Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, October 30, 2012

Wakristo wa Coptic Misri..-..Dhehebu La Kikristo Nchini Misri Linalopambana na Changamoto Nyingi, Licha ya hayo, Leo wanamchagua Papa.


Pope akiwa Kiroho zaidi.
Na Nelson Faustin.
Wakati Marekani wakipambana na dhahma ya kimbunga cha Sandy kilichofanya hata kampeni za uchaguzi ziahirishwe, Umma wa wakristo dunia nzima unaelekeza dua na maombi yao kwa wakristo wa madhehebu ya Kikoptiki wanafanya uchaguzi kumchagua Papa atakayekuwa mrithi wa hayati Baba mtakatifu Pope Shenouda III aliyefariki akiwa na umri wa miaka  88 mnamo tarehe 17 March 2012 na alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa, hii ni katika kuhakikisha kuwa wenzetu wanapata kiongozi ambaye atalisimamia dhehebu hili kwa nguvu zote kwani changmoto ni kubwa sana.

Je, Kiongozi huyu anapatikanaje?
Tumwombe Mungu.
Uchaguzi huu ambao kidogo ni tofauti na chaguzi za madhehebu mengine japo kuna vitu vichache ambavyo
vinaendana na uchaguzi wa Baba Mtakatifu wa kanisa Katoliki. Katika huu unaoendelea sasa ni kwamba, yapo majina matatu ambayo yataandikwa na kuwekwa katika altare kuu iliyopo katika kanisa kuu la St Mark's Cathedral mjini Cairo. Baada ya kukamilika kwa hatua hii ya kwanza, sala na dua zitadumu kwa kipindi cha siku tatu hdi nne na Mnamo Novemba 4 mwaka huu atachaguliwa mtoto ambaye atafungwa kitambaa usoni na baadaye atachukua kikaratasi chenye jina moja na huyo ndiye atakayekuwa Baba Mtakatifu wa dhehebu hilo na sherehe za kumweka wakfu zitafanyika Novemba 14 mwaka huu.

Mahubiri.
Nani amepata bahati hii inayoonekana Takatifu?
Waliobahatika kuingia katika nafasi hii ya kupiga kura kupata wateule hao watatu ni watu wa nyadhifa mbalimballi kama vile viongozi wa kanisa, viongozi wa serikali na wakakilishi kutoka katika kanisa la Kiethiopia lililo katika uhusiano wa karibu na dhehebu hili. Kwa pamoja waliwachagua Bishop Raphael, mwnye umri wa miaka 54 aliyekuwa msaidizi katika ofisi ya hayati papa Shenouda III na mjumbe wa Sinodi takatifu ambayo ipo katika uongozi wa juu wa dhehebu hili, pia Bishop Tawadros, mwnye umri wa miaka 60 aliyekuwa msaidizi wa kaimu askofu mkuu wa sasa Pope Pachomios na monk toka Alexandria  padri Raphael Ava Mina mwenye umri wa miaka 70 na yeye ndiye mzee kuliko wote japo wadhifa wake si kama wenzake wawili na inategemewa kuwa, kutokana na hali ya kisiasa nchini Misri, uongozi mpya utakuwa kiungo muhimu sana baina ya jamii na raisi mpya atakayechaguliwa nchini Misri.


Hali ikoje nchini Misri kwa sasa?
Tupige Kura.
Kwa mujibu wa  volunteer Shaker Talaat ni kuwa, chaguzi zote zimekuwa zikifanywa katika kipindi kigumu na hata sasa kutokana na hali halisi nchini Misri baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa dhidi ya utawala wa Hosni Mubarak, na hata sasa kutokana na wimbi la uislamu madarakani linaathiri maendeleo ya kanisa hili alisema  bi Magdy Helmi, (53) mwakilishi wa dhehebu hili kwenye moja ya majimbo ya dhehebu hili akiwaeleza waandishi wa  Reuters. 

Kanilsa la Wakoptiki.
Pope Shenouda III aliongeza kwa miongo 4 na alifanikiwa kupambana na changamoto zote zilizokuwa zikilikumba kanisa na kiongozi anayeingia madarakani anakutana na changamoto ya kuhakaikisha kuwa kasi ya ukuaji wa chama cha Islamic Brotherhood, lakini pia changamoto nyingine ni kutokana na matazamio vijana juu ya kazi atakayoifanya kiongozi huyu katika kuhakikisha kuwa dhehebu hili linaendela kusitawi.

Sisi tunajifunza nini?
Viongozi wa Kikoptiki.
Kwa nchi kama Tanzania, hatuna sababu ya kuacha kumwomba Mungu na kujitahidi kuimarisha Ukristo kwani kuna wenzentu ambao ni wa nchi kama Misri na Nigeria ambao wanachangamoto nyingi sana ikiwemo ya Boko haramu na mengine mengi. Tujitahidi sana kila mmoja katika nafasi yake kuhakikisha kuwa, tunatunza kile ambacho Mungu ametupa. Sidhani kama kuna sababu ya kulumbana kutokana na tofauti zetu, sidhani kama kuna sababu ya kuwaacha watu wachache waharibu ile sifa ya "Ukristo", bali tuwasaidie kwa kuwaelimisha kwa busara ili tuendelee kuwa pamoja. Changamoto zilizopo hazihitaji siasa bali zinahitaji busara na maombi ili kuweza kuzishinda.Huko Marekani- Lep
  • A tropical storm is classified as a hurricane when wind speeds reach 74mph
  • A hurricane can expend as much energy as 10,000 nuclear bombs over its lifecycle
  • The hurricane's spiral is due to the Coriolis Effect, which is generated by the Earth's rotation
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda