Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, October 26, 2012

Ngisere Sumleck: Wafugaji wapatieni watoto wenu Elimu

Na Mary Margwe,
Simanjiro

WITO umetolewa kwa jamii ya wafugaji nchini kuendeleza kikamilifu juhudi za kuwapatia elimu watoto wao ambao hivi sasa wamekuwa na mwamko mkubwa wa kupenda elimu.

Hayo yameelezwa na wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Lengasiti iliyopo Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara kwenye risala iliyosomwa na Bi.Ngisere Sumleck kwenye mahafali ya kuhitimu elimu hiyo.
Bi.Sumleck alisema elimu ndiyo ukombozi hususani kwa jamii ya wafugaji ambao kwa sasa wameonekana kupiga hatua kubwa ya maendeleo hapa nchini hivyo wazazi wanapaswa kutoa kipaumbele kwa watoto wao ambao hivi sasa wana mwamko mkubwa wa kusoma.
Alisema hivi sasa kila eneo la jamii ya wafugaji hapa nchini watoto wamekuwa wanapenda kupata elimu hivyo wazazi na walezi wanatakiwa kuwaunga mkono juhudi hizo badala ya kuendelea  kuwafanya kuwa wachungi wa mifugo yao.
Alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1995 ikiwa shule ya nane kusajiliwa wilayani humo na kati ya watoto 37 walioanza darasa la saba mwaka 2006 , ambapo watoto 32 walihitimu baada ya watano kuondolewa kwa kukariri darasa la nne.
Naye,mgeni rasmi wa mahafali hayo, Bw. Kanunga Paulo ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite, alisema anajitolea kumalizia ujenzi wa ofisi ya walimu inayogharimu sh. mil.1.3, baada ya wazazi kuchangia sh.550,000.
Aidha Bw.Kanunga alisema kuwa baada ya yeye kujitolea kujenga madarasa mawili kwa watoto wanaosoma shule ya awali hivi sasa amejitolea kujenga ofisi hiyo ili kuwawezesha walimu wa shule hiyo kufanya kazi zao ipasavyo.   
“Kutokana na mwamko mkubwa wa elimu waliyonayo watoto wetu na nawapa hongera kwa kupenda elimu hivyo nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu katika kuhakikisha kuwa wanapata mahitaji yao hapa shuleni,” alisema Kanunga.
Kwa upande wake, Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bw. Fidelis Mtenga alitoa wito kwa jamii ya wafugaji kung’ang’ania elimu kwani umasikini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa elimu. Bw.Mtenga alisema anaunga mkono falsafa ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ya elimu kwanza kwani kilimo kwanza kimeshindwa kufanikiwa kutokana na jamii kutokuwa na elimu hiyo.

“Hatuna elimu ya kilimo kwanza kwani hatuwezi kutekeleza jambo lolote bila elimu na elimu ndiyo mhimili wa maisha kwani hata kulima mtu anapaswa aelimishwe kwanza ndipo atanufaika na kilimo,” alisema Bw.Mtenga.
                                                    

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda