Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Saturday, October 13, 2012

Jamii inajua Umuhimu wa FLEGMATIKI-Unaijua HAIBA yako?


More of Flegmatiki….
Juma hili tumekuwa tukijifunza juu ya kile ambacho tumekipa jina la sifa njema za mwanadamu anayeitwa Flegmatiki kwa kuaangalia sifa njema alizonazo na ni kwa jinsi gani huyu mtu ni msaada katika jamii kutokana na jinsi yao ya kuishi na watu na jinsi wanavyo fanya maisha jinsi yalivyo. Tuendelee kuangalia sifa za flegmatiki kwa namna nyingine tena katika njanja zifuatazo.

 • Kwa aasili ni mwanadamu mwenye uwezo mkubwa sana wa kufikiri kutokana na utulivu alionao.
 • Ni wepesi kuendana na mazingira ya kila aina kutokana na unyofu wa moyo walionao.
 • Anafundishika kwa urahisi.
 • Anakiwango cha juu cha uvumilivu na kuleta hali ya amani wakati wa hali ngumu au magomvi katika jamii Fulani.
 • Ni wepesi sana kufundisha na mtu akaelewa lakini si atika kikundi cha watu kutokana na kwamba wana aibu sana.
 • Ni wazuri sana katika kazi ya ufuatiliaji wa jambo Fulani na jambo lenyewe likaleta manufaa.
 • Wanamahusiano mazuri na watu na wepesi sana katika kutunza hayo mahusiano yakadumu kwani hawana magomvi ya mara kwa mara.
 • They are peace makers, mapatano na usuluhishi ni jambo ambalo wanauwezo wa kulifanya kirahisi sana.
 • Ni watu ambao wapo tayari katika kufanya kazi ya kujitolea hata bila malipo yeyote.
 • Ukiwasikiliza kwa makini, na kutokana na hali yao ya utulivu wa nnje na wa ndani, Mungu kawapa uwezo wa kutabiri mambo yajayo na yakawa kama walivyotabiri. Lakini si kwa fujo na vurugu bali ni kwa utulivu wa hali ya juu unaweza hata usijue na hata hawapendi watu wengi wafahamu., tofauti na koleriki au sangwini-wazee wa masifa.
 • Ni wakarimu sana na wenye mkono wa msaada kwa wengine kwa kile kidogo walichonacho.
 • Hawana kelele.
 • Ni mtu mwenye kiasi sana katika mambo yote.
 • Ni watu wazuri sana katika diplomasia.
 • Katika upande wa saikolojia ni flegmatiki ni mshauri mzuri sana na anayeeleweka na kukubalika.
 • Kila anapoenda ni mwepesi sana kukubalika kwa watu wa kada zote kutokana na hali yake.
 • Ni wastaarabu sana kwa wakweli.

Endelea kufahamu mengi kwa kuandika neno “FLEGMATIKI AU KOLERIKI AU SANGWINI AU MELANKOLI” ili kujua haiba yako na za wengine ili uweze kuishi na watu bila matatizo na baadaye tuweze kupata mafanikio hasa sehemu za kazi, maofisini kuna tabu nyingi sana lakini “knowledge is power” ukipata elimu inakupa neema na nguvu ya kuishi na watu wengine.
                                           
 Mungu akubariki ndugu yangu……
Inaendelea ijumaa-Jikomboe kiuchumi, kiroho, kiafya, kimahusiano, kitaaluma 
na kisaikolojia pia.……………

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda