Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, November 26, 2012

DC Mbulu aagiza Agenda zao Kuu iwe ni Mazingira


Na Mary Margwe,
Haydom
Kamati za maendeleo za kata (WDC) , Wilayani Mbulu Mkoani Manyara zimetakiwa kuhakikisha kuwa wanapofanya vikao vyao vya maendeleo agenda kubwa iwe ni namna ya uhifadhi wa mazingira ili kuweza kilinda na kutunza vyanzo vya maji, ambayo ni rasimilimali pekee ya uhai wa mwanadamu.
Hayo yalibainishwa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara Bw.Anatory Choya wakati akiwahutubia wananchi kwenye kampeni ya Upandaji miti  iliyofanywa na kituo cha pembe nne za utamaduni cha Haydom katika “4CCP GREEN CAMPAIGN” Mjini Haydom, iliyofadhiliwa na shirika la misaada la makanisa ya Norway (Norwegian Church Aid )
Alisema  ni vema wananchi na viongzi kwa ujumla wakahakikisha kuwa wakatumia muda wao mwingi katika kuzungumza ni namna gani wanaweza kuhifadhi mazingira, ambapo kamati za maendeleo ya kata  na mikutano mingine ya hadhara watendaji wa kata na vijiji wametakiwa kuhakikisha kuwa agenda kubwa iwe ni namna ya uhifadhi wa mazingira na si vinginevyo.
“Tunalishukuru shirika la misaada  la makanisa ya Norway  (NCA)  kutusaidia kufanikisha kampeni hii ni kitendo ambacho kinatakiwa kuigwa na watu wote wa hapa Haydom, nadhani tukifanya hivi kwa kila kaya mazingira yetu yatabadilika  na kuwa mazuri na ya kuvutia na hatimaye kunufaisha kizazi hadi kizazi kwani  iwapomazingira  tutayatunza kikamili nayo yatatutunza kikamilifu na si vinginevyo.” alisema Choya.
Alisema Serikali inapoteza fedha nyingi katika harakati ya kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapata maji safi na salama, na hivyo kupanda miti  sambamba na kuitunza ni ishara tosha kuwa uhifandi wa mazingira utaboreka na hatimaye kuipa urahisi Serikali juu ya upatikanaji wa maji.
Aidha alifafanua kuwa Rais Jakaya Kikwete aliwahi kusema kuwa asilimia kubwa ya uaribifu wa mazingira unasababishwa  na wanadamu, unahatarisha  vyanzo vya maji  na hivyo nchi itakua jangwa  na nchi itakua gizani.
Alisema kauli hiyo aliisema kwenye siku ya mazingira duniani iliyofanyika Mjini Moshi mwaka huu, ”sasa ni vema wananchi  kwa pamoja na kila kaya kuhakikisha kuwa tunaiunga mkono kauli ya mh. Rais wetu kwa kupanda miti kwa wingi na kuitunza  ili ije itusaidie baadaye kwa matunda ,kivuli  na hata kwa biashara na hatimaye kubadili pato la kaya   na Taifa kiujumla“ alifafanua Choya.
Aidha alisema kwa kuwa madiwani ndio wasimamizi wakubwa wa shughuli za maendeleo ya kata, aliwataka kuhakikisha wanasimamia suala la uhifadhi wa mazingira kikamilifu ikiwa ni sambamba na upandahi wa miti kama ya matunda na kivuli katika kila kaya  ili kuleta mabadiliko  ya mazingira bora na sio bora mazingira,ambapo aliwataka zoezi hilo kuwa endelevu.
Akizungumzia  hali chafu ya mazingira ya mji wa Haydom alitoa siku 12 kwa uongozi wa Tarafa, kata, kijiji na vitongoji kuhakikisha unakua safi wakati wote na sio wakati wa ujio wa viongozi  kwa kile alichokidai kuwa hali hiyo ya uchafu unahatarisha afya zao na hivyo wanapaswa kuchukua hatua hizo haraka iwezekanavyo ili kunusuru afya zao.
Akisoma risala ya kampeni ya upandaji miti inayofanywa na kituo cha pembe nne za utamaduni 4CCP GREEN CAMPAIGN”  kwa niaba ya Mratibu Mratibu Msaidizi  Bi.Eliminata Awet, Bw.Nelson Faustine alisema katika  kituo hicho kuna nguzo sita ambazo ni utamaduni, afya, mazingira, ustawi wa maisha,elimu na kusisitiza jamii juu ya uongozi bora .
Bw.Faustine alisema kampeni hiyo ya upandaji miti ni moja kati  ya nguzo  za kituo hiko  ambacho kina lengo la kuhakikisha kuwa suala la  mazingira linapewa kupaumbele  kutokana na umuhimu wake kwa mji huo wa haydom na taifa kwa ujumla.
Alisema katika suala la kutoa  elimu  juu ya mabadiliko ya tabia nchi  lengo kuu hasa likiwa ni namna ya kutafuta mbinu za kupambana na nayo ikiwa ni pamoja na utunzaji wa uoto wa asili  kwa kupanda miti  katika maeneo yanayowazunguka  na hivyo wao kuona wawe wadau wa kwanza kwa kuonyesha mfano mfano kwa vitendo  kwa kupanda  zaidi ya elfu 10, ambapo zoezi hilo litakua endelevu katika mji huo wa Haydom.
Hata hivyo alifafanua kuwa miti hiyo iligawiwa katia shule zote za msingi na sekondari, vyuo, makanisani,misikitini, mahospitalini, sambamba na  na viongozi wote wanaozunguka eneo hilo la Haydom ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anafahamu wajibu wake wa kutunza rasilimali mazingira ambayo ikitumiwa vibaya inaathiri jamii, ambapo juhudi hizo za pamoja zitaleta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda