ugomvi unatoka wapi badala ya kuishi vizuri kwa wema na upendo? Alihoji Laiser.
Akisoma taarifa ya ujenzi ,Katibu wa ujenzi wa jengo hilo Bw.Walter Ulotu,alisema jengo hilo kwa sasa limefikia hatua ya upauzi ,ambapokatika harambee hiyo jumla ya sh. sh.mil 120,000,000.
Bw.Ulotu alisema wazo la kuwa na jengo  kubwa  la kanisa lilianza 2007,baada ya kanisa lililopo sasa kuonekana kuwa ni chakavu na dogo ambalo halitoshelezi na waumini  waliopo  kwa wakati huu haswa ikizingatiwa kuwa lipo makao makuu ya Mkoa wa  Manyara,na hivyo ilionekana uwepo wa haja ya kuwa na jengo jipya la kanisa  la kisasa  zaidi litakalofaa wakati wa sasa na ujao.
Alisema hilo lilianza ujenzi wake rasmi mei 2008 mara baada ya  ya kupata kupata mchoro,vibali ,mkandarasi  na msimamizi (Architects), ambapo jengo hilo linakisiwa kuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya  watu wapatao 3000, ambapo hadi kukamilika kwa ujenzi huo zinahitajika zaidi ya sh.mil.600,000.
“Jengo hili hadi kufikia hatua hii ya upauzi  tayari zimetumiza zaidi y ash.mil.186.3, ambapo ili kzi hii iweze kuanza na kuendelea tunaomba Mungu ikimpendeza  leo tupate walao sh.mil.120,000,000 ,hatua nyingine katika ujenzi zitaendelea  kuwezeshwa na michango na harambee zitakazofuata” alisema Bw.Ulotu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda