Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, October 28, 2012

9 Wakamatwa kwa Ujangili Yaeda Chini


Na Mary Margwe,
Mbulu
 
Jeshi la Polisi Wilayani Mbulu, Mkoani Manyara  inawashikilia watu 9 wanaosadikiwa kuwa  ni majangili kwa tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali kama nyumbu 5  na kanga 3 wakiwa na thamani ya zaidi ya sh. Mil.3.2, huku wakiwa na silaha, magari 2 na mmoja wapo akiwa na sare pea 3 ya Jeshi la wananchi Tanzania (JWT), ambapo kesho wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.
 
Kwa mujibu wa Afisa wanyama pori wa Wilaya ya Mbulu, Mkoani Manyara, Bw.Allan Shanny alisema kuwa watuhumiwa wa ujangili huo walikamatwa jana  majira ya saa.12 za asubuhi huko katika pori la hifadhi bonde la Yaeda chini, Wilayani Mbulu.
 
Bw.Shanny alisema alipata taarifa kutoka kwa wananchi wema, ambapo alitoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) George Kyando na kuchukua hatua mara moja ya kutuma askari na kuwakamata watuhumiwa hao 9 wa ujangili.
 
Aidha aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Bw.Juma Rashid (56) Mnyaturu mkazi wa Singida, Bw. Kukuni Wadee (30) Msukuma wa Geita ambaye yeye alikutwa akiwa na sare PEA 3 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWT), Bw.Greyson Msengi (61) Mnyiramba wa Singida, Bw. Raphael Matola (53) Myao wa Shinyanga, Bw. Shaban Omari (30) Mnyiramba wa Kijiji cha Dominiki Singida ambapo kesho Bw.Shani alisemwa kesho watafikishwa mahakamani.
 
Aliwataja wengine waliojitetea kuwa wao waliitwa kama mafundi wa kutengeneza magari na sio watuhumiwa wa ujangili ambao ni pamoja na  Bw. Bakari Mbwana (30) Mdigo mkazi wa Singida, Bw. Omari Abrahamu (57) Mnyaramba  wa Singida, Bw. Zosmos Patrick (33) Mnyaturu wa Singida na Bw.Adamu Issa (27) Mnyaturu wa Singida.
 
Bw. Shanny alifafanua kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na silaha (bunduki) aina ya short gun (na risasi zake 5), Mark 1V, panga 6, visu 4,  huku wakiwa na tochi kubwa 3, sufuria 5, na unga wa mahindi debe 2 ,na magari 2 aina ya Land Rover  TID lenye namba za usajili T652 APK, lililokua likiendeshwa na Bw. Raphael Matola (53) na huku gari lingine lenye namba za usajili T161 ARR likiendeshwa na Bw. Zosmos Patrick (33) huku wakiwa na wanyama aina ya nyumbu 5 na ndege aina ya kanga 3, wote wakiwa na thamani ya jumla y ash. Mil.3,209,480/=.
 
Aidha Bw. Shanny alisema kwa mujibu wa sheria ya wanyama pori ya mwaka 2009 inakataza shughuli za uwindaji haramu isipokua ni kwa kibali maalum (leseni ) tu, na kutoa mfano kuwa “ jangili akikamatwa anatozwa kwa dola za kimarekani kwa lengo kumshikisha adabu ama kama ni  fundisho ili asirudie tena, hivyo nyumbu mmoja kwa bei ya kitalii ni dola 400 ambapo ni sawa na sh.623,200 za kitanzania, ambapo kwa nyumbu 5 ni sawa n ash.3,116,000 za kitanzania” alifafanua Afisa Wanyama pori huyo.
 
Kwa  upande wa kanga mmoja Bw.Shanny alisema  ni sawa na dola 20 ambapo ni sawa na  sh.31,160  ambapo kwa kanga watatu ni sawa na sh 93,480/= ambapo alisema iwapo wangeingia kwa njia ya uwindaji halali wa kuwa na leseni  bei yake ingekua ni tofauti na kiwango hicho cha utalii.
 
Akielezea hali halisi ya ujangili katika bonde hilo la Yaeda chini alisema ni kubwa hususani kwa wanyama kama tembo kwa ajili ya meno  na wanyama wengine kwa ajili ya kufanya biashara kama kitoweo, ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira kwa uvamizi holela.
 
“Pamoja na upungufu wa watumishi wa sekta ya wanyama pori Wilayani hapa  lakini wananchi wamewezeshwa kupata elimu ya uhifadhi wa mazingira na ndio maana wanatoa ushirikiano  mkubwa Serikalini  juu ya matukio ya ujangili pamoja na uvamizi  wa maeneo ya hifadhi”alisema Bw.Shanny.
 
Hata hivyo aliendelea kufafanua kuwa katika hali ya kukabiliana na ujangili huo Serikali Wilayani Mbulu, Mkoani Manyara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi akitolea mfano wa Shirika lisilo la Kiserikali la uhifadhi wa wanyama pori la Afrika (WMA)  pamoja na TANAPA  kwa kuliona hilo wameanza kutoa elimu shilikisha ya jumuia ya uhifadhi ya wanyama pori, ambapo tayari vijiji 6 vimeshirikishwa kuunda jumuia hiyo itakayosaidia kukabiliana na hali ya ujangili katika bonde hilola yaedachini.
 
Alivitaja vijiji hivyo kata kwenye mabano kuwa ni pamoja na Kijiji cha Endanyawish (Masieda), Mongo wa Mono(Yaedachini), Yaedachini (Yaendachini), Domanga (Eshikesk) Eshikesh (Eshikesh) pamoaj na Endagulda (Eshikesh).
 
Hata hivyo aliwashukuru wadau mbali mbali waliotoa ushirikiano  wa kufanikisha zoezi mihimu la kuwakamata watuhumiwa wa ujangili ikiwa ni pamoja na wananchi wenyewe, Jeshi la polisi Wilaya chini ya OCD  Mbulu, George Kyando, na AWF na TANAPA kwa kuwawezesha mafunzo mabambali.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda