Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, October 11, 2012

LUCY STEPHANO AZIDI KUNG'AA: Ashinda taji la Redds Miss Photogenic 2012

Nyota ya Mrembo Lucy Stephano kutoka Haydom juzi usiku imezidi kung'aa na kupaa juu zaidi katika tasnia ya sanaa ya Urembo nchini baada ya kuibuka kidedea katika shindano ka kumsaka mrembo mwenye haiba katika picha liliwashindanisha warembo wengine 29 katika ukumbi wa Hoteli ya Emanyata wilaya ya Monduli mkoani Arusha yaani Redds Miss Photogenic 2012.Kwa Ushindi huo umemwezesha Lucy kuwa mshiriki wa kwanza kabisa kutinga hatua ya nusu fainali katika kumsaka Redds Miss Tanzania 2012 litakalofanyika Novemba 3 katika Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam ambapo mshindi ataiwakilisha Tanzania katika shindano la kumsaka mrembo wa dunia mwaka 2013. Hatua ya nusu fainali itajumuisha washiriki 15 ambapo watapatikana katika michojo na mashindano mwengine yatakayofanyika ikiwa ni pamoja na Miss Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman.

Lucy ambaye alianza safari yake ya urembo aliposhiriki katika shindano la kumsaka Miss Haydom 2012 na kushika nafasi ya 2 nyuma ya Agnes Michael, kisha kuibuka kidede katika shindanoo la kumsaka Miss Mbulu 2012 na kisha kushika nafasi ya tatu katika Miss Manyara 2012 na hatimaye kuwa mwakilishi wa Kanda ya Kaskazini katika shindano hili la sasa.

Katika hali ya kuonesha kuwa Lucy anakubalika na washiriki wenzake, wakati majina ya washiriki 5 bora walioingia hatua ya fainali yakitajwa, jina la Lucy lilipotajwa ukumbi mzima pamoja na washiriki wenzake walizizima kwa shangwe na kuwa dalili za Lucy kushinda zilionekana toka awali kabisa.

Ohayoda, wana Haydom na Mkoa wa Manyara kwa ujumla wanampongeza Lucy kwa kuwa balozi mzuri wa huku kwetu, na tunamtakia mafanikio mema katika kutimiza ndoto yake na kutuletea sifa.

Usikose Mahojiano baina ya Ohayoda na Lucy Stephano mara baada ya kutangazwa mshindi yatakayokujia jivi punde.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda