Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, November 5, 2012

KIKWETE ANGURUMA BABATI: "NITAFUTA ASASI ZA KIRAIA ZINAZOPINGA MAENDELEO"

Mary Margwe
Babati
RAIS Jakaya Kikwete amesema atazifuta asasi za kiraia ambazo zinazochochea na kurudisha nyuma maendeleo nchini kwa kueneza fikra potofu na kupinga ujenzi wa barabara ya lami ya Loliondo-Mugumu wakidai kuwa itawaathiri wanyama waliopo mbuga ya Serengeti.
 
Akizungumza juzi wakati wa uzinduzi wa barabara ya Minjingu-Babati hadi Singida uliofanyika eneo la Sinai mjini Babati mkoani Manyara, Rais Kikwete alisema atachukua sita kuzifuta asasi hizo endapo hazitajirekebisha.
 
Alisema barabara hiyo ya lami itajengwa kwa lami maeneo ambayo hayapo kwenye hifadhi kwani watajenga eneo la Loliondo mkoani Arusha na Mugumu mkoani Mara huku wakiacha hifadhi ya Serengeti bila kuweka lami.
 
“Sisi tumeenda shule na tukaelimika hivyo hatuwezi kujenga barabara ya lami kwenye eneo la hifadhi ya wanyama ila tutajenga barabara hadi Loliondo nakuacha hifadhi na mkoa wa Mara tutajenga Mugumu,” alisema Rais Kikwete.
 
Alisema asasi hizo hata zikiendelea kupiga kelele kuwa barabara hiyo isiwekwe lami yeye atasimamia hadi kuhalikisha inawekwa lami ili kuunganisha mikoa ya Arusha na Mara bila kuathiri wanyama kwani haitapita katika hifadhi ya Serengeti.
 
“Suala hili lisifanywe la kisiasa kwa kutafutia kura na kutaka kuzorotesha maendeleo kwani kila mtu ana haki ya kupata maendeleo hivyo barabara hiyo itajengwa tu hata kama kuna watu wanaipinga,” alisema Rais Kikwete.
 
Alisema baadhi ya wafadhili wa nje walidai kuwa Serikali ina washinikiza kuwaondoa kwenye asili baadhi ya jamii zinazokula mizizi na matunda kwa kuwapeleka shule jambo ambalo ni kinyume na mila,desturi na utamaduni wao.
 
“Mimi niliwaambia miaka iliyopita hata sisi tulikuwa tunaishi hivyo lakini sasa wanatakiwa wabadilike siyo kuishi hivyo na wageni wawapige picha wakafaidi kwa kupeleka picha zao ngambo na kujipatia fedha,” alisema Rais Kikwete.
 
Naye,Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli alisema Rais Kikwete amejitahidi kwa kiasi kikubwa hadi kusababisha mikoa mingi kuunganishwa kwa barabara ya lami na juhudi hizo zinaendelea hivi sasa kwa maeneo yaliyobaki.
 
“Ujenzi wa barabara za lami uliofanikishwa na Rais Kikwete ingekuwa ni nchi jirani ya Rwanda hivi sasa wangekosa eneo la kulima mashama kwani kila sehemu ingekuwa lami tupu,” alisema Magufuli.
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema barabara ya Mirerani-Kia inatarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami hivi karibuni baada ya Serikali kutangaza zabuni ya kampuni itakayojenga barabara hiyo.
 
Rais Kikwete aliyasema hayo juzi mjini Babati wakati akizindua barabara ya lami ya kutoka Minjingu-Babati hadi Singida katika ziara ya siku mbili ya mkoa huo ya kutembelea wilaya za Babati na Hanang’.
 
Alisema kwa vile alitoa ahadi ya ujenzi wa barabara hiyo atahakikisha inamalizika ili kuwarahisishia usafiri wakazi wa mji mdogo wa Mirerani ambao wengi wao wanajihusisha na uchimbaji wa madini.
 
Akizungumzia kuhusu kukamilika kwa barabara ya Minjingu-Babati hadi Singida Rais Kikwete alisema lengo lake ni kuhakikisha kuwa barabara zote zinazounganisha mikoa ya Tanzania zinawekewa lami.
 
Alisema alipokuwa anatoa ahadi mwaka 2005 na 2010 baadhi ya wanasiasa walidai kuwa anadanganya wananchi kwa vile anaomba kura lakini hivi sasa barabara hizo zinakamilika na Rais ajaye ataunganisha barabara za wilaya.
 
Naye,Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli alisema barabara zilizojengwa nchini zinatokana na faida ya Rais Kikwete kuzunguka nchi mbalimbali kuomba msaada ambao umenufaisha wananchi wengi bila kujali itikadi ya vyama. 
 
“Rais ulipokuwa unazunguka kwenye nchi mbalimbali baadhi ya wanasiasa walidai kuwa wewe ni hodari wa kuzunguka dunia na sisi tunaona faida yake kwa hizi barabara hivyo endelea kuzunguka tu,” alisema Magufuli. 
 
Pia,Rais Kikwete aliweka jiwe la msingi kwenye barabara ya Babati-Kondoa hadi Dodoma kwenye eneo la Bonga ambayo itafika eneo la Moyamoya na Makutupora mkoani Dodoma.
 
Kwa upande wake,Mkuu wa mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo alisema barabara ya Minjingu-Babati hadi Singida imerahisisha shughuli za kiuchumi na maendeleo kwani kabla ya hapo usafiri ulikuwa ni tatizo kubwa. 
 
“Kabla hiyo barabara haijajengwa wakazi wa mkoa wa Manyara walikuwa wanapata shida hasa wakati mvua zinaponyesha lakini hivi sasa unaweza kufika Arusha kwa kutumia saa mbili na Singida unatumia saa tatu,” alisema Mbwilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda