Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, October 19, 2012

Bado Mungu Anaipenda na Kuihurumia Tanzania, Tusiogope Bali Tuamke na Kujali kile Mungu alichotupa kama Zawadi. (Picha za Maombi ya Kitaifa yaliyofanyika Arusha)Na Nelson Faustin.
Kimtihani zaidi-St. Joseph G. Sem.
Wakati mabomu yakiendelea kurindima kule kariakoo na posta na maeneo mengine ambapo taifa zima linashangaa kwa yale tunayoyaona kwani hatujazoea kuona hali kama hii, wakati huo huo kuna wadogo zangu wa kidato cha nne kule St. Joseph's Girl's seminary Mwanza wakati huu huu siku hii ya leo wanafanya mahafali yao ya kumaliza kidato cha nne wakiwawakilisha wanafunzi wote ambao wamemaliza elimu yao ya O-level ili waje nao tushirikiane nao katika mshangao huu humu duniani ambapo hatujui itakuwaje ila Mungu ndiye ngome yetu siku zote na hakika ana majibu kwaajili ya watu wake wote.

Sir Nelly., Mode, Agy, Janeth na Sister.
Siku moja baada ya mtoto mmoja kukojolea Q'uran yani Jumamosi tarehe 13 Oktoba 2012 pale uwanja wa shekh Amri Abeid Arusha kulikuwa na kazi kubwa ambayo iliandaliwa na kituo cha maombi cha radio safina na katika hili mimi mwenyewe niliyehudhuria naona thamani ya muda tuliotumia kama taifa kukaa pale uwanjani na kumwambia Mungu kwa habari ya Tanzania kuhusu amani yetu, hali yeu ya kiuchumi, hali yetu ya kisiasa, mahusiano yetu ya kidini na kadhalika.
Maelfu wakimwita BWANA YESU for Tanzania.

Maombi hayo yalianza saa tatu hadi saa nne mchana na watu walitumia nafasi hii kumwita Mungu kwa habari ya toba juu ya madhabahu ambazo kwa kujua au kwa kutokujua zilijengwa na viongozi wetu hali ambayo inasababisha taifa letu liwe na hali iliyonayo leo. Pia tuliomba sana juu ya roho ya udini na hali yoyote ya kisiasa ambayo inatufanya tufike hapa tulipo leo. Kwa pamoja tuliomba toba juu ya madhabahu hizo na kuliweka wakfu taifa chini ya uangalizi wa Roho Mtakatifu bila kujali dini zao, makabila yao, itikadi zao kisiasa, maeneo watokayo, lugha zao na hata hali zao za kitaifa.

Wapendwa wakisemezana.
Ninachoona leo ni kuwa, kama si maombi yale na maombi ambayo yamekuwa yakifanywa na watu mbalimbali kwa habari ya taifa letu ambalo ninauhakika kuwa Mungu analihurumia sana napata sababu ya kusema kuwa, hata sasa Mungu amewasikia watu wake na hakika hataacha hata mguu wa wenye haki wake usogezwe, si wa waislamu, si wawakristo, si wa kabila lolote kwani yeye ni Mungu wa wote wenye mwili.


Ilikuwa ni Kuvunja, kung'oa na Kuharibu hila za Ibilisi.
Nilitiwa moyo sana na watu wengi waliohudhuria maombi hayo ya kuliombea Taifa kwani uwanjwa mzima kwenye ngazi, jukwaa kuu na kwenye majani palijaa kabisa.

Ndugu zangu, hali ya taifa letu kwa sasa si nzuri sana kwani kuna kitu ambacho hatupaswi kukiacha kikue Tukiyaacha haya mwisho wa siku tutashindwa kuishi pamoja kama ndugu kitu ambacho ni desturi yetu. Kila asiyependa hali hii, aikatae kwa kutumia simu yake, facebook, twitter, blogu, web na kiiiiiiiiila mbinu ambayo kibinadamu inawezekana lakini zaidi sana kumwomba Mungu atupe kile alichotuzawadia kama taifa. Kama wewe ni mkristu, take time and talk to at least one of any person whom you think he/she has a link to what we are facing today.
Kushangilia Ushindi wa Ukombozi wa Tanzania.
Asanteni sana Radio Safina kwa maono ya kuliombea taifa, pia Mwl. Mwakasege na watu wote wa dini zote, makabila yote na vyama vyote vya siasa, kwa kuendelea kuliweka taifa hili Mbele ya uso wa Mungu. Tusikubali kuchezewa na Ibilisi, Bado tuna mengi ya kufanya katika harakati za kulikomboa hili taifa..Mungu awabariki sana.

Hadi watoto walikusanyika kumwita Bwana.
 .
Njaa Haikuwa sababu ya Kuacha taifa liingie kwa hali unayoiona katika Picha hizi.Mungu bado Anawapenda Hawa ndugu zetu,,,,,TusiwachukieTukipokea Maelekezo ya jinsi ya kuzivamia Ngome za Ibilisi.


Tutafakari Ukuu wa Mungu Juu ya Tanzania.


Nikakutana na Ze Blogger mmasai, tukachart kidogo....


wanafunzi wangu wakijiandaa kuwa kidato cha nne mwakani, hawa Wanajifunza nini juu ya Tanzania ya leo?

Tujifunike Jua ila hapa Hadi Mbingu zituelewe.
Lango la Kuingilia Uwanjani, watu walifurika.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda