Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, November 13, 2012

Breaking News: Baba ampiga mwanae na kumuua Kinyama

Mtu moja mkazi wa Kijiji cha Getarer kilichopo nje kidogo ya mjia wa Haydom Bw. Emmanuel Benedict mwenye miaka 33 anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Haydom kwa mauaji ya binti yake mwenye umri wa miaka 12.

Akiongea na Ohayoda mara baada ya kuhifadhi mwili wa marehemu katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Kilutheri ya Haydom, mkuu wa polisi Jamii tarafa ya Haydom A/Insp Mfero, amesema kuwa mtuhumiwa alimpiga marehemu usiku wa kuamkia jana hadi kufa nyumbani kwake huko Getarer na chanzo cha kumpiga bado hakijafahamika

Akieleza kuhusu tukio hilo, jirani wa mtuhumiwa ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema kuwa mtuhumiwa amekuwa akimpiga mara kwa mara mtoto huyo na kusababisha mtoto huyo kutoroka mara kwa mara hasa nyakati za jioni wakati baba yeke anaporejea nyumbani.
"Mara nyingi marehemu hukimbilia kwangu au kwa bibi yake na hukaa hata siku tatu" alisema jirani huyo.

"Siku hiyo mtoto huyo alikimbilia kwa bibi yake na mtuhumiwa kwenda kumfuata majira ya saa tatu usiku na kuanza kumpa kipigo kwa muda mrefu sana, zaidi ya nusu saa" kilieleza chanzo kimoja

Mdogo wa marehemu alieleza kuwa baba amekuwa akimpiga dada yake na hivyo dada yake kutoroka nyumbani kila mara, na hiyo juzi alimpiga kwa kamba ya tairi la gari (ipo pichani) kwa muda mrefu na kisha kumfungia ndani hadi alipofariki.

Habari zaidi zinasema kuwa marehemu alikuwa mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Endagew alipigwa na baba yake majira ya saa tatu usiku na kufariki saa kumi na moja alfajiri nyumbani kwao pasipo hata kupelekwa hospitali ambapo pengine asingefikwa na mauti.
Mama wa marehemu alipohojiwa na Ohayoda alisema kuwa mume wake alimfungia ndani na kumtishia kwa panga kama angepiga kelele kuwaita majirani na hakuwa na la kufanya hadi mauti yalipomkumba binti yake.

Mauaji hayo yamezua majonzi makubwa sana katika mji wa Haydom na vitongoji vyake kwani ni ukatili wa kiwango cha hali ya juu sana na kutaka mtuhumiwa achukuliwe hatua kali za kisheria huku kina mama wakimnyooshea kidole mama wa marehemu kwa kushindwa kuchukua uamuzi na kuokoa maisha ya binti yake.

Katika hatua nyingine, inasemekana kuwa mtuhumiwa amekuwa akimpiga mtoto huyo mara kwa mara kutokana na binti huyo kumsikiliza zaidi mama yake kuliko baba na inaaminika kuwa kabla ya kuolewa na mtuhumiwa, mama wa marehemu alikuwa na ujauzito ambao ulikuwa si wa mtuhumiwa na kupelekea mtuhumiwa kutokumpenda binti huyo.

Aidha A/Insp. Mfero ameeleza kuwa mauaji hayo yanatokana na mfumo dume ambao umekithiri katika jamii za huku kwani na tabia ya baadhi ya wazazi wanaoamini kuwa kumpiga mtoto ni kumrekebisha na kuwa ili mtoto akuheshimu lazima umpige.

"Haya ni madhara ya mfumo dume na imani potofu kuwa unapompiga mtoto unamnyoosha kumbe badala yake unamfanya awe sugu" alisema afande Mfero.
Inspekta Mfero alitoa wito kwa wananchi kutokufanya uhalifu na kutaka matukio haya yakomeshwe katika jamii.
Marehemu amezikwa leo nyumbani kwao Getarer na mamia ya waombolezaji wamehudhuria mazishi hayo huku mtuhumiwa akiwa bado yupo rumande na atapelekwa mahakamani kesho.Mwili wa marehemu ulipowasili kwenye Chumba cha kuhifadhi maiti HLH
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari la polisi huku mtuhumiwa (aliyekaa mwenye kofia) akiwa chini ya ulinzi mkali
Mtuhumiwa


Mtuhumiwa Emmanuel Benedict, 33
Tairi alilotumia mtuhumiwa kumpiga hadi kumwua mwanae

Mwili wa marehemu ukiingizwa Mortuary 
Mama wa Marehemu

1 comment:

  1. Afungwe kifungo cha maisha aliyesababisha kifo cha huyo mtoto. Kutoa uhai wa mtu ni kosa la jinai, Dah! Inaniuma sana maana mwanadamu hana mamlaka ya kutoa uhai wa mwingine.


    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda