Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, October 10, 2012

SIKITIKO LANGU.....Usifanye Kutokujua Kwa Wengine Kuwa Mtaji Kwako (They call it Negative Manipulation...)


(Sikitikolangu capt.)
Ni kweli kuwa, kila mtu anajua maisha ni zaidi ya kile tukionacho au kile tunachotamani kwani si rahisi kupata kila kitu ndio maana kila mara tunasisitizwa kumwomba Mungu kwani hatujui maisha yataendaje na yakoje…..lakini cha kusikitisha ni kwamba baadhi ya wanadamu wenzetu wametumia nafasi ya kutokujuakwa watu wenigine kwaajili ya kujinufaisha wenyewe…sawa inaweza ikawa ni ujanja wa kukuweka mjini lakini kiukweli wewe na mimi tuna kila sababu ya kufahamu kuwa si jambo jema na linaondoa uaminifu kati ya wanajamii….ni kweli kwa sasa hatuaminiani, si makanisani, si misikitini, si maofisini, si serikalini, si mahospitalini na kila sehemu ambayo sote tunazitegemea kwaajili ya kuweka maisha sawa…

Searching for opportunities, increasing capital,  searching for good life etc zimekuwa ni sababu ambazo zimeleta kitu ambacho ninakiita, “A point of Manipulation”, Manipulation is the point of taking someone’s IGNORANCE as an ADVANTAGE..

Aya hii iliyopita hapo juu nimeamua kuiandika kwa lugha ya kigeni ili kuliweka vizuri zaidi, kiuhalisia ni kwamba, watu wamekuwa wakitumia ujinga au kutokufahamu kwa watu wengine kama njia ya wao ya kujipatia riziki, si hivyo  tu bali hata kama njia ya kuwakandamiza kwa manufaa yao binafsi au kwa manufaa ya kampuni zao, nyumbani au ofisini nakadhalika.

“Experience” ni ishu ambayo wengi wetu tumeitumia kuwatesa sana wengine bila kukumbuka kuwa, kila mmoja wetu alianzia mahali Fulani, zaidi ya hilo kuna wengine ambao wao ni viongozi au wasimamizi mahali pa kazi na kuna haki ambazo waajiriwa wanapaswa wajulishwe bila kujali kama wanafahamu au la ili nao wawe sehemu ya ofisi hiyo lakini baadhi ya wasimamizi hutumia nafasi hii kumaliza juu kwa juu na wakati mwingine malipo ya muhusika huchukuliwa na watu wasiohusika. Tabia hii inaweza ikachukua kipindi kirefu kulingana na ushapu wa muhusika anayedhulumiwa bila kufahamu japo angepata fursa ya kufahamu isingemfanya kufika alipofika.

Nakumbuka rafiki yangu Fulani aliwahi kufanya kazi katika sehemu Fulani tena ya kanisa, na kwa bahati mbaya alianza  kazi akiwa katika kipindi kigumu sana na kwa bahati mbaya kutokana na ugeni kazini lakini pia kutokana na njaa ya kazi alipata kazi lakini hakuuliza maswala ya “salary scale na Pension na maswala yote ya Payee na mengineyo yahusuyo mikataba na usalama wake kazini”, na kutokana na hali aliyokuwa nayo “Uflegmatiki” hakuwa tayari kusababisha tafrani mahali pake pa kazi. Kwa takribani miezi sita alipata kufahamu kuwa,
  • Mshahara aliokuwa akilipwa si sawa kulingana na kiwango chake cha elimu.
  • “Benefits” zake kama mfanyakazi hakuwahi kuzipata kwa kuwa hakuwahi kuelezwa.
  • “Pension” hakuwahi kuandikishwa kwenye mfuko wowote wa hifadhi ya jamii kwani kwa kawaida mwajiri anakulipia 10% na mwajiri analipa 10% ila yeye hakuwahi kupata na kufahamu.
  • Alifanya kazi sana kwa bidii lakini kwa bahati mbaya ile “allowance pay” na “overtime” hakuwahi kulipwa japo hata chakula cha mchana wakati mwingine hakikuwa kinatolewa.
  • Cha ajabu pia ni kuwa, hakuwahi kusaini mkataba kwa muda wa miezi tisa na ikabidi asaini mkataba huo baadaye kwa kutumia mfumo wa “flashback” japo hadi mwisho wa mkataba alikuwa amezishisha miezi mitatu.
Na mengine mengi, lakini yote hayo alikuwa na fursa ya kufahamu toka kwa mwajiri wake na akafanya kazi bila wasi wasi. Huo ni mfano wa mtu mmoja ila wapo wengine wengi ambao wanafanya kazi au wanaishi maisha magumu sana lakini hawakustahili kwani siku zote si kila siyefahamu hawezi kufahamu. Unaweza kumwaficha lakini siku akifahamu inaweza ikawa mbaya sana kwako.

Kama mtu hafahamu kitu Fulani, usitumie kutokufahamu kwake kama chambo cha manufaa kwako, utafanikiwa leo kwa kutumia mgongo wake lakini BARAKA za Mungu kwako zinakuwa LAANA kwako, unajizibia riziki za hapa duniani kwa sababu ya kitu kidogo tu, ridhika na ulichonacho kwani ni Chako, usitamani cha mwingine.

Wengine huwazuia wengine fursa ya kufahamu kwani wakifahamu itakuwa ya “mshikemshike ndege tunduni”, mjinga mwerevu akijua huwa mwerevu kuliko mwerevu mwenyewe…..tuna kila sababu ya kuhakisha kuwa tunasaidiana. Mbali na kulifanya hili kama jukumu la kisheria lakini tulifanye kama jukumu la kila mtu kiubinadamu.

Naweza nikaandika sana lakini nimalizie kwa kusema kuwa, guys Manipulation Is baaaaaad, usikubali kufanya kazi na mtu ya aina yoyote mahali popote bila ya kuangalia sheria zinasemaje ili kuepuka migogoro baadaye, afadhali ukafahamu ukawa kimya ukisubiri wakati mwafaka kusema kuliko kutokufahamu kabisa. Kwa uzoefu wangu ni kuwa, makampuni mengi yamepotea, mashirika mengi yamekufa, migogoro ni mingi majumbani na makazini kutokana na tatizo hili la “manipulation”. Tuthaminiane, tusaidiane, tuelekezane kwa upole…maisha haya bila umoja ni ngumu sana….

Juma lijalo nitaongelea “positive and negative manipulation in Relationship”

Do not use other people’s Ignorance for your own advantage, give them knowledge so that you help them see the truth and if they do not realize, that will be their own disadvantage.
Nelson Faustin Ndelemo-Tanzanian

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda