Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, October 3, 2012

MUHTASARI WA KIKAO CHA PILI CHA MBULU YOUTH GROUP

MUHTASARI WA KIKAO CHA PILI CHA MBULU YOUTH GROUP (MYG) CHA JUMAPILI YA TAR 23/09/2012
ULIOFANYIKA NEW ROYAL NJOMBE HOTEL UBUNGO –DAR ES SALAAM

I.(A.)WALIOHUDHURIA 
1. ADAM ISRAEL MAYO 
2. JOHN Q. NAKEI 
3. REVOCATUS A. PANGA 
4. BENNY MAO 
5. ANNA KHADAY 
6. TUMAINI MAYO
7. ALEXANDER MAYO 

(B. ) UDHURU MAALUM 
1. MILIMILI AKOUNAY
2. NDG JOHN 
3. GODFREY E. MASSAY

(C ) WALIOPATA TAARIFA NA HAWAKUHUDHURIA 
NI WAJUMBE ZAIDI YA 30 
II. AGENDA ZA KIKAO 
1.1KUFAHAMIANA 
2.1 KUSAIDINA KULINGANA NA TAALUMA TULIZONAZO AU (FURSA) 
3.1. KUIMARISHA UMOJA WETU (Katiba, Usajili, Akaunti ya Taasisi , Sanduku la barua , Ofisi nk )
1.1 KUFAHAMIANA 
Kikao kilifunguliwa mnamo saa 11.00 jioni na Ndg Adam I Mayo na baada ya hapo tulitambulisha kwa majina yetu na kufahamiana zaidi kama wanaTaasisi tunaokusudia kuwa na mashirikiano yenye tija katika jamii zetu tuwapo huku mjini na sehemu nyinginezo ilipo jamii yetu .

2.1 KUSAIDIANA KULINGANA NA TAALUMA TULIZONAZO (MAAZIMIO) 
Baada ya kujitambulisha kwa majina na sehemu tunazoishi kwa hapa mjini na pia machimbuko yetu (nyumbani tulipotoka) kila mmoja alijitambulisha kwa Professional yake na jinsi gani ataweza kuisaidia jamii yake kulingana na Taaluma yake pindi arudipo Nyumbani kwa matembezi au Likizo .Kila Mjumbe alitoa mipango mikakati yake katika kuisaidia jamii ya kwetu iliyo nyumbani na popote nchini Tanzania kadri ya ufahamu na uelewa ktk Taaluma yake .

3.1 KUIMARISHA UMOJA WETU (TAASISI) 
Mipango Mikakati iliyo mbele yetu kwa sasa ni jinsi ya kuimarisha huu umoja wetu kwa kuwa na Katiba ambayo itakuwa ndio muongozo mkuu katika kufanya kile ambacho tumekikusudia katika jamii yetu. Mchakato wa katiba unategemea mawazo ya Wanagroup wote popote walipo na huu mchakato unaweza kuanza sasa hivi .Pia mojawapo ya mambo mengine baada ya mchakato wa Katiba kukamilika ndipo hapo tunatarajia kuisajili hii Taasisi yetu ili Tupate Baraka zote za Kiserikali katika moja ya shughuli zetu . Na haya yote yanategemea mawazo ya kila mmoja wetu na kila mtu akijitoa kwa nafasi yake .Moja ya makubaliano ya kikao ilikuwa ni kila mmoja alete watu wawili na hata zaidi ya hapo kwa sababu mambo yaliyo mbele yetu yanahitaji zaidi idadi ya Wanachama alahu 20 na zaidi ili kukamilisha taratibu za Mwanzo za hiki kikundi chetu ambacho kinatazamiwa kuwa Taasisi Bora na ya kwanza ktk kuchochea maendeleo kwa jamii yetu .

4.1 CHANGAMOTO 
Baadhi ya Changamoto katika shughuli zetu ni hali ya mahudhurio kwa Wajumbe na hasa Wanawake ambao tunaamini ndio Jeshi kubwa na kichocheo cha mafanikio . Pia udhuru nyingi zinapozidi kawaida kuchelewa kuanza kwa vikao na suala zima la uhamasishaji linakuwa kwa watu wachache . Kwa hiyo tunaomba kila mmoja ajaribu kumvuta mwenzake kadri atakavyoweza .Kitu kingine hatuna baadhi ya contact za wadau ktk Group hivyo tunaomba ushirikiano wenu ktk hilo .Pia suala la kiuchumi bado si zuri sana kwa sababu kikundi chetu bado ni kichanga kinahitaji malezi ya kila mmoja wetu ili kizidi kusonga mbele.

5.1 HITIMISHO 
Mwisho tunapenda kuwashukuru wote Wanaokesha kutuombea walioshiriki kwa namna moja ama nyingine ktk kufanikisha kikao chetu .Pia waliokuwa wakitusaidia kufikisha ujumbe kwa kila mdau aliye kila pande za Jiji la Dar es Salaam na maeneo Jirani . Pia walio mikoani kwa kutupa moyo nasi tunatambua uwepo wenu popote mlipo na Mungu wa upendo andelee kuwapa moyo huo huo daima milele .
KWA MAONI USHAURI NA PALE PANAPOHITAJI NYONGEZA TUNAWAKARIBISHA SANA NA KWA MAWASILIANO ZAIDI 0719870097/0718982010/0763461146 
Email: amayo7814@yahoo.com TOGETHER WE CAN

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda