Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, October 8, 2012

FLEGMATIKI, Binadamu Mwenye Tabia za aina ya tofauti kuliko wote.

Na Nelson Faustin JR Psy.
Si jambo la kawaida kumwita mtu malaika. lakini kwa sifa zao hawa huonekana kama malaika japo kwa asili ni wanadamu kama sisi na kuna mambo ambayo wanayo ambayo wewe na mimi ambaye si FLEGMATIKI unajikuta unawapa sifa ya kuwa malaika.

Baada ya kuona sifa utangulizi watu waliopo katika kundi hili, hatuna budi sasa kujifunza japo sifa chache za wanadamu hawa makundi kwa makundi.
Japo nimekuwa kimya kwa muda mrefu lakini ashukuriwe Mungu atupaye neema kubwa ya kuendelea kuwa pamoja katika gurudumu hili la maisha hapa Tanzania nchi yetu iliyo ya neema nyingi sana.

(Tujifunze kwa watoto)
Leo tueendelee kujifunza haiba za watu mbalimbali hasa wale ambao hatukumalizia kuzifahamu tabia zao vizuri. Leo tujifunze kundi hili la watu wanaoitwa FLEGMATIKI kwa kuangalia tabia zao kwa upande wa sifa zao njema na mapungufu yao pamoja na njia bora za kuweza kuishi nao bila ya kuwafanya wawe na masikitiko na kuona kuwa maisha ni magumu.

Baada ya kuona utangulizi wa maana ya FLEGMATIKI katika makala iliyopita, katika makala hii tunaenda kuona sifa njema za mwanadamu mwenye tabia za flegmatiki na namna ambavyo yeye ni mtu wa muhimu sana katika kuweka katika maisha yetu ya kila siku kwani ni kweli tunawahitaji na bila wao fujo na vurugu hazitaisha kabisa. Cha kuamini  tu ni kuwa hawa watu ni tabia ya utofauti sana na si watu wa fujo bali ni watu ambao siku zote wanaishi ilio kuleta amani, faraja, furaha na mafanikio makubwa kutokana na tabia zake Mungu alizomuumbia.

(Je, Mungu anajivunia kuwa na wewe?)
Dondoo za sifa njema za Flegmatiki ni kama vile zifuatazo.
·         Ni watu ambao kwaasili wana amani na wanapenda kutafuta amani na watu wote.
·         Ni wapole sana na wasiopenda makuu. Ukifanya tathmini utaona kuwa koleriki na sangwini wana ujasiri wa kusifu juu ya utu wao lakini hata kama Flegmatiki ana nafasi kubwa kiasi gani lakin kwa kawaida wapo kimya.
·         Utayari wa kufanya kazi ya hiari bila ya maswali maswali mengi ni swala lao la msingi ambalo ni la kawaida kabisa bila ya kusukumwa sukumwa na mtu.
·         Wanaamani na ututlivu wa ndani na wanafuraha mara zote hata kama wakiudhiwa.
·         Si wepesi kukasirika hata kama imewapasa kufanya hivyo japo kama wanadamu wa kawaida bado hukasirika.
·         Magonjwa ya moyo na matatizo mengine ya kisaikolojia ni hadithi kwao.
·         Wapo tayari kupata hasara ili tu wapate utulivu na kuepuka migogoro na kwao nivyema WASIHUSISHWE  kama jambo husika litaleta migogoro baadaye.
·         Kuweka vinyongo moyoni kwao ni suala ambalo ni gumu sana na ni wepesi sana kusamehe. Kusamehe kwao ni jambo rahisi sana ukilinganisha na makundi mengine ambayo kusamehe ni ishu ya kuamua na kufanya.
·         Ni watu ambao kwa kiingereza tunawaita, “simple guys” yani wana maisha marahisi sana hata kama wanauwezo mkubwa kiuchumi, kumbuka hawana makuu kabisa.
·         Wana uungwana sana, si watu wakuona “kwani utanifanya nini’, yani hawa wajamaa bhana, kusema…I am sorry….ni jambo rahisi sana..
Ustawi wa FLEGMATIKI ni kama wa Tausi
·         Wanaweza wakaamua kusikia jambo lakini si wepesi sana kusisimka japo ni watendaji…hii hutokana na hali yao ya utulivu.
·         Hawa wajamaa wanahuruma sana na moyo wa kuwajali wengine..ndiyo maana wengine wanakuwa manesi kwani ni kazi ambayo inhitaji huruma sana.
·         Ni watu wenye maadili mema, si rahisi sana kuwakuta katika mambo ambayo si ya kumpendeza Mungu na hata kama wakiingia ni wepesi sana kutoka kwani dhamira zao haziwaruhusu kufanya hivyo.
·         Ni washauri na wasikilizaji wazuri.
·         Ni watu wanaojua kutunza siri, wengi hutumiwa katika shughuli hata za usalama wa taifa na mengine kama hayo.
·         Ni watu ambao ni rahisi sana kuishi naye kuliko mtu mwingine wa kundi lingine lolote,.

Flegmatics r never Angels. 
Mpaka hapa, ninaamini tayari umejua ni nani ambaye ni Flegmatiki na tayari umeshawafahamu kwa majina. Kipindi kijacho tutaendelea kujifunza tabia njema za kundi hili la Flegmatiki.

Endelea kufahamu mengi kwa kuandika neno “FLEGMATIKI AU KOLERIKI AU SANGWINI AU MELANKOLI” ili kujua haiba yako na za wengine ili uweze kuishi na watu bila matatizo na baadaye tuweze kupata mafanikio hasa sehemu za kazi, maofisini kuna tabu nyingi sana lakini “knowledge is power” ukipata elimu inakupa neema na nguvu ya kuishi na watu wengine.

                                           
 Mungu akubariki ndugu yangu……

Inaendelea ijumaa-Jikomboe kiuchumi, kiroho, kiafya, kimahusiano, kitaaluma 
na kisaikolojia pia.……………

1 comment:

  1. Samahani ndugu Nelson tafadhali naomba kujua ni njiaagani ambayo ninaweza kuitumia ili niweze kuijua haiba yangu naomba vigezo ili nijifahamu. Asante

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda