Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, November 12, 2012

How Do I Improve My Personality? This is Easy if You will Agree to get the Pain of knowing The Negative Part of You.


Na Nelson Fautin
Baada ya kuona makundi yote manne tangu tuanze, na kujifunza mengi juu ya "Haiba", kujifahamu kila mmoja na kundi lake na kufahamu kwa undani juu ya tabia za mkundi yote "manne" yani Makoleriki, Maflegmatiki, Mamelankoli na Masangwini. Katika kufahamu mambo mbalimbali, kuna jambo ambalo linasumbua watu wengi sana kwa sasa kwamba, Je ni kwa jinsi gani naweza kubadili haiba yangu? Hii ni baada ya kujua kuwa, kuna vitu ambavyo umeviona huwa huvipendi kuhusu tabia ya maisha yako, ni kweli kuwa unapaswa kuamua kuwa, kila mtu anatamani sana kuhakikisha kuwa anaishi kwa kuwafanya wengine nao waishi kwa amani, katika hili ni "RAHISI" kubadili haiba na kuwa na tabia fulani bado ukiwa katika kundi lako.

Suala si kuhama kundi lako, bali ishu ni kulifahamu kundi lako na tabia zake na kuziboresha, ila kwa asili huwezi hama kutoka haiba moja kwenda kwenye haiba nyingine bali unaweza kuwa wa haiba fulani na ukazirekebisha baaddhi ya weaknesses ambazo unazifahamu zinakunyima amani, ufanisi na kukuweka mbali na watu. Kuna wakati fulani ambao utakuwa unaishi na watu kumbe kwa wakati woote watakuwa wanakuvumilia tu hapa na pale. 


Sasa, tunafanyaje?
 • Kwanza ya yote, weka uhalisia wa kukubali kuwa kuna kubadilika kama ukiamua kubadilika. Zaidi sana kubali dhahiri kuwa, kuna the "Negative side about you" na utahitaji KUUBALI NA KUBADILKA.
 • Jitambue kuwa upo katika kundi gani, na ufahamu kuwa unasifa njema zipi na mapungugu yapi. Hayo yote tumesha ainisha katika makala hii, ni kazi yako kufuatilia tulipoanzia hadi hapa tulipo.
 • Watambue wanaokuzunguka, baada ya kuwafahamu watakusaidia kujifahamu. Kila mtu ni sababu ya kukua kwako na kuendelea kwako. Kuwa tayari katika kupewa namna ya kubadilika kwako.
 • Kama upo katika kundi fulani, jitahidi sana kuzifahamu tabia mbalimbali katika kundi hilo ili ujue ni kwa wakati upi utaonyesha tabia za aina ipi kwani si kila wakati utaweza kuwa wa tabia fulani. Kwa mfano, wewe ni mkali (Koleriki) lakini unadili na watu wapole (Flegmatiki), itakubidi sana kuwa mpole ili mambo yaende.
 • Kama wewe ni kiongozi, ili uweze kuwaongoza wengine, jitambue baada ya hapo, ainisha watu wa timu yako kutokana na tabia zao ili wasikufanye ukakosa amani na ufanisi. Jitahidi sana kuwaangalia wale ambao una uhakika watakusaidia ili wawe karibu yako kukusaidia katika mapungufu yako.
 • Fahamu kuwa Tabia zako zinaathiri wengine hata kama hawakuambii, kwa maana hii, unatakiwa kusoma alama za nyakati kwa kuangalia "reactions" za wanaokuzunguka mara baada ya wewe kuongea au kufanya jambo fulani. 
 • Sema na watu wanaoweza kukusaidia katika kubadili haiba yako, omba ushauri au uliza kuhusu ni mambo gani ambayo yanakufanya uwe kero kwa wengine. Angalia mtu ambaye una uhakika kuwa hatakudanganya ili uangamie au mtu ambaye "atakuonea aibu au atakujibu kwa unafiki". Be ready to accept the reality hata kweli ukweli unauma sana.
 • Ainisha vitabia vyote vibaya, ishi ukiviua kimoja baada ya kingine huku ukijua kuwa huu ni mchakato utakao kuhitaji kwa muda wa kipindi fulani. Japo utaanguka lakini take time it is possible.
 • Acha kujifanya "Mr. Perfect au Ms. Perfect". Hii imewafanya wengi sana kushindwa kuishi na watu, utasikia tu mtu anakuambia, fulani ni mwache alivyo....hii ni mbaya sana.
 • Weka muda wa mabadiliko hayo. Kila baada ya kipindi fulani utajua ni jambo gani ambalo umelifanya na limekubadilisha kwa kiasi gani.
 • Kuwa wazi ili usaidike. Usiishi kwa kuigiza haiba fulani, hii itakuweka katika mazingira ambayo kwa nafasi fulani ambayo hutaweza kuwa "the real you" ambapo baadaye utasabisha uishi maisha ya kujilaumu sana.
 • Kuna tabia ambazo ni rahisi kuwa controlled, kama vile :-
 1. Hasira, 
 2. Kuongea kwa sauti ya juu. 
 3. Upole uliopita kiasi.
 4. Kutokuwa na mpangilio. 
 5. Kujiona wewe ndo unafahamu kuliko wengine.
 6. Kumiliki mazungumzo.
 7. Kiherehere. nk
 • Kuna tabia ambazo zinaweza kuchuka muda kubadilika, kama vile:-
 1. Kupenda sana uongozi kuliko kuongozwa.
 2. Kuweka sana vinyongo moyoni.
 3. Kukosa umakini katika kazi (Masangwini)
 4. Kuwa na misimamo isiyobadilika.
 5. Kuamini kuwa, You are always right.
Haya ni machache, bado tutajifunza zaidi na zaidi.

Mungu akubariki.
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda