Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, November 26, 2012

Kubadili Haiba,....I am tired of my Personality, Can I change it?


Na Nelson Faustin.
Kama kuna mwanadamu ambaye anapenda kuishi maisha ya "ukauzu" basi huyo anamatatizo na dhamira yake inakuwa imeshakufa kabisa. Suala la msingi hapa ni kuhakikisha kuwa, japo kuna vitabia fulani fulani katika haiba nyingine ambazo ni ngumu sana na zinaweza zikaleta hali ya kuchokwa na kuchukiwa na jamii kwa namna moja au nyingine ukajikuta unakuwa "kero kwa jamii". 

Hakuna mkamilifu wala hakuna ambaye anapenda kufanya jambo ili kuwafurahisha watu wengine bali tuishi maisha ambayo ni rahsi kuyafurahia. Ukitaka kujua kuwa wewe ni kero kwa namna fulani basi kuna viashiria ambavyo kama utaviona "do not ignore them" embu jaribu kufuatilia. 

Viashiria kama vile:-
 • Watu kukukwepa katika mijumuiko fulani fulani.
 • Kutoa maelezo au maelekezo ambayo no body will care about them as you thought.
 • Kukosa marafiki wa kudumu ambao watakuwa wanakushauri.
 • Kukosa watu ambao watakuwa wanakuunga mkono.
 • Kujenga jamii ya wanafiki ambao watakuwa wanakuzunguka kwa kujua au kwa kutokujua.
 • Kuonekana kituko katika kila mahali utakapo kuwa.
 • Ukiwa katika mazingira mageni, ni rahisi kupoteza thamani na kuonekana wa kawaida sana.
 • Utajikuta unafanya "defensive mechanism" kwa kuwa mkali au mnyonge sana.
 • Utajikuta unalipua majukumu yako. 
Kutokana na haya maisha yanakosa ladha hata kama wewe ni "kauzu" kwa kuwa tu ni mwanadamu, unahitaji sana kujifunza kwani mwisho wa siku wapo ambao wanaamua kuishi maisha ya kuigiza tu, au wengine wanaamua kuwa wapole kupita kiasi, au wengine wanaamua kujitenga na kuhamahama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, au pia kuwa na maisha ya kulalamika kila mara, wengine kama melankoliki wanaamua kujimaliza kwani maisha yanakuwa hayana maana tena kwao.

 
Kubadli haiba (change of Personality) ni jambao ambalo ukiamua unaweza kulifanya, kila kitu kinawezekana kama tu mtu ataamua kuona kwanza kuwa kuna sababu ya kubadillika bila ya kusubiri kusababishwa na mazingira fulani ambayo yatakulazimu kubadilika bila ya utayari wako, matokeo yake ni kuumia sana.

Kwa kuwa wewe si mnyama, unahitaji kwanza kusoma alama za nyakati ili uone kama kuna hali yoyote ya kuwa na kukubalika kwako, kama hakakuna, tafuta mbinu ya kujua namna ya kupambana na hali hii. 

Huwezi kubadili the real you lakini unaweza kuboresha na kuwa na lilmits kutokana na kuwa tabia ya asili inabaki, lakini unaweza kufahamu mapungufu yako na ukaweza kuyabadili. Uwe ni melankoli, flegmatiki, sangwini au Koleriki, unaweza kuboresha haiba yako.

 1. Jikubali the real you na mapungufu yako.
 2. Ainisha mapungufu yako yote.
 3. Kubali kurekebishwa pale inapobidi.
 4. Jali utu wa wenzako wanaokuzunguka.
 5. Tambua kuwa katika duania hii haupo peke yako wapo watu wengine ambao wanakuhitaji.
 6. Tambua mahitaji ya wengine hata kama hauta wasaidia lakini walau uwe katika nafasi ya kuwaonesha kuwa angalau umeona.
 7. Uwe radhi kujifunza lugha za tabia za wanadamu kama vile:-
 • Kuomba msamaha.
 • Kuwa na sikio la kukubali kuwasikia wengine.
 • Kuepuka maneno ambayo yataleta tafsiri ambayo si nzuri.
 • Kusema HAPANA mahali pa Hapna na NDIYO mahali pa Ndiyo.
 • Mahusiano ya wanadamu kutokana na umri wao.
Athari zipo nyingi na katika mjumuiko wa watu wa aina yeyote, lazima utakutana na watu wa aina mbalimballi, kwa mfano shuleni, ofisini, mahali pa biashara, mahalip pa ibada, nyumbani, nk, huku kote tunahitaji kuthaminiana kwani maisha yetu sote yanaanzia huku na hata kama unaakili kiasi gani, utajiri kiasi gani, familiya kubwa kiasi gani, bado unahitaji sana kutambua uwepo wa wengine kwaajili ya usitawi wako kimaisha. Acha maisha ya wanyama, wewe ni mwanadamu, ikikubidi kubadilika, badilika.......muda na uwezo unao.
 
Asante....


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda