Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, October 29, 2012

FLEGMATICS, Ni Rahisi sana Kuchukuliana naye Kuliko Watu wa Haiba Nyingine.

Na Nelson Faustin.
Mtoto wa Raisi-Flegmatiki.
Katika maisha haya, Japo Mungu ametuumba na tofauti za kila aina pia ametupa njia za kuweza kuchukuliana kila mmoja na mapungufu yake. Wataalamu wa saikolojia ya jamii na saikolojia ya mahali pa kazi (socia psichology na occupational psychology) wanaweka wazi kuwa, licha ya mapungufu ambayo kila mmoja wetu anayo, bado lazima tuishi pamoja kwani katika mapungufu yetu kila mmoja ndo anaelewa umuhimu wa mtu fulani na je, unawezaje kuishi na huyu na usiweze kuishi na yule. Si jambo jema kuona watu wanasema, "ni vigumu sana kuishi na mtu fulani" ni kauli ambayo kwa muda mfupi inakuweka mbali na watu.

Hasa katika mahali pa kazi na kwenye familiya zetu au sehemu yeyote ambayo watu wa haiba zote nne watkikutana ni lazima kuna kutofautiana, ishu ya msingi ni kuweza kuzichukua na kuziedit ili tuweze kwenda sawa. Leo tunaenda kuona njia rahisi sana ya kuweza kuchukuliana na Flegmatiki kwani tayari tumeona mapungufu yake na kwa kuwa hakuna mwanadamu ambaye ni kamilifu, yatupasa kuangalia upande wa pili namna ya kuchukuliana na flegmatiki ambaye tunaweza kuona ni sawa kuishi naye ila ni vigumu kidogo hasa kama wewe ni Koleriki.

Mama Geby.
Just take the following kwa kuanzia....
 • Kwanza kabisa, tambua uwepo wao na uwaheshimu kwani si watu wa kutaka heshima sana na kama hutawaheshimu kuna kitu ambacho kwa namna moja au nyingine itakubidi uwe mnafiki au korofi kama ishara ya kujilinda kutokana na namna yao ya kuchukulia mitazamo na maneno yako juu yao.
 • Jifunze tabia yao ya upole na ukimya hata wakati ambapo unatamani sana aseme kitu. Kwa mfano, katika mahusiano ya mume na mke, kama mmoja si msemaji sana na anasema katika nyakati fulani fulani tu, jifunze kulibeba hili kwani bila ya hivyo utajikuta unakwazika kwa kila hatua.
 • Kama,  wewe ni flegmatiki na uanahusiana kwa ukaribu na flegmatiki mwenzako, jitahidi sana kuvunja ukimya na kufanya mambo katika uhalisia wake, bila hivyo mtajikuta mkitengeneza haiba/Personality nyingine ambayo si yenu.
 • Angela and Friends-In a worship.
 • Usiwaonee kutokana na upole wao hata kama hawata kulaumu kwa lolote kwani hiyo ndoyo hulka yao. Kama ukiwalaumu sana wataishia kuweka kiburi ambacho huwezi kukigundua hadi utakapoona matokeo mabaya ya kazi yenyewe.
 • Tumia hekima sana unapowatuma kazi kwani hawana "a Direct No" hivyo kama  wewe ni wa nafasi ya juu zaidi yao, basi mpe nafasi ya kufanya kazi kwa utaratibu ili wasilipue kwa kuogopa. Kama wewe ni mdogo basi angalia hekima kwanza kabla ya kazi ili kuepuka kuonekana huna adabu.
 • Watie moyo kuchukua hatua pale haki zao zinapochukuliwa kwani kwaasili ni watu wa kuridhika sana hata kama wamekandamizwa. Waonyeshe na uwape njia ya kuelekea.
 • Katika eneo la madeni, Flegmatiki hawajui kudai haki yao, kama unadaiwa na Flegmatiki, jitahidi sana kumpa haki yake hata kabla ya yeye kukudai kwani anaweza asikudai kabisa.
 • Kutokana na kuwa, hawana msukumo wa ndani mara nyingi hawawezi kufikia malengo yanayotakiwa, tumia busara na upole katika kumuonesha sababu za kufikia malengo fulani na madhara ya kuridhika kabla ya kufikia mahali fulani.
 • Wapatie majukumu lakini si kuwapa nafasi za kuwa viongozi. Katika eneo la uongozi wape kina Koleriki na si hawa kwani upole wao ni udhaifu katika kuongoza.
 • Unatakiwa kuwa na utulivu unapohusiana nao. Si watu wa kujitoa kwa ukamilifu katika mahusiano na hivyo inasababisha watu kuona hakuna "special touch", lakini ukiwapa nafasi ya kuweka hisia zao vizuri, utafurahi sana.
 • Jitahidi sana kuwaamini na kujiamini unapokuwa nao, usikubali kuwaonesha kuwa huwaamini bali wape nafasi ya kukuona kuwa wewe ni tegemeo na hata wao wanakitu cha kufanya.
 • Usiwakasirishe kwani wakikasirika, ni ngumu sana kuwatuliza. Fanya kila njia kuwaweka katika mazingira ya kutokukasirika, na ukiona hawakasiriki basi usishinikze kukasirika kwao.
 • Mpongeze ili awe na ujasiri wa kufanya vizuri zaidi.
 • Kama kuna kitu  kitaleta mabadiliko, basi waambie mapema ili wajiandae kwa kupamabana na hali yao ya kutokupenda mabadiliko ili mabadiliko yatakapotokea basi waweze kukimbizana na mabadiliko hayo, kinyume na hayo utawaburuza sana.
 • Heshimu mipaka yao.
 • Wape muda wa kutafakari na kufanyia kazi mapungufu yao.
Nyakati za Furaha.
Kagose and Friends.
Hadi hapa, tumefikia mwisho wa safu hii, vipindi vijavyo tutajifunza namna ya Kuboresha haiba, tutajibu maswali ambayo tuliyaainisha katika kipindi cha wakati fulani.


BAADA YA SOMO HILI LA HAIBA, TUTAJIFUNZA MASOMO MENGINE KWA KUJIBU MASWALI YAFUATAYO.

 1. Kama mzazi, Kuna Ulazima wa Kufahamu Tabia/Haiba ya Mwanangu? Kama Inatofautiana na yangu Nifanyeje?
 2. Hivi kwa nini baadhi Watu Waliopendana sana huwa Maadui wakubwa sana Baada ya mahusiano yao kuvunjika? (utapata na ushuhuda wangu hapa)
 3. Kwanini Wasichana Wengi WALEO wanakuwa na mawazo ya kukataa kuolewa tangu wakati wakiwa na umri wa miaka 16+?
 4. Je, kuna Uzuri au Ubaya wowote wa mahusiano ya kimapenzi (Tutapata kuona shuhuda za mahusiano yaliyodumu hadi ndoa na zilizovunjikana na kuleta hasara kubwa sana)
 5. Kwa nini wanaume wengi leo wana Hofu kubwa kuhusu kuoa?
 6. Je, kuna umuhimu wowote wa Msamaha katika jamii?
 7. Itakuwaje kama ndoa ni ya watu wenye haiba za tabia tofauti kwenye makundi tofauti kama vile sangwini na Melankoli, au sangwini na sangwini, au ya flegmatiki na koleriki, nk?Je wanaweza wakaishi pamoja? Na Je, zinadumu?
 8. Tutajaribu pia kuangalia mwanzo na hatma ya "life style ya Usharobaro", na Je, ina sababu zozote za kisaikolojia? Na je walio wa hulka hii Je, ni Masangwini, Makoleriki, Mamelankoli au Maflegmatiki? 
Tunaamini utanufaika sana na safu hii..........
NB: Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA au JINA LA HAIBA/TABIA FULANI kama vile Koleriki, Melankoli au Sangwini au Flegmatiki" kwenye search engine yetu hapo juu ili kupata tulipoanzia hadi tulipo. 
 
Namailizi kwa kusema.......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu, ni zawadi ya KUJITAMBUA (A point of self-Actualization) katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili 
 ya sifa na utukufu wake YEYE mwenyewe.
Unajitambua? Au Unaishi tu kwa sababu siku zinaenda?
KAMA KAWA,, MUNGU AKUTUNZE...0753-038005
sonnelly06@gmail.com
(We are little Beings, trying to give you the little we have)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda