Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, October 23, 2012

Papaa On Tuesday......Laiti Kama huja baada ya JutoIkiwa Imebaki miezi miwili na siku 7 ili mwaka wa 2012 uweze kumalizika tuingie mwaka 2013 mwaka wenye matukio mengi sana tukianzia na kuingia kwenye mfumo wa digitali katika TV zetu basi tujue, tutakavyouanza mwaka ndivyo tutakavyoumaliza.
Ikiwa wengine wetu wametimiza malengo yao ya mwaka, wengine wakiwa wako nusu wengine wakiwa wameyaacha malengo yao basi tujue mwaka ndio unakaribia kabisa kumalizika, wenye kujipongeza wakae mkao wa pongezi, wengi kujitia moyo basi wazidi kujipanga na wenye kujilaumu wakusanye nguvu upya.

Papaa On Tuesday niliyotaka kuituma baada ya kuiandika moyo wangu na mkono wangu umekuwa mzito sana kufanya hivyo kwa sababu ambazo ninataka kuiwakilisha kama mada siku ya leo. Si kwamba huwa ninaandika tu na kutuma lakini pia kuna ku-i-sense ndani ya moyo kama mzigo utaenda kugusa mtu mmoja ama lah. Nikiwa ninajiandaa kuipost Papaa On Tuesday ya leo yenye Jina la "Let It Go.......".Ndani yangu ikasema leo niongee hiki sasa ninachokiandika saa hii ambacho nimekipata asubuhi hii ya leo ya Jumanne tarehe 23 mwezi October.
Kwa namna ambavyo Mungu ametuumba kila mtu ana nafsi, mwili na roho. Unapoishi maisha ya hapa duniani nafsi nayo inaishi na roho nayo inaishi sambamba na mwili unavyoishi. Mtu yeyote mwenye furaha ama huzuni ya ndani nje atachangamka. Ndio maana unaweza sikia mtu ameamka kisha anasema "Leo sijui nimeamkaje??", unaweza kuta ulilala vizuri tu lakini ukaamka uko "off mood". Unaweza kuta mtu amekaa kwenye dala dala ghafla huyo mtu anasonya msonyo mrefuuuuu, kumbe alikuwa ana kikao cha nafsi,mwili na roho. Au unaweza kuta mtu mmekaa mahali ghafla anatabasamu kumbe alikuwa amevusha mbayaaa. Kila mwanadamu awe mzungu ama mbongo, awe mrefu ama mfupi, awe UAMSHO ama yeyote ana "Sauti Ya Ndani". Miezi michache iliyopita niliandika kuhusu kusikiliza Sauti Ya Mtu wa Ndani.

Mara nyingi sana either tumekosea kufanya kwenye maisha si kwa sababu hatukuhisi kuna kitu kitatokea lakini tunashindwa kuhusianisha kila tunachokisikia ndani na mwitikio wa nje. Ukiuliza Watu waliowahi Kuibiwa ama Kutapeliwa kama mpaka wanaibiwa hawakusikia chochote ndani yao??watakuambia "Yaani sijui ilikuaje nilikuw anasikia kabisa niache Pochi nyumbani nikapuuzia". Kuna watu wakiwa wanadanganywa  huwa wanajua kabisa hapa wanadanganywa lakini "wanapuuuzia". Kwa hulka ya mwanadamu kwa namna Mungu alivyotuumba ndani yetu ameweka mawasiliano ya ajabu sana kati ya nafsi, roho na mwili. Nafsi na Roho viko more advanced kuliko mwili. Kama kuna hatari yoyote inatokea roho huanza kuwasiliana na mwili tatizo volume ya nafsi ni ndogo sana kuliko ya masikio ya mwilini kuitikia kile ambacho nafsi inakisema.

Kwani wewe haijawahi kutokea unapewa hata hela ama hata zawadi unajikuta ndani yako haufurahii hicho unachopewa??haujawahi kutokea kwenye maisha yako hata mtu kwa mara ya kwanza mnakutana hamjawahi kukutana mnaweza mkawa mnaongea hata biashara au jambo lingine la Kijamii lakini unajikuta tu "nafsi" yako haimpokei kabisa huyo mtu hata kama ana bonge la idea ya biashara ama fedha lakini unajikuta unakosa "connection" ya kile anachokisema na yeye anayekisema unajikuta tu humkubali wala humpokei ndani ya moyo wako. Mwisho wa siku unasikia yule jamaa ni tapeli, ndipo ghafla unakumbuka kile ulichokuwa unasikia.
Imewahi nitokea kwenye maish
a yangu nimepata kazi nzuri na mshahara mnono kufanya kazi na Watu fulani, tukiwa kwenye final process kabisa offer ikiwa mkononi Moyo wangu ukakataaa kabisa, kweli dau ni nono, mazingira ni mazuri lakini moyo wangu haupo tayari. Kung'ang'aniza naona nakuwa sina amani wala sina furaha kuliko kukataa. Nilipokataa wakaniuliza kwanini nimekataa nikakosa maelezo  ya Kuwaelewesha kwanini nimekataa lakini ukweli ndani yangu kumekataa.
Mara nyingi sana tumepata hasara, ama maumivu ama lolote la kutupata kwa sababu ya kuto kusikiliza sauti ya ndani. Kuna watu wengi sana nawajua waliwahi nusurika ajali kwa sababu tu kusikiliza sauti ya ndani, kuna wakati imewahi tokea hata kwenye mitihani ukiwa haujuwi kabisa jibu ukaamua kuandika mawazo yako ama kuchagua jibu mojawapo na matokeo yalivyokuja ukawa umefaulu unajiuliza we ilikuaje??Kuna watu wamenusurika kuolewa na watu wenye tabia kama za "UAMSHO" kwa sababu ndani tu kulikataa, hana sababu ya msingi sana ya kumweleza mtu lakini ndani yake kulikataa kabisa kumpokea mtu huyo. Niliwahi sema kwa wale walio kwenye ndoa wanaweza kubaliana na mimi kuwa wanawake Volume za nafsi zao ziko juu sana wakati mwingine. Wanawake wanaweza ku-sense hatari kabla ya Mwanaume. Nimeshuhudia mara kadhaa kwenye marafiki zangu walio oa wake zao waliwahi waaambia "Sitaki Uwe Close na Mdaa Fulani". Wanaume wao wanaona kama dalili ya wivu fulani hivi, lakini ukimuuliza mke wake kwanini ni fulani tu na sio mwingine utasikia hata mimi sijui ila ndani kumemkataa. Hata kwenye biashara ama  Vikundi vya maendeleo ambavyo wanaume tunakaa kama siku ikatokea Mkeo akawaona unaofanya nao kazi na biashara from no where anaweza kukuambia fulani kama simuelewi elewi hivi.
Ipo haja ya kusikiliza wakati mwingine sauti ya ndani, nafsi yako inakuambia nini na nini unaamini katika hilo. Si mara zote nafsi inatupoteza lakini ukianza kuishi pia kwa kusikiliza sauti ya ndani utajikuta mambo mengi una ya sense kabla hayajawa kweli utajikuta hatari nyingi sana zinakukosa. Kuna nyakati nataka kufanya maamuzi kwenye maisha lakini nakuta nafsi yangu haina amani wala furaha yawezekana ninachotaka kukifanya kitawapendeza watu na mie nitaonekana mtu kati ya watu lakini je moyo wangu una amani katika hilo. Watu wengi sana waliowahi kuwaona nyoka ama hatari nyingine atakuambia alisikia tu ndani kitu kinamwambia "Tazama Kulia" ama "Tazama Juu" unashangaa unapofanya hivyo ndo unamuona nyoka ama hatari iliyopo. Tatizo ni pale watu wanapokuuliza we Ulijuaje??
Sio rahisi kuitii sauti ya ndani lakini inahitaji mazoezi, kuna magari utapanda na ajabu utasikuta umesahau kitu ukashuka unaposhuka tu gari inagongwa. KUna siku rafiki yangu ali park gari mahali kwa muda kama wa nusu saa akimsubiri mtu, ghafla akajisikia akaweke mafuta kwanza kisha ndipo aendelee kusubiri, ile anatoa tu gari lake pale alipo park dakika 1 tu Lori imeacha njia limeeenda pale paleeeee alipokuwa ame park. Tukamuuliza Ilikuaje ukaamua kutoka pale baada ya ku park nusu saa akasema nilikaa nikawaza nikajisemea nikaweke mafuta kwanza ile natoka ndo imetokea haya yote. Hii hali ukiishi nayo utagundua kuna watu wengine hata ukitaka kuwashirikisha mambo yako nafsi inakataa kabisa, unaweka kabisa ukapanga appointment na mtu ukafika ile unaanza kuongea tu unakuta kuna ugumu unaupata. Kuna Kamati nimewahi kuwepo za kuandaa mambo fulani fulani from no where nikahisi hii kamati "mwisho wa siku tutagombana" pole pole nikajitoa ajabu haukuchukua hata muda watu wanasema 'afadhari wewe ulijitoa mapema".
Jifunze kusikiliza sauti ya ndani itakusaidia katika mambo madogo na makubwa. Mungu aliyetuumba anaweza kukusaidia sana ukimwomba akusaidie kusikiliza Sauti ya Ndani. Mimi mwenyewe nilikuwa nimeandaa Papaa On Tuesday nyingine kabisa ghafla Nikajisikia kumwambia Mtu kwa kuandika Kujifunza Kusikiliza Sauti Ya Ndani. Inawezekana ni wewe Msomaji wangu unayesoma sasa Kuna Issues kibao unashindwa kuamua sababu kuna Utata wa Kile unachokisikia na Kile watu wanachokushauri, Inawekana unatamani kuacha kazi sababu moyo wako unaamini kuna biashara unaweza kufanya zaidi ya Ajira uliyonayo ila HOFU imekutanda ila Moyo wako uko tayari hata kulala njaa kwa sababu ya kile Moyo wako unachotaka ukifanye. Kuna mwingine nafsi yake imeinama kabisa u have been so disappointed na kile kinachoendelea kwenye maisha yako pengine ukaamini Ukisoma Papaa On Tuesday leo utapata Kitu, usisikilize tu mawazo yako sikiliza na nafsi yako pia maana yamkini Papaa On Tuesday Ijayo ya Let It Go inaweza kuwa ya kwako.


Wenu Mtiifu,
Papaa Ze Blogger
0713 49410. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda