Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, October 16, 2012

Papaa On Tuesday.....Unakokwenda Inategemea Sana UlikotokaZangu pole nataka kuzipeleka kwa ndugu zetu wa Mbagala waliopata usumbufu na uharibifu wa mali zao kufuatia kitendo cha wiki iliyopita siku ya Ijumaa. Poleni sana ndugu zetu wa TAG, KKKT na Adventists kwa kuharibiwa makanisa yenu. Bado Tanzania ni Nchi ya Amani, ingawa wapo wanaotamani kuwepo na vita. Maana kila unalolikiri ndilo unalolipata. Blog inatambua fika Tanzania ni nchi ya Amani. Tunakokwenda huko inategemea sana na tunakotoka maana hapa tulipo ni matokeo ya kule tulikotoka sisi kama Watanzania. Kuna mambo tuliyaruhusu tulipokuwa na wakati wa kuyaruhusu ama kuyakataa, hakuna ambalo linatokea kama hatukutoa mwanya wa hayo yote kutoke.

Hapa tulipo ni matokeo ya tulikotoka kama Taifa, Taaluma uliyonayo ni matokeo ya shule uliyosoma,maisha unayoishi ni matokeo ya msingi uliyojijengea kwenye familia, kwenye mahusiano, kwenye biashara na kwenye maisha ya kawaida, kuna mwanya uliuachia ambao either utakupa matokeo hasi ama chanya, kuna tabia tunazo zinatokana na mwanya tuliouacha kwenye Jamii yetu.
Nimekuwa nikihudhuria midaharo mingi sana na semina mbalimbali miaka ya hivi karibuni na nimebaini jambo moja kwa mtazamo wangu asilimia kubwa wanaongea kuhusu "future". Asikuambie mtu future inatisha ndo maana hata mitaani wanasema "Fainali Uzeeni". Motivational Speakers wengi wetu tumejikita na watu kujipanga ki akili na Kimaamuzi kwa maisha yajayo, hata Papaa On Tuesday inatuelekeza huko huko hata vitabu vitakatifu Kuran na Biblia vinaongelea maisha yajayo, kila mahali ni future future future chezea future. Lakini swali la Kujiuliza Future inaanza Lini???miaka 10 iliyopita yamkini tulisema miaka 10 ijayo itakuwa a,b,c ukadhani ni mbali ghafla hii hapa ukipima graph yako ya maendeleo imepanda, imeshuka ama iko pale pale na Je kupanda kwake inapanda kwa speed gani??Maendeleo ni maendeleo inawezekana ukaendelea kurudi nyuma na ukaendelea kwenda mbele lakini Unakokwenda inategemea sana ulikotoka.

Maisha ya Watanzania wengi hasa wale wa tabaka la chini sio wanaosoma Papaa On Tuesday, Sio wanaokwenda facebook, sio wanaosoma magazeti "Serious" sio wanaofatilia nini kinaendelea, wengi wetu sisi wa Tabaka la Kati ndio tunaowasaidia hawa wa Tabaka la chini, hawa ndio tegemezi ingawa pia wapo tabaka la kati ambao pia ni tegemezi, kipato tunachokipata ndicho kinasomesha wadogo zetu, ndicho tunachowasaidia wazazi wetu, kipato tunachokipata hakikai, leo unapata unga unagundua mchele umeiesha, unapata mchele unagundua hujanunua kitabu cha mtoto, unanunua kitabu cha mtoto unagundua kuna mchango wa harusi wa ndugu yako kabisa hujatoa, unajikuta unatamani kwa siku kuwe na masaa 29 siki iwe na siku 13. Ajabu katika masaa hayo hayo 24 kuna watu wanatamani yapunguzwe yako mengi sana maana wao wanalala tu kila kitu "Wanasubiri".

Hili ni Taifa lililojengwa "Kusubiria". Tunasubiria Tume ituambie hata kama Ukweli tunaujua. Mtu akimaliza Shule Mitihani yake hata Chuo Kikuu mfumo unamwambia anapaswa "Kusubiria Kazi". Atakaa nyumbani kana kwamba Kazi zinawatafuta wao. Kuna watu hawajisikii vibaya maisha ya Kukaa tu "Kusubiria". Kuna wengine wanasubiria ndugu zao wawape Mitaji, Kuna Watu Wanasubiria Ndugu zao Wawatafutie kazi, Kuna Watu Wametuma barua zao Wanasubiria Majibu, Kuna Watu Wameomba likizo ofisini kwao Wanasubiria Boss wao ajibu, Kuna Watu Wanamatatizo kwenye ndoa Wanasubiria Kikao, Kuna Watu wamefanya kazi na kampuni fulani Wanasubiria Malipo. Tunakokwenda Inategemea sana tunakotoka na hasa tulipo.

Tuko hivi tulivyo leo kutokana na mchanganyiko wa mambo mengi. Watanzania ni Taifa ambalo tunaujua ukweli wa jambo na tunaamua "kusubiria" mwisho wake. Utasikia mtu anasema we subiria tu mpaka mwisho utaujua ukweli, hata kama huo ukweli anaujua still bado atasubiria. Hakuna wa Kumlaumu kwenye maisha yetu ya kila siku kila mtu anawajibika na maisha yake mwenyewe. Kila tabia tuliyonayo iwe ya heri ama shari ni matokeo ya  mlango tulioufungua katika maisha kuna nanafasi uliiachia mambo yakawa kama hivi yalivyo sasa inawezekana ni kimwili ama kiroho.

Wiki iliyopita nilikuwa ninatazama Filamu ya Marehemu Kanumba yenye Jina la Ndoa Yangu. Katika Filamu hiyo inaonesha kulikuwa na changamoto nyingi sana za wanandoa walioshiriki, lakini mwisho wa siku utagundua kuna "mwanya" kuna "mlango' ambao wanandoa waliufungua kwenye ndoa yao ikawa na misuko suko. Chochote ambachpo kinaendelea leo kwenye maisha kuna mahali ulifungua mlango na ikawa. Pengine tumeshindwa kupiga hatua kwenye maisha yetu sababu kuna mlango tumeufunga. Sio vibaya kutokuwa na marafiki kwenye maisha, na sio vibaya pia kuwa na marafiki pia sasa kuwa na marafiki ama kutokuwa nao inategemea na mlango ulio ufungua ama ulioufunga kwenye maisha yako. Maana ikifika mahali unahitaji marafiki unahitaji watu unagundua kuwa huna hao unao wahitaji ndipo unagundua hukuwahi kufungua huo mlango.

Ukimuona leo mtu anatabia yoyote kwenye maisha iwe ya ukahaba ama tabia nzuri kumbuka kuwa kuna siku alifungua mlango wa hiyo tabia. Kwa wale waliowahi na wale ambao wanakunywa pombe watakuambia vizuri siku ya kwanza kunywa wengine ilikuwa ni chungu, ilikuwa ni mbaya once walipofungulia mlango wa ulevi na unywaji mpaka leo wamekuwa hivyo walivyo, tunapokwenda kwenye maisha inategemea sana tumetoka wapi. Kwenye mapenzi kuna watu wengine wanafurahia wengine wanaumia na kama kuna shida yoyote imewahi kutokea kwa wanandoa ukianza kuwashauri swali la kwanza mara nyingi utasikia "haya mambo yameanza lini", mwingine anasema "amebadilika sana siku hizi" utagundua kila tabia mbaya kwenye mapenzi na kwenye maisha ilifunguliwa mlango ikaingia na kuna sababu iliyopelekea kuingia kwa kila tabia mbaya ama nzuri. Tunakokwenda inategemea sana na tulikotoka na tulipo.
Kama nchi kama Kanisa tupo hapa tulipo kutokana na yale yaliyopewa nafasi miaka ya nyuma. Ufisadi umefika hapa kutokana na mwanya uliokuwepo, tofauti za madhehebu zimefika hapa kutokana na mapengufu yaliyokuwepo, watoto wako walivyo leo kutokana malezi na makuzi. Inawezekana mtoto ni lege lege ama mkomavu wa mawazo sio kama ajali ila aliyoyapa nafasi kwenye maisha. Wengi wetu leo tuko tulivyo hata kujieleza hatuwezi kwa sababu ya woga tuliouruhusu. Mwanaume ama Mwanamke uliyenaye anayafanya hayo anayoyafanya sababu ya msingi mlioujenga. Nothing happened accidentally kuna mwanya kanafasi kakipatikana tu linakupata linalokupata.
Haya tunayiyasikia siku ya leo ya Waislam kuchoma makanisa ni matokeo ya mianya iliyoachwa either na Kanisa ama Serikali, na tunakokwenda kama Tanzania inategemea sana na tunakotoka. Leo hii Misri Serikali Ikiyumba tu kidogo wananchi wanenda kwenye ile "freedom Square" yao ambako walipindulia serikali iliyopita. Pale ndipo wamejenga madhabahu ya mapinduzi.We hujawahi kuona mtu ulimfanyia kosa zamani pengine mpenzi ama mwajiri ama yeyote, na ukadhani mambo yameisha kabisa, kila inapotokea nafasi anakukumbushia kosa lako, na ukikumbushwa kosa lako unajikuta unakosa raha kabisa na ujasiri wa kuendelea kufanya ama kusema. Kuna rafiki yangu alikuwa na Mke wake ambaye walikuwa na raha na amani ikatokea miaka imepita hawajapata mtoto, walipoenda kwa daktari kwa uchunguzi ikabainika kuwa mdada kizazi kimeharibika kutokana Sarakasi za Ujanani, na yule mkaka hakuwa akilitambua hilo kwanza. Basi kila Wakikaa Mdada akitoa wazo, mkaka anachomekea "Yaani ungekuwa hujaharibu Kizazi tungekuwa na watoto saa hizi Wawili" yule mdada anaumia sana, anajijutia makosa yake anaomba msamaha na kumwambia kwa Mungu yote yanawezekana. Yanakuwa kama yameisha, siku mkaka akikasirika utasikia "Ungekuwa hujachezea kizazi chako, Saa hizi tungekuwa mbali" au wakiona familia ina watoto basi mkaka anamwambia mdada "sio unaona wenzio waliojitunza". Yule mdada akajiuliza hivi hali hii mpaka lini???safari ya ndoa ikaishia ndani ya miaka sita tu, walipokuwa ilikuwa inategemea sana kila mmoja wao alikotoka.
Kuna mambo kadha wa kadha ambayo mtu anaweza kuyafanya sasa akatengeneza ule mwanzo mbaya aliyokuwa nayo hapo awali ambayo mengine yamemletea doa la kwenye maisha, kitaaluma na hata kiroho. Kuna mbambo kadha wa kadha pia ambayo mtu anaweza kuyafanya leo ili asifungulie mlango mambo ambayo hayana faida kwenye maisha. Kuna wengine kile siku wanshindwa kwenda mbele sababu ya kitu kimoja ama viwili, wengine wamekosa maendeleo kwa sababu moja tu ama mbili leo hii wangekuwa mbali sana kwenye maisha lakini tangu walipofungulia mlango wamejitahidi kuufunga wameshindwa. Jiulize nini umefungulia mlango na kukuacha katika hali uliyo nayo. Unakokwenda Inategema Sana na Unakotoka.

Ze Blogger
0713 494110.

1 comment:

  1. Hii article ni nzuri sana, imenipa point moja muhimu sana - Kumbe kila kitu kilichokutokea au kinachokutokea sasa hivi ni kwa sababu umejifungulia mlango mwenyewe jambo hili kwa kuliruhusu.... je mtu atajienguaje? akifunga mlango itasaidia sasa?

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda