Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, November 20, 2012

ALAT yawataka wabunge wa Mkoa wa Manyara kuhudhuria Mikutano Majimboni


Na Mary Margwe, 
Katesh-Hanang
 
Wabunge wa Mkoa wa Manyara wametakiwa kuhakikisha kuwa wanahudhuria vikao mbalimbali vinavyoendelea katika majimbo yao, ili kuweza kubaini matatizo yanayowakabili wananchi wao na hatimaye kuyafikasha bungeni kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi stahili.
 
Hayo yalibainishwa jana na wajumbe wa  Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) Mkoa wa Manyara chini ya mwenyekiti wa ALAT, ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya ya Babati Vijini Bw.Nicodemus Tarmo, na katibu wake Mkurugenzi wa mji wa Babati Bi.Stellka Paschal, kilichofanyika katika Wilaya ya Hanang.
 
Kikao hicho cha AlAT kilifanyika katika ukumbi wa mikutano ya Halmashauri ya Wilaya hiyo, kikao ambacho kina jumuisha  viongozi wa Wilaya wa Mkoa mzima kama wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, wenyeviti wa Halmashauri na madiwani wawili kutoka kila Wilaya.
 
Jumuiya hiyo ya Serikali za Mitaa(ALAT) Mkoani Manyara, ilibainisha baadhi ya vikao vilivyodaiwa kutokuhudhuriwa na wabunge hao kuwa ni pamoja na huo mkutano wa AlAT na vikao vya baraza la madiwani, kwa kufanya hivyo kutasaidia kuchukua baadhi ya ya changamoto zinazowakabili na hatimaye kuyafikisha na kuyasemea bungeni.
 
Mkoa wa Manyara wenye wabunge 6 wa majimbo na wabunge watatu wa viti maalum, chakushangaza aliyehidhuria kiakao hicho cha ALAT ni mbunge mmoja tu  wa Bababti Vijijini Bw. Jitu Urajlal Soni
 
Aidha akijibu hoja hiyo ya kushindwa kuhudhuriwa kwa vikao kwa wabunge hao Bw.Soni alifafanua kuwa ni pamoja na taarifa kushindwa kuwafikia kwa wakati, na mafuta ya magari hoja ambayo ilizua mjadala mkubwa kwa wajumbe hao uliochukua takribani masaa 2 kujadili juu ya suala hilo la mafuta kwa wabunge hao.
 
“Wabunge wengine wanasema hadi sasa hivi hawajapata taarifa yoyote juu ya mkutano huu, na hivyo kusema kuwa wataalikwa kama watoto wadogo, hivyo ingependeza walau taarifa kama hizi zikiwafikia wabunge kama wiki mbili au moja kabla ya kikao husika, pia nitajitahidi kuhakikisha nitaleta ratiba ya vikao vya mwaka mzima vya bunge ili kuepusha tariba kutoingiliana na vikao vingine vya huku,hivyo ni vema taarifa ikatolewa mapema ili kuondoa malalamiko kama haya” alisema Soni.
 
Kufuatia sula la mafuta ya wabunge wengi wa wajumbe wa ALAT walitoa hoja ya kuwa kila jimbo watumie kusafiria gari moja kufika sehemu husika ili kuokoa gharama za mafuta, kwa kile walichokidai kuwa wakitumia usafiri fotauti tofauti watakua wakiziingizi hasara Halmashauri zao.
 
Kauli ambayo ilipingwa vikali na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Bw.Saimon Mayeye, aliyedai kuwa kitendo hicho si cha kiitifaki kwani kuchangia gari moja kunaweza kukatokea dharura ya gafla kwa baadhi ya viongozi na kutakiwa kusafiri, huku viongozi wengine watakua hawana usafiri.
 
Bw.Mayeye alisema kamwe mafuta ya wabunge hayawezi kurudisha maendeleo ya Halmashauri nyuma, ambapo alidai sula hilo linatakiwa kutafakari kwa kina na sio kukurupuka, kwani wabunge ndio wanaotetea hoja mbalimbali zinazohusu Halmashauri kule bungeni, hivyo ni muhimu wawekewe mafuta ili waweze kuhudhuria vikao.
 
“Suala la mafuta ya wabunge ili kuhudhuria vikao vinavyowahusu kamwe halitakwepeka kabisa" huku akitolea mfano wa wabunge wawili wa Kiteto kama Naibu waziri wa mifugo na Uvuvi Bw. Benedict Ole Nangoro na mbunge wa viti maalum Bi. Martha Umbula, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri, Mwenyekiti wa Hmlashauri, huku wakiwa na madiwani wao wawili kweli kabisa itawezekana vipi viongozi wote hao kusafiria gari moja eti kwa sababu ya kuogopa gaharama za mafuta hili haliwezekani kabisa kwani kunaweza kukatokea dharura yoyote ya kiongozi kutakiwa kusafiri wengine watasafiri vipi?alihoji Mayeye.
 
Naye mjumbe wa ALAT, Diwani wa Kata ya Endonyongijape Wilaya ya Simnjiro, Bw.Jacob Kimeso Lukendo aliitetea hoja hiyo kwa kile alichodai kuwa wabunge wanatakiwa kuwa usafiri wao tofauti na viongozi wengine kwani wao wanaweza kupitia kwa wapiga kura wao, na hivyo kushindwa kuwa huru katika utendaji wa kazi zao.
 
Bw.Lukendo alisema kuwa ni vema wabunge wakatafutiwa mafuta ili waweze kutumia magari yao badala ya kuchangia gari moja  huku likiwa na viongozi zaidi ya watatu, jambo ambalo linaweza kusababisha kutokea migongano isiyo ya lazima, hivyo matuta sio suala la kukwepeka kwa wabunge.
 
Aidha licha ya kutetewa kwa kauli hiyo lakini bado iliendelewa kupingwa na mjumbe mwingine Diwani wa kata ya Bonga Babati Mjini Bw.Pasian Siay aliwataka wajumbe hao kutokujikita zaidi katika suala la itifaki badala ya utekelezaji wa kazi ili kufanya kazi kwa ufanisi, kwani nyingi zinatumika kuliko ufanisi wa kazi.
 
Bw.Siay alisema kwa kuwa mikutano hiyo ni sehemu ya kazi zao wanatakiwa kuhudhuria vikao hivyo kwa gharama zao na sio kutegemea wawekewe mafuta na Halmashauri ambazo bado hali ya uchumi wake si mzuri, huku wajumbe wengine wamekua wakishindwa kuhudhuria vikao hivyo kwa kisingizio cha kuchelewa kwa taarifa, bila kujali kuwa rasilimali fedha za wananchi zinapotea na pia kupelekea kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.
 
“Rasilimali fedha zimekua zikipotea bila sababu, tunaomba taarifa ziwafikie wabunge wiki moja kabla, hebu tuanze kutenda ya matumizi ya rasilimali fedha kwani zinapotea bila sababu, kwani tunatumia rasilimali fedha vibaya sana na huku kushindwa kupeleka mrejesho kwa wananchi wa maazimio yaliyokua yamefikiwa”alisema Siay.
 
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Bw.Paulo Zacharia Isaay alisema kwa kuwa ALAT ni chombo ambacho kipo kwa mujibu wa sheria, aliwataka wajumbe kuhakikisha kuwa wanapotaka kutekeleza maazimio yao wahakikishe wanayaheshimu ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
 
Bw.Isaay alisema suala la wabunge kuhudhuria vikao ni la msingi kuliko wanavyorifikiria ama kulichukulia wengine kwa kile alichokidai kuwa baadhi ya maazimio yaliyoazimiwa yanatakiwa yachukuliwe ili wayafikishe bungeni, hivyo wanatakiwa kuhudhuria  vikao hivyo mara kwa mara watakapoarifiwa, kwani licha ya kuyafikisha bungeni pia wao wenyewe wanatakiwa kuyafahamu baadhi ya masuala mbalimbali yanayoendelea katika majimbo yao .
 
Aidha naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Bw.Anju Mangola alisema wabunge kupata mafuta katika halmashauri zao ni haki yao ya msingi ikiwa yapo la kama hakuna basi si tatizo kwao kwani  wakielezwa wataelewa namna halmashauri zao zilivyokua na hali mbaya kuliko kuendelea na mabishano ya muda mrefu.
 
Hata hivyo kikao hicho kilifikia muafaka kuwa Bw. SSoni ahakikishe anawapelekea ratiba ya vikao vya mwaka mzima vya bunge ili nao waweze kupanga ratiba zao bila kuingiliana ili wabunge waweze kuhudhuria vikao vivyo majimboni kwao, kuhusiana na suala la mafuta ya wabunge wamedai watalizungumzia wakati mwingine wabunge hao watakapofika wote katika kikao kitakachofanyika Wilayani Kiteto.
 
Akielezea baadhi ya changamoto zinazozikabili Halmashauri za Mkoa wa Manyara katika ukusanyaji wa mapato yake, kwa niaba ya katibu wa ALAT Mkoa Bi.Stella Paschal, mweka hazina wa AlAT Mkoa Bw. Paul Mamba Sweya alisema kuwa ni pamoja na viwango vya ushuru kutokuwa sawa  kwa halmashauri zote  za Mkoa wa Manyara na zile za Wilaya za jirani zinazoizunguka halmashauri zao.
 
“mfano ushuru wa gunia moja  la mahindi lenye thamani ya sh.60,000 katika halmashauri ya wilaya ya Babati wao hutoza sh.1500 huku wakati halmashauri ya mji wa Babati wao wanatoza sh.500 hadi 1000 tu! Jambo ambalo inatakiwa wawe na usawa katika utozaji wao wa ushuru” alisema Sweya.
 
Changamoto zingeni ni ukwepaji wa ulipaji ushuru kwa wafanyabiashara wa mazao kwa kusafirisha mazo usiku, hali hiyo imekua ikizikosesha kipato halmashauri, wafanyabiashara wanaonunua mazao ya chakula kutosajiliwa au kutokua na kibali cha ununuzi wa mazao wa mazao kutoka Halmashauri wakati wanakwenda kununua mazao kwenye masoko au vijijini kwa wakulima.
 
Aidha aliendelea kusema baadhi ya changamoto kuwa kuondolewa kwa baadhi ya kizuizi (vituo) cha kukusanyia ushuru wa katika baadhi ya vituo kufuatia kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw.Elaston Mbwilo aliyepunguza baadhi ya vituo huku akitolea mfano wa Dareda  kwa halmashauri ya Wilaya ya Babati.
 
“Wafanyabiashara kutokua na uelewa wa kutosha kuhusu ushuru  na ada mbalimbali za halmashauri na hivyo kusababisha ukwepaji mkubwa  mfano ushuru wa huduma kwenye hoteli za kitalii, baadhi ya viongozi wa ngazi ya msingi hawakuweza kupata elimu ya kutosha, hivyo kushindwa kuhamasisha jamii husika kuweza kulipa ushuru mbalimbali wa halmashauri kama ilivyokusudiwa.” alifafanua Bw.Sweya ambaye ni mweka hazina wa ALAT Mkoa wa Manyara.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda