Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, September 26, 2012

SIKITIKO LANGU LEO NI JUU YA BINADAMU "WALALAMISHI na WENYE MANUNG'UNIKO YASIYOISHA" (Complainers in All aspects)

.........................Basi yatendeni mambo yote pasipo manug'uniko yeyote........Mungu ni mwema sana kwani ametukutanisha tena katika mtaa huu wa kujiweka sawa kwani kutokana na maisha kuwa na michanganyo ya aina yake, kila mmoja anatatufa tabia ambayo ataweza kuwanayo ili na yeye aweze kupambana na changamoto za kimaisha tulizonazo.

Kutokana na changamoto hizo utawakuta wengine wameamua kumshika Mungu kabisa kabisa kwani kwa imani yao hilo ndo tumaini la pekee, wengine ponda mali kufa kwaja, wengine ni kupambana kihalali mpala kieleweke, wengine wameamua kuwa mafisadi na wazulumishi, wengine wameamua kuwa na ubinafsi wa kutumia kile kidogo kwaajili yao peke yao, wengine wamechagua kuishi maisha ya kuishi misha ya kubangaiza ilimradi siku zinaenda wakisubiri neema ya Mungu, wengine wameamua kuwa wategemezi hata katika umri mkubwa liwalo na liwe.

Makundi yote niliyokutajia hapo juu kila moja lina idadi ya watu ya kutosha wanaume kwa wanawake, wazee kwa vijana, wasomi kwa wasiosoma, nakadhalika, lakini kundi ambalo leo nitalizungumzia japo kwa ufupi sana ni wale ambao kutwa kuchwa ni walalamishi na wanung'unikaji katika kila jambo.

Kila mtu anajua kuwa, kila mwanadamu ana wajibu wa kupambana na maisha yake mwenyewe hata kama kuna mtu ambaye anatakiwa kuwa na wewe katika maisha yako na hajakuwepo basi usinung'unike. Kuna watu ambao sikuzote wapo katika kulaumu, watalaumu sana utasikia mara serikali hii bhana haina hata njia za kuwasaidia raia wake, oh mara wazazi wangu ndo chanzo cha mimi kuwa masikini, oh mara bongo hata ukisoma maisha ni magumu tu, oh mara boss ni mkorofi pindi boss anapotaka perfection kwenye kazi, oh mara dunia imekuwa na wadanganyifu wakutosha, oh mara michango imekuwa mingi sana mara zaka, mara ujenzi.........nakadhalika........

Kulalamika au kulaumu si dhambi bali dhambi ni kulamu au kunung'unika na kuacha kufanya mambo ambayo yatakufanya utoke hapo ulipo na kuwa na maisha ya utofauti na yenye utoshelevu kwako na kwa familiya yako na wote wanaokuzunguka. Kuna watu ambao kila kitu lazima wanung'unike hata kama wanauwezo wa kufanya kitu fulani. Hapa hatuwaangalii wale ambao hawana shughuli za kipato cha kuwapatia kipato bali hata wenye uwezo nao wamo.

Inawezekana kuishi maisha ambayo hayana maung'uniko au malalamiko. Unafanyaje? Nadhani wewe na mimi tunajua kuwa hata kuna mazingira mengine ambayo hata unung'unike kiasi gani, maisha yatabaki yalivyona utaishia kumkosea Mungu bure, yanini ujitese kwa mambo yapitayo? Kama unaweza kufanya, fanya lakini kama huwezi basi acha na ufunge kinywa chako au utoe maelezo ambayo si ya kulalamika bali ni yakuonesha hali halisi. Inawezekana kabisa kuwa na maisha ambayo hakuna mtu ambaye atakufanya ulalamike kwani utakuwa unafanya kwa nafasi yako wewe kama wewe na  ukikaa vibaya utaona kila mtu ni mubaya wako.

Ukikutana na jambo lolote, kabla ya kuanza kulalamika, uliza kwanza nani aahusika, kama ni wewe basi fanya, kama hakuna wa kufanya basi achana nalo kwani kama halikuhusu na halikudhuru japo unatamani kifanyike na hakifanyiki kama inavyotakiwa basi achana nalo kwani hata katika kulalamika hakuna mtu wa kukusaidia. Wale ambao hawana hamu ya kujishughulisha na kuona matunda ya kazi zao huku wakitarajia watu wengine wawasaidie. Hawa watu kutwa kuchwa ni wanung'unikaji tu hata kama wamesaidiwa bado msaada kwao hautoshi na nataka nikwambie kuwa, kama hii ni tabia yako, kuiacha itakuwa ngumu sana na ukishazoea una matatizo makubwa sana. Mungu akusaidie.....

Huwezi piga hatua katika maisha kwa kuishi maisha ya aina hii hata kama Mungu kakujallia akili na nguvu na kumjua na kuwafahamu watu na kuwa na network kubwa lakini kwa kweli kama ukiwa na tabia kama hii;-
  • Watu watakukimbia kila siku.
  • Unapata matatizo ya sonono au kwa kiingereza "depression"
  • Unapunguza uwezo wako kufikiri na kutumia vipaji vyako ipasavyo.
  • Maisha yako yatakuwa hayana uhalisia na utakuwa unaishi tu kwa sababu wengine wanaishi.
  • Siku zote maisha yako yatakuwa na msongamano, huwezi kuwa huru kabisa.
  • Uwajibikaji kwako itakuwa ni hadithi.
Hayo na mengine mengi, ila cha msingi ni mimi na wewe tuone kuwa kuwa tuna kila sababau ya kutafsiri na kutafakari kuwa maisha bila manung'uniko na kalalamika mara kwa mara yanawezekana, kila mtu aone kuwa ana kila sababu ya "kutimiza wajibu wake kwa hali na mali" usipate muda wa kuona kuwa mtu fulani au kikundi fulani au Mungu ni chanzo cha mateso yako hapa duniani. Pambana, maisha yako ni ya kwako mwenyewe na huna sababu kumlaumu mtu kwa lolote, piga kazi tafuta njia za kutoka. 

Lakini pia, kila mara unatakiwa kujua kuwa, hata kama Mungu amekujalia uwezo, usitoe kwa manung'uniko kwani hujalazimishwa bali do what you are willing to do na si kila mara usipotoa mambo hayataenda, NO...unaweza usitoe na mambo yakaenda, usiilaumu serikali kwa lolote, usimlaumu Mungu, usilalamike kwa lolote bali tafuta sababu ya kufanya mambo yakupe sababu ya kuishi kwa amani na kwa utoshelevu...


Count your words............................Barikiwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda