Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, November 5, 2012

BREAKING NEWS: BALOZI WA NAMIBIA KUTEMBELEA HAYDOM NA YAEDA CHINI KUANZIA KESHO

Na Amani Paul
Haydom
Ikiwa ni miezi miwili toka Tamasha la kwanza kabisa laUtamaduni kufanyika katika mkoa wa Manyara na mikoa ya jirani likiwa na lengo la kuukuza utamaduni wa jamii za Haydom hasa Wahadzabe, Wairaqw, Wadatooga na Wanyiramba na Wanyisanzu, Balozi wa Namibia nchini Japhet Isaack atawasili Haydom kesho jioni (Jumanne tarehe 6 Novemba) na kisha jumatano ataenda katika bonde la Yaeda Chini kuwatembelea Wahadzabe.
Nyumba ya Wahadzabe

Taarifa zilizotolewa na afisa Ubalozi wa Namibia nchini Tanzania, zilisema kuwa Balozi huyo alipata habari kuhusu Wahadzabe ambao wanafanana mambo mengi sana na jamii ya kule kwao (bushmen) ambayo yeye ametokea kutoka kwa moja ya balozi hapa nchini na hivyo kuamua kuja kujionea yeye mwenyewe.

"Mheshimiwa balozi anapenda kuja kukutana na Wahadzabe, amesikia wanafanana mambo mengi hasa lifestyle(maisha), lungha na hata muunekano, hivyo anataka kuja kujionea kwa macho na ikiwezekana kuanzisha ushirikiano baina ya jamii hizo" alieleza afisa huyo.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuhusu Wahadzabe, Ubalozi uliwasiliana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kupitia RAS ndugu Bitekeko Kilangio ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Utamaduni la haydom lililofanyika kuanzia terehe 6 hadi 8 mwezi Septemba 2012 na kukabidhi jukumu la kuupokea ugeni huo kwa Kituo cha Utamaduni Haydom kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa WIlaya ya Mbulu.

Aidha DC wa Mbulu ndugu Anatoly Choya ameeleza kuwa Balozi huyo atafika kesho jioni na kulala Haydom, na kesho kutwa atatembelea Yaeda Chini kukutana na Wahadzabe na kuwa kila kitu kitaratibiwa na 4CCP.

Katika ziara hiyo balozi huyo atatoa misaada ya vitu mbalimbali kwa Wahadzabe ikiwemo chakula kwani kwa sasa jamii hiyo ambayo ni moja ya jamii yenye idadi ndogo zaidi ya watu nchini Tanzania inakabiliwa na baa la njaa.

Ifahamike kuwa, eneo la Haydom ni eneo pekee katika Afrika ambapo makundi yote manne ya Lugha za bara la Afrika yanapatikana katika sehemu moja. Makundi hayo ambayo ni Wahadzabe ambao inasemekana ni jamii Wakhoisan (bushmen) wa Jangwa la Kalahari kusini mwa Afrika, Wabantu (wanyiramba na Wanyisanzu na Wasukuma) wanaotokea Afrika Magharibi, Wakushi (wairaqw) kutoka pembe ya Afrika na Wadatooga ambao ni jamii ya Kinailitiki (wakiwemo wamasai, waluo n.k) wao wanatokea Sudan. Jamii zote hizi zinapatikana Haydom!

Kutokana na ugeni huo, Ohayoda imebaini kuwa ni moja ya mafanikio ya Tamasha lililofanyika miezi miwili iliyopita kwani Tamasha hilo liliandikwa katika vyombo kadhaa vya habari ndani na nje ya nchi ambapo Balozi wa Norway nchini Tanzania baada ya kuzisoma kwenye gazeti moja nchini Norway (Ohayoda ina nakala) alisambaza ujumbe kwa "contacts" wake wote nchini zikiwemo balozi mbalimbali na hivyo kuitangaza 4CCP, Haydom na Jamii za huku na kuwa Tamasha linalofuata kuwa na ugeni mkubwa zaidi.


3 comments:

  1. Good Amani you did well, God be on your way move forward. Makabila yetu sasa yatajulikana world wide especially Haydom our home land.

    ReplyDelete
  2. Haydom ni mahali pazuri sana na makabila ya Haydom na Singida ni kama makabila yaliyo kuwa yamesahaulika, ila tamaduni zao ni nzuri. Kweli alyemwinua Amani ni Mungu mwenyewe maana kupitia yeye tutajua utamaduni wetu, mila na desturi wenginee tumekulia huko lakini hatueleewi mambo ya mila na desturi zetu. Barikiwa sana Amani Mungu akutie nguvu.

    ReplyDelete
  3. Good Amani you did well, God be on your way move forward. Makabila yetu sasa yatajulikana world wide especially Haydom our home land.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda