Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, November 14, 2012

4CCP kufanya kampeni ya Upandaji miti "GREEN CAMPAIGN" Novemba 24

Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni Haydom (Haydom Four Corners Cultural Programme 4CCP) kinatarajia kufanya kampeni ya upandaji miti katika mji wa Haydom na vitongoji vyake tarehe 24 Novemba 2012 itakayowahusisha taasisi za dini (makanisa na misikiti), taasisi za elimu, serikali na wananchi wote
Kampeni hiyo yenye jina la GREEN CAMPAIGN ina lengo la kuufanya mji wa Haydom kuwa wa kijani kwa kupanda miti takribani 10,000 kila mwaka ikiwa ni sehemu ya shughuli za 4CCP katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi (Climatic changes mitigation).
Pamoja na kampeni hiyo ya upandaji miti, kituo hicho kinatoa elimu kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi kwa wanavijiji na katika shule mbalimbali za sekondari zikizopo katika wilaya za Mbulu, Iramba na Hanang ambapo wananchi wengi wamepokea elimu hiyo na kuifanyia kazi.

Katika kijiji cha Mazangiri wilaya ya Iramba pekee, wananchi wamekwisha kutengeneza majiko sanifu zaidi ya 100 na katika vijiji vingine 23 ambako 4CCP huendesha programu hiyo majiko mengi yamekwisha kutengenezwa ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa mkaa mbadala ambao unasaidia kupunguza matumizi ya kuni.

Majiko haya ambayo hutengenezwa na VICOBA ambazo zimeundwa na 4CCP katika vijiji hivyo tayari vimekuwa na mafanikio makubwa sana na kupunguza matumizi ya kuni na hata vijiji ambavyo haviko katika programu ya 4CCP vimeshiriki na kuanza kutengeneza majiko haya katika vijiji vyao.
Akizungumza na Ohayoda, Nelson Faustin ambaye anatoa mafunzo hayo vijijini na katika shule mbalimbali amesema kuwa wananchi wamepokea elimu vizuri na wanashauku ya kushiriki katika kuhifadhi mazingira
"Kwa kweli wananchi wengi walikuwa hawaelewi hili swala, lakini baada ya kuwaelimisha madhara ya uharibifu wa mazingira kwanza wengi waliogopa hasa walipojua kuwa kama hali hii haitadhibitiwa dunia inaweza isikalike baada ya miaka michache, lakini pia walipatwa na hasira kuwa ni shughuli za binadamu hasa viwanda ndiyo vinachangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia ya nchi" Alisema mwalimu Nelson
"Lakini wamepokea kwa shauku na tayari wameanza kuchukua hatua kwa kutengeneza majiko na pia kushiriki katika zoezi la kupanda miti" aliongeza Nelson
Aidha 4CCP imetoa zaidi ya Shilingi Milioni 15.8 kwa vijiji 5 ambazo zitatumika kujenga matenki kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua hasa katika maeneo yenye matatizo ya maji hasa shule na zahanati ambazo ni Mama Kari Secondary School, Shule ya Msingi Gidarudagaw, Zahanati ya Mongo wa Mono zote za wilaya ya Mbulu na shule ya Msingi Mazangiri wilaya ya Iramba. 4CCP imetoa fedha kwa ajili ya kununua saruji, nondo na gharama za fundi huku wananchi wakichangia nguvu kazi, mawe, mchanga, matofali na kokoto ambazo hupatikana katika mazingira yao.
Katika hatua nyingine, jumla ya Shilingi 120,000/= zilikusanywa papo hapo katika kikao cha wazazi wa shule ya Sekondari ya Mama Kari mara baada ya 4CCP kufika shuleni hapo na kuwapelekea mradi hua ambapo wazazi hao kwa pamoja walikubaliana kuchangia kila mmoja shilingi 4000/= ili ujenzi huo uanze mara moja na mpaka sasa mawe, matofali, kokoto na mchanga tayari vimekwishapelekwa katika eneo la ujenzi.

Hii ni sehemu ya shughuli za 4CCP ambapo pamoja na kuhifadhi tamaduni za jamii za huku, imekuwa ikisaidia kuleta maendeleo katika jamii kwa kutoa elimu hasa ya mazingira, elimu ya Haki Ardhi juu ya umilikaji ardhi vijijini, VOCOBA, Mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za Umma yaani Public Expenditure Tracking System (PETS), UKIMWI, haki za wanawake na madhara ya matumizi ya pombe. Na hivi karibuni programu mpya kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule za sekondari kujitambua na kufanya maamuzi sahihi ya kitaaluma (Capacity Building) na uundaji vikundi vya mazingira katika shule mbali mbali za sekondari ambapo mpaka sasa Shule za Sekondari za Dr. Olsen na Mama Kari zimekwisha kufikiwa huku shule za sekondari Yaeda Chini, Maghang, Haydom (Endagew), Basotu na shule zadhaa za msingi zitafikia hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda