Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, October 9, 2012

Papaa On Tuesday....Ukizimia Siku Ya Taabu Nguvu Zako ni Chache--2


Ingawa nimekuwa nikiandika Papaa On Tuesday kila Jumanne, lakini kuna POT ambazo hata mimi mwenyewe huwa nina zi feel sana kwenye maisha yangu. Kila Moja inauzito wake lakini kuna Papaa On Tuesday ambazo nakumbuka niliziandika huku Machozi yakinitoka sababu ya memory zilizokuwa zikipita kichwani kwa kadri nilivyokuwa nikiandika na kuzisoma.

Kati ya POT hizo mojawapo ni hii ya Kuzimia Siku Ya Tabu. Unajua unaweza ukawa unajiona ngangari, unaweza kutatua matatizo ya watu, unaweza ukawa pouwa tu na ukaonekana stable kumbe bana hujakutana na jambo la kukutikisa. Ukipata jambo la kukutikisha ndio utajua how strong uko. Tatizo ama matatizo wakati mwingi sana hudhihirisha tabia zetu zingine zilizojificha. Inawezekana ukadhani mtu hana hasira kumbe hajapata fursa ya kukasirika, unaweza dhani mtu hana matusi kumbe hajapata mazingira ya kuropoka tusi, unaweza ukadhani Jamaa Mwaminifu kumbe hajapata mazingira ya Usaliti. Ukitaka kupima nguvu zako ni chache ama nyingi uwepo kwenye mazingira yaliyokuwa yana ku favor asilimia mia nane kisha ukachomoka salama. Ulikuwa na Uwezo Wote tena pasipo kutumia hata nguvu kidogo kutenda uovu lakini ukajiepusha nao.
Ni rahisi sana kuwanyoshea wengine vidole pasipo kujua sababu iliyopelekea mtu kuamua kile alicho kifanya. Nimewahi kukutana na watu wengi sana wanaojutia kile walichokifanya baada ya kukifanya sio kwamba walipenda kufanya. Mimi sina tatizo sana na kile walichokifanya ila nina tatizo na Uwezo wa Wao kutokurudia kufanya. Rafiki yangu Mussa aliwahi sema Watu wengi sana wanatumia nguvu kuzuia kuanguka kuliko kujipanga kimtazamo kuwa Nitasimamaje mara baada ya kuanguka katika Maisha. Kuna watu wameanguka kibiashara nba kushindwa kusimama tena, kuna watu wamewahi anguka kwenye mahusino. Kuna watu wamewahi kuanguka kimasomo, kila mtu ana namna yake ya kuanguka. Issue inakuwa what next baada ya issue kutokea. Unajipangaje upya baada ya KUHARIBU. Niliwahi andika Papaa On Tuesday Mwanzoni mwa mwaka huu kuwa ukiona Unajipanga Ujue Ulipanguka. Jipange Sawa Sawa Kuvunjika Kwa Koleo Sio Mwisho wa Uhunzi. Ukizimia Siku Ya Tabu Nguvu Zako Ni Chache.


Maisha yetu ya kila siku yamezungukwa na changamoto zisizo na Idadi, na mfumo wa maisha tuliyokulia wengi hayakutupa fursa ya kukabiliana namna ya kutafuta fumbuzi ya changamoto hizo. Tangu utotoni chochote kilichokuwa kinatukabili tunawaeleza wazazi, pensel ikipotea tunamwambia mama, wakati wa likizo tunaomba hela ya tuition, tukiwa shule swali likitushindwa swali la hesabu mwalimu atafanya kwa niaba yetu, kama kuna mwanafunzi machine kama Mozes Mwizarubi, basi tunampelekea yeye “atufanyie” Maswali na pengine tuna submit na kweli tunawekewa pata…matokeo yake mambo yote mepesi tuliokuwa tunafanya wenyewe yale yenye kutuhitaji tutumie akili zetu tuliwapa wengine,tukafaulu, tumeanza kazi na wengine tunafamilia, je kwa sasa yakija magumu tunapeleka wapi?hapa ndo kuna maturity ya mtu. Nakumbuka kila baba alipokuwa hana hela anasema subiri nirudi kutoka mjini, au njoo ofisini, nilikuwa najiuliza huko mjini kwenye hela ama Ofisini kwanini asije nazo nyumbani?Bwana we utu uzima dawa.

Papaa On Tuesday ya Leo inatoka katika Mithali 24:10. Ukizimia Siku Ya Taabu, Nguvu zako ni Chache. Sitaki ni fafanue kiundani, lakini tutazame neno nguvu ni kama uwezo, ability, capability,stahimili na uamuzi chanya baada ya tatizo.
Ukitaka kujua umekuwa kwa kiwango gani sio wakati kila kitu kimekaa sawa, Ukitaka kujua umekomaa kimaamuzi si wakati hakuna anayekusemea mabaya, ukitaka kujua ni kwa kiasi gani umekuwa si wakati mpenzi wako anakuchekea, ukitaka kujua umekomaa kimaamuzi sio wakati umepata promotion kazini maneno yanakutoka.

Unaongea nini unapopata Taarifa umefukuzwa kazi?unafanya nini pale yule uliyempenda kuliko kitu kingine anaposema its over, what do you do when a person you trusted ame-kucheat or lie to you.
Unaongea nini mtu uliyempa fedha zako akaamua kukuzima, mtu uliyekuwa unafanya nae biashara akikugeuka…..Ukiona umezimia kimaamuzi jua nguvu zako za kukabiliana na Changamoto za Maisha ni Chache na unahitaji nguvu kusimama.
Nikiwa Chuoni nakumbuka a woman I loved, a.k.a first lady ….Marafiki Zangu wanakumbuka unakuja jua unayempendaaaa ana-date na mtu mwingine, the same time Baba yangu ametolewa kwenye gazeti kwa Scandal na Jioni hiyo hiyo nilikuwa ninaanza Semina ya Siku tatu nakumbuka it was “Spiritual Emphasis Week” kwenye Fellowship. Nilikuwa nawakati mgumu sana sana mtu mzima nikaenda Valley (porini) nikaliaaaaaaa then nikaja chuo niko pouwa na kila mtu alikuwa anajua niko pouwa the only person ambaye alijua nakumbuka ni Mdada alikuwa anaitwa Lucy Kayombo hahaha wewe uliyezoea kuwatia watu moyo, kuwapa ushauri wengine yakikufika unajipangaje. .kuna wengine ukiwaambia watasema “Kha kama hata wewe limekupata hilo je sie?lazima tujifunze kutafuta fumbuzi za mambo na nguvu zetu kupimwa katika kila hatua ya tatizo tunayopitia.

Mambo yanapokuwa yanakukabili kwanza chekecha ubongo, tujifunze ku-sacrifice niliwahi wafundisha watu kuwa ukitaka kujua umekuwa ama lah kwaanza utaanza kuona una majukumu yanayokutaka wewe ufanye kama wewe, mfn. Kodi ya Nyumba, kulipia Karo za Wadogo zako,kulipa Luku, Kununua chakula na kununua mapazia na vyombo vya ndani na ku-Sacrifice kununua nguo mpya, blackberry na cheni ya gold basi jua umeanza kuwa mtu mzima kimaamuzi, ila ukiona unaachia kununua kitasa kipya cha mlango ulioharibika na unaenda kununua shati la kuvaa kwenye harusi wakati wewe mwenyewe umealikwa tena kwa kadi ya mtu mwingine basi jua level yako ya kuanza kukabiliana na changamoto za maisha bado iko Pentium one. 

Changamoto pamoja na matatizo husababisha akili zetu zifanye kazi zaidi ya kawaida, Changamoto hupelekea ubunifu, Changamoto ina shape tabia zetu utajiuliza how?umewahi poteza nauli ukiwa Posta na unataka kwenda Tegeta?ile shida ina ku-provoke kufanya mambo ambayo si tabia yako utalala Posta?au wewe ni mdada unatoka Chang’ombe una drive ukiwa Buguruni tairi likapata Pancha tena uko peke yako unafanyaje? Na mtu uliyekuwa unadhani anaweza kukusaidia unampigia simu is not reachable kama ni u-Sister duu utakutoka ntakuambia, na akili yako itafanya kazi kwa kiwango cha tofauti sana . Au umewahi achwa na mtu uliyempenda sana kisha akakualika katika harusi yake, je utaenda?why utaenda, au hautaenda?na kama hautaenda why hautaenda?Ukizimia Tu siku ya Taabu nguvu zako ni chache. Au umewahi itwa kwenye Kikao cha Kanisa Mchungaji wenu uliyemuamini amepata Skando ya Uzinzi na Ubadhilifu wa fedha then wewe ndo upo unaulizwa toa mawazo unaongea nini?

Sisi ni Taifa la Sasa na Baadae wengine wameshaanza majukumu ya kifamilia na wengine bado,kama umezoea kila kitu kuongea na watu kuwahadithia watu basi jiandae kuaibika kama ni shida, kwa research yangu isiyo rasmi inaonesha watu wenye uwezo wa kutunza Siri wamepungua sana ukimwambia mtu saa hizi saa 8 anajua mwingine. Changamoto zije kut+afuta msaada iwe ni njia mbadala baada ya kwako kushindikana. 
Tujifunze kukabiliana na Yale yanayotusibu kusumbuliwa na tatizo moja zaidi ya mara 5 hilo hilo kila mwezi hilo hilo kila wiki…basi wewe Jua unahitaji msaada zaidi.

Lazima tujiulize kwanini jambo fulani linatupata, kwanini kila nikijaribu kufanya Saving kila mwezi mwishowe unaila hiyo hela, kwanini kila mwezi lazima lazima nikope, kwanini kila relation ninayoingia inakuwa kimeo, kwanini ninapenda kuvaa nguo mpya, kwanini nikisoma kabla ya mtihani sielewi mpaka test itangazwe, kwanini naweza kuangalia tamthilia masaa 2 lakini siwezi kukaa lisaa limoja kuplan maisha yangu. Kwanini hata lile ninalo li plan na kulitafutia pesa hatimaye silifanyi?Je shida iko wapi?kwanini nikiambiwa Siri ya mtu yaaani lazima nitamwambia mwingine….Hivi kwanini wakati wa matatizo akili yangu haifanyi kazi?wakati mwingine hatujiulizi hivi kwanini mpaka sasa sijaoa?au kwanini mpaka sasa sijaolewa?ninatabia ya kujiuliza na kuandika, hivi kwanini hili linanisumbua na ninaandika ukweli sio hata mie mwenyewe najidanganya eti najipendelea……all its about me. Wewe keshao utakuwa na Kampuni yako, wewe Kesho utakuwa na Familia yao , wewe utawekwa katika sehemu ya kufanya maamuzi magumu either ya Kijamii au hata Kanisani kwenu utafanyaje? Wewe Jua Jambo moja Ukizimia Siku Ya Taabu Nguvu zako ni Chache.

Na Papaa Sebene-Kila Jumanne.
0713 494110


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda