Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, October 30, 2012

Papaa On Tuesday...Usichukue Maamuzi ya Kuwajeruhi Wengi Wanaokupenda sababu ya mmoja Aliyekujeruhi.


Ikiwa leo tunaumaliza mwezi wa October na kuukaribisha mwezi wa November kisha December mwaka uwe umekwisha tunakila sababu ya Kumshukuru Mugu kwa ajili ya fadhiri zake na wema wake kwetu kila ainapoitwa leo.
Zangu salamu ziwafikie wasomaji wote wa Papaa On Tuesday ambao wiki iliyopita wakati tunaongea kuhusu sauti ya ndani waliwasiliana nami juu ya mada ile Mungu wangu na awabariki sana. Wiki iliyopita wakati nimeanza kuandika mada hii ya leo ya Let It Go, ghafla moyo ukanielekeza niandike Papaa On Tuesday ile iliyopia kuhusu sauto ya ndani nami nikatii sauti ya ndani nikamwaga maneno kama kawaida, leo moyo wangu na miko yangu imepata kibali cha kuituma mada hii ya "Let It Go".
Mara nyingi sana kwenye maisha kuna watu wapo wa aina mbali mbali, kuna wanaojali hisia za wengine na utu wao na kuna watu ambao wao furaha yao ni kuona machozi ya wengine yakitoka. Watu wengi kwenye maisha wame experience kuumia kwa namna moja ama nyingine, wengine wamejeruhiwa na mapenzi, wengine wamejeruhiwa na waajiri wao, wengine wamejeruhiwa na wafanyabiashara wenzao, wengine wafanyakazi wenzao na wengine wamewahi jijeruhi wenyewe...mmh hivi inawezekana kujijeruhi??ndio inawezekana kwani we hujui kuwa kuna watu waliwahi kujikosea na hawajajisamehe kila akikaa picha inamjia alichokifanya anakosa amani na raha, Mungu naaweza kukusamehe, watu wanaweza kukusamehe kuna ngoma zingine inapaswa ujisamehe mwenyewe ili maisha yaweze kusonga.
Kuna tabia nyingi sana ambazo tunazo kwenye maisha zinajengwa ama zinazaliwa baada ya mambo kadha wa kadha kutokea kwenye maisha yetu. Ndio maana kuna msemo wa kiswahili aliyeng'atwa na nyoka hata akiona unyasi anastuka. Ukisoma vizuri utaona kustuka ni tabia iliyozaliwa baada ya kung'atwa na nyoka yamkini huyu mtu hakuwahi kustuka stuka hapo kabla. Kwenye kizazi chetu kuna tabia ya chuki, kuto kuaminiana, kuhujumiana na pengine wivu wa kupindukia si kwa sababu ya mapenzi ila tu ni kwa sababu ya Jeraha mtu alilowahi kulipata kwenye maisha yake. Kuna watu waliamua kuwachukiwa watu wa kundi fulani sababu tu kuna mtu aliwahi mjeruhi ama watu wachache waliwahi mjeruhi. Kuna mtu anaweza sema Chama Fulani hakifai si kwasababu kweli hakifai ila tu Kuna jereha la nafsi huyu mtu analo dhidi ya Chama Fulani. Kuna Wanawake wengi sana kwenye Kizazi chetu ambao wao wanaamini kabisa Wanaume Wote Wanafanana, na Kuna Watu Wako Tayari kuwa na Watoto lakini sio Waume wa Kukaa nao kwenye maisha sababu tu kuna mtu amewahi mjeruhi nafsi yake, Kuna Mtu amewahi mtwaa mke wa mtu ama mke wa mtu kuanzia hapo jeraha la nafsi halijapona, kuna watu wamewahi waona wapenzi wao wakiwasaliti kwenye maisha jambo lilitokea miaka ama miezi imeisha na kana kwamba mmesameheana lakini Letting It Go sio jambo rahisi. Unatamani kuachilia lakini bado moyo una ukakasi.
Usitoe ahadi kwa watu ukiwa siku umefurahi sana, ama usichukue uamuzi siku ukiwa na hasira sana sababu matendo hayo unayafanya ukiwa hauko normal, siku ambayo utakuwa normal ndipo utagundua maneno uliyoyasema yanauzito kiasi gani. Kuna watu aliamua kwneye maiusha yao kuchukia wanawake wote duniani na wengine kutokuwaamini wake zao kisa na mkasa eti wanawahisi ok inawezekana hujamuhisi una uhakika kabisa na kosa alilokufanyia huwa najiuliza inakusaidia nini kuliweka jambo moyoni muda mrefu??Wiki Iliyopita nilikuwa naongea na mtu kwa simu akiwa anaomba ushauri kwangu katika mazungumzo akasema Ninawachukia Wanaume Ninawachukia Kupita maelezo na aliongea huku akiwa na hasira sana. Nikamuuliza Umeanza kuwachukia lini na kwanini. Akasema tangu mwaka 2010 baada ya Mwanaume wa Tatu kuniacha solemba baada ya kunichezea. Nikamuuliza Umewahi kujiuliza Kwanini Wanaume wote wamekukimbia??nikamuuliza tangu umeanza Kuwachukia wanaume 2010 umesaidika na nini kimaendeleo kwa kuwachukia, kwa maana kwamba kupitia chuki kuna hatua umepiga. Unaweza laumu kila mtu kwenye maisha kwa kukusababishia matatizo ama uwe hivyo ulivyo. Inawezekana kweli unahasira sana lakini maisha lazima yasonge kukasirika na kuwa na vinyongo hupelekea visasi. Usichukue Uamuzi wa Kuchukia Wanaokupenda  Kwa sababu ya Mmoja aliyewahi kukuchukia ama kukumiza kwenye maisha.
 
 
Mmoja wa wamarafiki zangu wa kike wiki iliyopita alinipigia simu huku akilia akitaka kuacha kazi baada ya manyanyaso ya boss wake mwanamke kila kukicha. Kila analofanya la heri linakuwa Kero amemkalia kooni sana na siku hiyo huyu Boss alimenenea maneno magumu sana ambayo alishindwa kuyastahimili kama mwanadamu naye akafunguka tena alifunguka kwa volume kubwa ndipo boss nae akafunguka kwa Sub-woofer kwa sauti kubwa zaidi mpaka huyu dada akatoa machozi. Kumbe si mara ya kwanza huyu mdada kufanyiwa hivi na boss tayari ana jeraha juzi ilikuwa ni kama kulitonesha jeraha la awali. Huyu mdada anasema hawezi kufanya kazi sehemu yoyote ambayo boss ni mwanamke kisa na mkasa boss wa sasa ni tatizo. 

Usichukie kila mtu kwenye maisha sababu kuna mtu aliwahi kufanyia jambo baya. Huwezi ku Generalize kuwa watu fulani ni wabaya kwa experience ya watu wawili watatu kwenye uwigo unaouongelea. Kama kuna Jeraha Let It Go. Kumchukia mtu ama kundi la Watu ambao wao Wanaendelea vema na mambo yao ni kijirudisha nyuma, utajikuta wakati unaotakiwa kupenda wewe bado una jeraha, wakati unaotakiwa kufanya kazi kwa uhuru unashindwa sababu ulishazoea kukosolewa. Fungua ukurasa mpya kwenye maisha sahau yaliyopita kanyaga twende mbele na maisha ya kila siku. Kuchukia watu sababu ya mmoja aliyekujeruhi itakugharimu. Kuwa Muangalifu sana na maneno unayoyasema kutokana na bad experience kwenye maisha. Unayoyasema ujue unaumba, Ukisema Wanawake wote ni vimeo duniani basi ujue kinywa chako kinatengeneza Vimeo. Ukisema Ninawachukia watu fulani basi ujue umefungulia mlango wa chuki kwenye maisha yako. Kama unaweza kaa na mtu muyamalize kwa amani Utapata maradhi bure katika mwili wako kwa hasira zako duniani wakati unao wachukia ndo kwanza wananenepa zao. Let It Go Chapa lapa.  

0713494110
Papaa Ze Blogger

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda