Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, November 26, 2012

Kampeni ya Upandaji miti yafana Haydom

Na Amani Paul
Haydom
Tarehe 24 Novemba 2012 Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni Haydom yaani Four Corners Cultural Programme 4CCP ilizindua kapeni ya kwanza na ya aina yake kufanyika katika mji mdogo wa Haydom yenye lengo la kupanda miti na kuubadili mji wa Haydom kuwa wa Kijani yaani The Green Campaign.

Kampeni hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira ilizinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ndugu Anatoly Choya aliyekuwa mgeni rasmi ambaye alitoa wananchi kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kuitunza na kuilinda miti yote itakayopandwa wakati wa kampeni hiyo.

" Nitarudi baada ya siku 12 kuja kukagua miti hii tunayoipanda leo, na ninatoa agizo kwa viongozi wa serikali   wachukue hatua madhubuti kuzuia uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na mbuzi wanaozurura ovya na taka taka zinazozagaa katika mitaro" alisema ndugu Choya

Awali mkuu huyo wa Wilaya ya Mbulu aliipongeza 4CCP kwa kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo katika wilaya ya Mbulu na kuwaomba wazidi kushiriki zaidi na wasikatishwa tamaa huku akiwataka wananchi kuunga mkono juhudi za 4CCP katika kuleta maendeleo ya jamii
"Niwapongeze 4CCP kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya, sisi kama serikali tunawaunga mkono na tupo pamoja hasa katika jambo hili jema la upandaji wa mazingira ambalo linamanufaa kwa kizazi cha sasa na kile kijacho" Aliongeza Choya, "Naomba miche hii itunzwe, ilindwe na ithaminiwe, nikikuta hata mche mmoja umeharibika nitapambana na wahusika"

Akizungumza katika Kampeni hiyo mratibu msaidizi wa 4CCP Bi. Eliminata Awet kwa niaba ya Mratibu wa 4CCP Bi. Anna Kari Evjen Olsen ambaye naye alikwuwepo hapo aliwaomba wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti na kuepuka shughuli zote zinazochangia uharibifu wa mazingira hivyo kupelekea kuongeza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi

Kampeni hii ilihusisha shule za msingi Ng'wandakw na Haydom, shule za sekondari za Dr. Olsen, Mama Kari na Haydom, chuo cha Ufundi Haydom, madhehebu yote ya dini yaliopo Haydom ambazo ni Kanisa Katoliki, KKKT Haydom, TAG Ng'wandakw, Full Gospel Bible Fellowship, FPCT na Msikiti wa Haydom. Aidha wananchi mbalimbali walijitokeza na kushiriki katika zoezi hilo.

Wakati huo huo katika hali ya kushangaza, kampeni hiyo iliingia "mdudu" wa siasa baada ya mwenyekiti wa CCM kijiji cha Haydom Bw. Diamet kulalamika kwa mkuu wa Wilaya kuwa wao kama chama hawajaalikwa ilihali zoezi hilo linatekeleza ilani ya chama chake na hivyo kutokujitokeza katika shughuli hiyo kwa kuwa hana mwaliko hoja ambayo siyo tu iliushangaza umati wa watu waliokuwepo hapo kwa kuwa zoezi hilo halihusiani na siasa bali pia mkuu huyo wa wilaya "aliipotezea" na badala yake kuipongeza 4CCP kwa kazi kubwa na nzuri inayoifanya.

Lakini kama hiyo haitoshi, suala la mgogoro wa uongozi unaoendelea katika kijiji cha Haydom halikubaki nyuma na mkuu wa wilaya alitumia muda mwingi kuwaasa wananchi kufuata sheria za nchi na kutokufanya vurugu wakati wanadai haki zao na kuongeza kuwa yeyote atakayeleta vurugu atashughulikiwa kikamilifu.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda