Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, October 26, 2012

Ole Sendeka amwaga mamilioni Kata ya Endiamtu-Mererani

Na Mary Margwe,
Simanjiro Manyara

ZAIDI ya sh.mil. 45, zimetumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo katika kata ya Endiamtu Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.


Hayo yamesemwa juzi na Diwani wa kata hiyo, Bw.Lucas Zacharia wakati akizungumza na waandishi wa habari alipopokelewa na wakazi wa kata hiyo mara baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM wa mkoa  huo,

Bw.Zacharia alisema  kata hiyo ni ya mfano katika Halmashauri ya Wilayani hiyo kwa kusimamia vyema miradi yake na kuwa ya ubora ukilinganisha na kata zingine za Wilaya hiyo,ambapo alisema ni uaminifu na uwajibikaji unahitajika katika matumizi ya fedha .
Aidha aliitaja miongoni mwa miradi ya kata hiyo kuwa ni pamoja na ya ujenzi wa madarasa matano ya shule ya msingi Endiamtu, ujenzi wa wodi ya kina mama wajawazito kwenye kituo cha afya, sakafu ya maabara na ujenzi wa sehemu ya mifugo kunywa maji (mbauti).

Alitaja miradi mingine mipya ya kata hiyo kuwa ni ofisi ya kisasa ya walimu wa shule ya msingi Endiamtu,chumba cha kuhifadhi maiti kwenye kituo cha afya,ujenzi wa barabara za mitaa ya kata hiyo na ujenzi wa kisima cha kitongoji cha Kairo. 
“Maendeleo yote hayo yamepatikana kutokana na ushirikiano mkubwa na mzuri kutoka kwa mbunge wetu wa Simanjiro,Simba wa mkoa wa Manyara Bw. Christopher Ole Sendeka kwani mimi peke yangu nisingeweza kufikia hayo yote,”  alisema Bw.Zacharia. 
Alisema Bw. Ole Sendeka alitoa sh. mil.20, mifuko mitano ya saruji na mabati 50 kwenye kata hiyo na Diwani huyo Zacharia akachangia sh. 4 milioni huku marafiki zake wakitoa sh.2.5 milioni na wananchi wa kata hiyo wakachangia sh.18 milioni kwa lengo la kugharamia shughuli za miradi mbalimbali iliyoko katika kata hiyo ya Endiamtu.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani Bw.Albert Siloli alimpongeza Bw.Zacharia kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Uchumi na Fedha wa CCM mkoa wa Manyara ambapo alisema ameipa heshima kubwa kata yake ya Endiamtu.
Bw.Siloli alisema pamoja na ushindi  alioupata Bw.Zacharia amekua akisimamia maendeleo makubwa kwenye kata ya Endiamtu kwa muda mfupi aliochaguliwa hivyo kuwapa wakati mgumu wapinzani kwa kile alichokidai  kuwa  watakosa jambo la kuzungumza juu ya CCM.
Naye,Katibu wa CCM kata ya Endiamtu, Bw.Salimu Mohamed alisema kata yake inatakiwa kupongezwa kwani imeweza kutoa viongozi wawili wakubwa wa mkoa huo akiwemo Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Manyara, Bi.Dorah Mushi na Bw.Lucas Zacharia.ambaye ni Katibu wa Uchumi na fedha wa Mkoa wa Manyara.
“Kutokana na hali hiyo tunalo deni kubwa la kuwapa ushirikiano ili waweze kutumikia nafasi hizo kwa ufasaha kwani wilaya tano zimetupa heshima kubwa sisi wilaya ya Simanjiro hadi tukaweza kutoa viongozi hao,” alisema Bw.Mohamed.
Hata hivyo pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa kata hiyo,Wilaya na hususani Mkoa kuwapa ushirikiano viongozi hao ili kuhakikisha kuwa wanafikia malengo yaliyowekwa kikamilifu na si vinginevyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda