Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, November 15, 2012

"As a Boss"...How do I know the Personalities of the people am Leading??

Na Nelson Faustin.
Ni jambo la kawaida kuwa, katika kikundi cha watu lazima utawakuta watu wa kada na hulka mbalimbali, dini, makabila, mitazamo, utendaji na hata uzoefu na uwezo wa aina mbalimbali. Hii pia inaingia katika suala la tabia tofauti tofauti katika maeneo ambayo wewe kama "boss" unaongoza na unhitaji kuzifahamu personality zao na uweze pia kudili nazo kiundani ili kuleta ufanisi zaidi. Hapa kila mmoja hana budi kumfahamu mwingine kwani katika sehemu za kazi kuna makundi yote manne na kila kundi lina faida na hasara zake na wewe kama kiongozi wa mahali hapo una kila sababu ya kujifahamu kwanza na kuweza kuwafahamu wengine pia ili muweze kuwa na ufanisi.

Sasa, katika hili, kila mmoja anapaswa kufahamu kuwa, hakuna mwanadamu aliyemkamilifu, na katika mapungufu yetu tunakamilishana, katika kufahamiana, tuna ikila sababu ya kuhakikisha kuwa kama wewe ni kiongozi, Know your team by using the following tips.

 • Ni lazima ujifatambue haiba yako kwanza ndipo utaweza kuzitambua za wengine.
 • Ni lazima pia uweze kujiongoza kwanza ndipo uweze kuwaongoza wengine. 
 • Tambua au ainisha "haiba" au Personality ya eneo unalolingoza, kama ni kanisa, sehemu ya burudani, ofisi ya fedha, shule au msikiti kwani sehemu pia hu-shape tabia za watu. 
 • Fahamu makundi ya muhimu katika kushughulika nao kwenye timu yako hasa Koleriki na Melankoli ambao ni wapinzani wazuri hata kwa mazuri. 
 • Weka mpango kazi ukizingatia sana haiba za watu katika timu yako. Proper fitting of Persons according to their personality.
 • Tambua maeneo yako yaliodhaifu, na uanishe aina za watu ambao watakusaidia katika udhaifu wako ili kuleta ufanisi. Usiwakaribishe watako kuvunja moyo lakini pia hakikisha kuwa hata wewe huwavunji moyo wale unaowaongoza.
 • Tumia maeneo yao dhaifu kuwapa hamasa, kuwapongeza, kuwashawishi ili kufikia malengo mahususi mliyokusudia.
 • "Avoid Labeling", ukiwawekea wat alama kutokana na madhaifu yao, ni kuwadhoofisha kisaikolojia na mwishowe inaharibu utendaji na ufanisi.
 • Fundisha timu yako juu ya haiba mbalimbali ili kuwasaidia kupata nafasi ya kujifahamu na kufahamiana vizuri.
 • Pata nafasi ya vikao vya mara kwa mara na ujitahidi kupata maoni na mapendekezo kwa watu tofauti toufauti katika kundi ili kila mmoja aone kuwa yeye sehemu ya jumuiya hiyo.
 • Weka sheria lakini wasaidie watendaji kufahamu kuwa, sheria si mzigo bali ni vidhibiti mwendo vya tabia ya binadamu, hivyo wasiigize maisha kwa kuzitii sana sheria kwa shurti. Hii  husababisha "iritation of the working enviroment"
 •  Ukifahamu kuwa wapo wenye haiba moja na hawawezi kufanya kazi vizuri, usiwaweke katika kitengo kimoja, kwa mfano, usiwaweke sanguine pamoja au Flegmatiki pamoja afadhali mamelankoli , hawa wakikaa pamoja japo watabishana lakini bado watafanya kazi vizuri.
 • Kila mara, weka timu pamoja.
Kwa kiongozi ambaye anajali zaidi utu, huyo atapata mafanikio makubwa sana. Kila mmoja wetu anapaswa kufahmu kuwa, watu si mashine na wana mahitaji ya kupendwa, kusikilizwa, kueleweka, kuonekana, kuthaminiwa na kupewa kipaumbele. Hivyo wana kila sababu ya kusikilizwa na kupewa kile ambacho wanakihitaji kwanza ili wafanye vizuri.  

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda