Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, October 24, 2012

KURA YA MAONI: Miaka 10 ya Mkoa wa Manyara, Je mkoa umekidhi mahitaji ya wananchi kiuchumi, kiutamaduni na kijiografia?

Wapenzi wasomaji wa Ohayoda tunapenda kuwakaribisha tena katika kipengele hiki kinachokupa wewe msomaji kutoa maoni yako kuhusu masuala mbalimbali ambayo yanajiri katika jamii yetu. Baada ya kipengele hiki kutokuonekana hewani kwa muda mrefu kwa sababu kadha wa kadha, sasa kimerejea kikiwa na mada moto kila wiki.
Mnamo mwaka 2002 baada ya kilio cha muda mrefu cha wananchi wa mkoa wa Arusha ambao ulikuwa mkoa mkubwa kuliko yote nchini, mkoa wa Arusha uligawanywa na kutoa mkoa mpya wa Manyara na kufanya idadi ya mikoa nchini kuwa 26. Awali mkoa mpya ulipendekezwa kuitwa mkoa wa Bonde la Ufa (Rift Valley) na kuwa na wilaya tano za Mbulu, Hanang, Babati, Karatu na Ngorongoro ambayo ilikuwa katika ukanda mmoja kijiografia na kiutamaduni na mkoa wa Arusha kuwa na wilaya za Arumeru, Arusha, Monduli, Simanjiro na Kiteto. Lakini baada ya mchakato na sababu ambazo mpaka leo hazijawekwa wazi mkoa mpya ukaitwa Manyara na ukawa na wilaya tano za Mbulu, Babati, Hanang, Simanjiro na Kiteto makao makuu yakiwa Babati ambao ramani yake ipo hapo chini.

"Fast Forward" miaka 10 baadaye, mkoa wa Manyara unatimiza miaka 10 mwaka huu. Wakati viongozi wakifanya mchakato wa kusherehekea miaka hiyo 10, Ohayoda inapenda kupata maoni ya wasomaji wake, je Mkoa wa Manyara umetimiza malengo ya kuanzishwa?

Jiografia ya mkoa wa Manyara ni ngumu na hata ukiwauliza wanafunzi na hata "viongozi" wa mkoa wa Manyara "mkoa wa manyara umepakana na mikoa ipi" wengi hawajui. Mkoa wa Manyara umepakana na mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kwa Mashariki, Arusha upande wa Kaskazini, Dodoma upande wa Kusini, Singida na Shinyanga kwa upande wa Magharibi.
Kifupi ramani yake ipo kama 8 iliyolazwa na wilaya za kiteto na Simanjiro ziko mbali sana na makao makuu ya mkoa yaani Babati.
NAMNA YA KUSHIRIKI: Piga kura yako juu kabisa ya blog kwa kuchagua jibu sahihi kisha bofya VOTE nawe utaona kura yako ikiongezeka, matokea yatawajia baada ya wiki moja bila uchakachuzi wowote.

2 comments:

  1. Naipongeza Ohayooda kuweka vitu hivi hadharani."Mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru..." Hakuna hata mtu mmoja asiyependa kuwa huru, ni ukweli tu utatuweka huru na si lolote wala chochote. Watu wengine wameitafsiri siasa kama "siHasa" na Serikali kama "sirikali" - Kwa kifupi ningesema tuiombee sana tena sana nchi yetu ya Tanzania na viongozi wake. Hilo tu kwa leo

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda