Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, October 11, 2012

Lucy Stephano alonga na OHAYODA: Ushindi ni lazima

Mara baada ya Lucy Stephano kutangazwa kuwa Redds Miss Photogenic 2012 na kuwabwaga washiriki wengine 29 wanaoshiriki katika king'ang'anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania liliofanyika katika Hoteli ya Emanyata, Ohayoda ilipata fursa ya kufanya mahojiano (exclusive interview) na mlimbwende huyo ambaye pia anashikilia mataji ya Redds Haydom Miss Talent 2012, 1st Runner Up Redds Miss Haydom 2012, Redds Miss Mbulu 2012, 2nd Runner Up Redds Miss Manyara 2012 na Redds Miss Nothern Zone 2012
Redds Miss Photogenic 2012
Lucy Stephno

Blogger aliamua "kumvutia waya" mrembo huyo mwenye haiba zaidi nchini, ambaye ameiwakilisha vema Haydom na Mkoa wa Manyara kwa ujumla, na hivi ndivyo azungumzo yalivyokuwa;

Simu: Ngrrrrrrrrrrrrrr ngrrrrrrrrrrrrrrrrrrr ngrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr

Lucy: Halloooooo mambo kaka Amani
Blogger: Saitaa xaye
Lucy: Sayuu ako

Blogger: Kwanza Hongera sana kwa kuibuka mshindi mwenye haiba zaidi nchini
Lucy: Asante sana

Blogger: Unajisikiaje kushinda taji hilo
Lucy: Kwa kweli najisikia furaha sana hasa kuwa mshiriki wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali, I am more confident sasa na nina uhakika wa kufanya vizuri zaidi katika hatua ya nusu fainali na kuibuka mshindi.

Blogger: Nini kinakupa huo ujasiri? Maana kadiri siku zinavyozidi umekuwa ukifanya vizuri ukizingatia ulikuwa mshindi wa pili Miss haydom?
Lucy: Mwanzoni nilikuwa sijiamini na ilikuwa jambo geni hasa Haydom na mtazamo wa watu kuwa U-miss ni uhuni na umalaya, lakini baada ya kujua ni sanaa kama sanaa zingine na kujitambua kuwa ninaweza, nimepata confidence na hata wshiriki wengine walitarajia ningeshinda taji la Miss Photogenic

Blogger: Kwa kushinda taji hilo, umepata zawadi gani?
Lucy: Zaidi ya kuingia 15 Bora (nusu fainali) sijui kama watanipa zawadi nyingine maana hatukuahidiwa

Blogger: Ni vigezo gani hutumika kumpata Miss Photogenic?
Lucy: Wanaangalia mtu mwenye mvuto na haiba katika picha.

Blogger: Washiriki wenzako wamechukuliaje Ushindi wako?
Lucy: Wengi walifurahi maana walitarajia ningeshinda, hata tulipoingia fainali wengi walinitia moyo na kuwa nilistahili

Blogger: Inasemekana katika mashindano hayo mara nyingi mshindi hufahamika kabla yaani wengine huwa wasindikizaji tu, kuna ukweli katika hilo?
Lucy: Sina uhakika na hilo kwa kweli maana kama ingekuwa hivyo mimi nisingeshinda maana wapo washiriki waliotoka mijini na wenye kufahamiana na watu wengi, naamini haki hufanyika

Blogger: Kuna tetesi kuwa sasa Lucy hatarudi tena haydom, kuna ukweli katika hilo?
Lucy: Hahahahaaaa huo ni uzushi tu kakaangu, Haydom ni nyumbani lazima nirudi baada ya mashindano, mimi ni yule yule sijabadilika kitu. Japo ninajua kuna fursa nyingi za kazi ninazoweza kuzipata hasa Dar ambazo zitaweza kunifanya nifanye kazi huko lakini bado nitarudi Haydom

Blogger: Watu wa Haydom na Mkoa wa Manyara watarajie nini kutoka kwako baada ya mashindano hayo?
Lucy: Watarajie kuwa balozi mzuri hasa wa Haydom na mkoa wa Manyara na nitaitumia nafasi nitakayoipata kuielimisha jamii juu ya mambo mbalimbali kwa kadiri nitakavyopewa majukumu na wahusika.

Blogger: Ungependa kuwashukuru nani haswa kwa kukuwezesha kufika hapo ulipo?
Lucy: Kwanza ni familia yangu kwa kuniruhusu kushiriki na kunipa sapoti, Mama Mzungu kwa kunishawishi nishiriki na kunitia moyo, Teddy, Cecy, Mr. Sinjela wa Mbulu, Ohayoda na Wasomaji wote Ohayoda, Jumuia nzima ya Haydom Lutheran Hospital na wana Haydom kwa ujumla.

Blogger: Mwisho unaujumbe gani kwa wanaHaydom na wasomaji wa Ohayoda
Lucy: Ninawashukuru sana na ninaomba wazidi kuniombea na kunipa sapoti, ninawaahidi nitafanya vizuri na kulileta taji Haydom

Ohayoda inamtakia Lucy mafanikio mema na kuwa balozi mzuri wa Haydom na Mkoa wa Manyara kwa ujumla. Unaweza kuacha ujumbe wa maandishi hapa chini na kumpa sapoti naye ataupata moja kwa moja ili aweze kutuwakilisha vyema.1 comment:

  1. KUNA KILA SABABU YA KUMTANGAZA AJULIKANE ZAIDI KATIKA MITANDAO ILI APATE NAFASI KUBWA ZAIDI KWANI TUSIPO MUINUA SISI MAJIRANI ZAKE HUKU NYUMBANI TUNATEGEMEA NANI AMUINUE? NIKIWA PRO. WA REDDS MISS MANYARA 2012 NITAHAKIKISHA PICHA ZOTE ALIZOPIGA NA VIDEO NAZITUPIA KTK NET ILI IJIDHIHIRISHE KUWA ANASTAILI.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda