Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, October 26, 2012

FLEGMATICS...Like Angles But with Differences and Weaknesses like Choleric, Melancholy and Sanguine...(Mapungufu ya Flegmatiki)


Na Nelson Faustin.
Happy Galz.
Mungu katika uumbaji wake ni mwema sana na anajua namna ya kuwaweka watu wake kama atakavyo yeye, Ni kweli kuwa, kwa asili tunamwona mwanadamu mwenye tabia za kiFlegmatiki kama mtu ambaye ana tabia  kama malaika kutokana na jinsi anavyoishi na watu na kila mara tunajifunza kutokana na namna ambavyo wanachukuliana na kila aina la kundi na kwa ajabu ni kuwa kila aina ya kundi ni rahisi kuishi nao bila wasiwasi wowote. 

Lakini cha kushangaza ni kuwa, hata wao wanamapungufu yao mengi sana ambayo kwa namna fulani kama ilivyo kwa Koleriki, Melankoli na Sangwi waakera katika maeneo fulani na lazima tuwaambie ili kama walikuwa hawajui basi wajifahamu, wafahamu mapungufu yao na baadaye tuwape nafasi ya kujirekebisha ili aweze kuishi na watu vizuri.
Twins For Twins as One...Like Angels vile.

Mapungufu yenyewe ni kama haya yafuatayo:-
 • Ni watu wasiotaka mabadiliko ya hararka kama ikiwabidi kufanya hivyo, hawa ni waoga wa mabadiliko, bora akae na kitu hata kama hakilipo Kwa mfano kwenye mahusiano, anaweza akaamua kwenye relationship ambayo hailipi lakini akakomaa hapohapo.
 • Flegmatiki maranyingi wana haliya uzembe na uvuvu ndani yao. Si wachangamkia dili yani.
 • Ni watu wenye aibu sana, hata kama ni kufanya jambo hawalifanyi mbele ya watu bali mbali na watu.
 • Huridhika haraka sana na hivyo husababisha kutokufikiwa kwa malengo kusudiwa.
 • Wanangu after work.
 • Ni waoga sana sana, si wepesi sana kuamua mambo au kufanya mambo mbalimbali.
 • Ni watu ambao hupenda sana kukaa peke yao, wanapenda sana hali ya upweke katika maisha yao.
 • Kutokana na kutokupenda sana mabadiliko chanya, hawa ni wavivu sana na hukwamisha mambo kwa kukatisha tamaa.
 • Ubinafsi wao husababishwa na jinsi ambavyo wanapenda kukaa peke yao na kujiona kuwa wanauwezo mkubwa sana wa kufanya mambo zaidi ya kujichanganya na watu wengine..inshort hawapendi fujo.
 • Flegmatiki hana kusudi la maisha kwa maana kwamba ni wepesi kuridhika na si wepesi sana kupambana ili kufanya mabadiliko katika maisha yao. Kwa hivi kama mtu ni baba mwenye nyumba..hatari sana.
 • Si wepesi sana kuamini kila mtu ila wakishaamini wameamini na ni vigumu kuacha kuamini kwani tumesema wanaudhaifu mwingine wa kutokupenda mabadiliko katika jamii.
 • Koleriki, Sangwini, Melankoli wana kiburi ambacho kinaonekana wazi, lakini kwa Flegmatiki si rahisi sana kuona kiburi chake na matokeo yake husababisha maafa baadaye.
 • Hali yake ya kuwa na Usiri ndani husababisha kutokufanikisha baadhi ya mambo hata pale ambapo taarifa hiyo inakuwa inahitajika. Kwa makusudi anaweza kaa kimya, kumbuka nimesema anatabia ya kiburi cha ndani.
 • Dada Ziada.
 • Flegmatiki ana tabasabu la kinafiki na si rahisi sana kuwafahmu kirahisi lakini hatari yake ni kuwa hufanya mambo ambayo ni tofauti mtu anachotegemea, Utaishia kusema..."hivi Nelson amefanya nini hiki? Sikuwahi kufikiri kama anaweza akafanya kitu kama hiki."
 • Kisaikolojia yeyote anayekuangalia machoni ni ishara ya ujasiri na uwazi, lakin kwa Flegmatiki ni tofauti kwani hawamwangalii mtu usoni, hii ni hatari kidogo kwani huwezi jua anawaza nini na atafanya nini.
 • Wanaishi lakini si kwa uhalisia zaidi, hawa wajamaa wamejaa nadharia zaidi.
 • Kwa wao maisha yakiwa kama walivyoyazoea ni raha sana kwao, hawapendi mabadiliko kabisa, badala yake mabadiliko yakitokea huwawia vigumu sana kujikita kama hali halisi ilivyo.
 • Ni wepesi sana kuburuzwa na watu wa haiba nyingine.
 • Si wepesi wa kuchukua hatua pale inapobidi, kwa tabia hii hujikuta wanamaisha yaleyale au wasaidiwa kufanya maamuzi katika mambo yanayowahusu na wao wapo kimya tu.
Jembe langu In His Days-R.I.P kaka

Kidogo wanaboa, hata ukikaa naye hana story yani., ni vigumu sana kuishi nao hasa kama wewe ni Sangwini mpenda stori kwani kama wewe unaongea sana wao hukusikiliza tu. Haya ni baadhi ya mambo ambayo hawa wajamaa wanayo, yapo mengi sana sana.


Andika jina la haiba fulani kama vile Melankoli, Flegmatiki, Sangwini au Koleriki ili kuzifahau tabia za watu mbalimbali 
Kila mtu anapaswa kuzifahamu tabia na Haiba ya mtoto wake pindi akiwa mdogo ili umwezehe kuishi na kukabiliana na maisha katika hali zote, waoto hao wanne kila mmoja ana tabia yake, can you depict eachone in his/her group?


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda