Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, September 12, 2012

SIKITIKO LANGU LEO LI JUU YA "WANADAMU WABABAISHAJI".

a.k.a MEKU. Photo by Saphy Elton.
Salamu kwa ndugu wote wapenzi wa Ohayoda, kwa bahati mbaya tulishindwa kuwafikia kwa siku kadhaa kutokana na majukumu ya "Haydom Cultural Festivals" ambayo yalimalizika salama, mwanadamu atapata sifa ila Utukufu wa Mungu hatugusi kwani yeye ndiye aliyewezesha haya yote. Pole kwa wote ambao hamkuweza kufika lakini muamini kuwa kila mwaka itakuwepo na hii itakuwa ni kutoka utukufu hadi utukufu.
 
 Japo Mdau mmkuu m-ohayoda mwenyewe Mh. Amani Paul Gasseri aliyekuwa "vision Bearer" ameshawashukuru wote lakini sina budi kuwashukuru "the dream team", 4ccp, wana Haydom wote na washiriki wote, Mungu awatunze tuonane tena mwakani.

Maisha yanapozidi kuwa magumu, kuna kundi la watu linaongezeka kila siku. Namshukuru Mungu kwani nimepata vision ya kuzungumzia haya makundi kila jumatano kwani makala ya sikitiko langu imehamia siku ya jumatano ili kuipa nafasi "Papaa on tuesday" http://www.samsasali.blogspot.com/2012/09/papaa-on-tuesday.html  iweze kufikisha ujumbe tarajiwa.

Ndugu zangu, hakuna kitu kinakera kwa watu wote hata kama wewe ni mzazi, mlezi, mfanyakazi, boss, mtumishi wa Mungu, babu, bibi, mwanafunzi, mwalimu, daktari, nesi, mzungu, mwafrika au mtu mwingine awaye yote kuwa "MBABAISHAJI". Huyu si mwongo kwa uhalisia ila ni watu ambao wanajua kitu fulani hakiwezekani lakini bado wanakupa uhakika kuwa bado kinawezekana na wewe unakuwa na matumaini kuwa kinawezekana ila utajua kuwa hakiwezekani baada ya kuona kuwa hakijawezekana au kimewezekana lakini kwa sehemu tu, hii inaboa sana kwani hawa watu wanashindwa kuwa katika uhalisia  au "failing to be realistic". Na hawa si wanasiasa bali tunaangalia maisha ya kawaida kabisa kabisa huku mitaani.

"The Dream Team ndani ya Jezi, TRUE PIPO"
Amani, Lucy na Saphy katika Pozi la 1940's
Kwa mfano mkaka unajua kuwa hutamwoa mdada fulani lakini unakuwa unazugazuga naye kimtindo tu hadi unampotezea muda tu na kwa wadada likewise, au boss unajua kuwa issue fulani haiwezekani kabisa lakini bado unatoa matumaini wakati unajua haiwezekani, siuseme tu...jamani ishu fulani ni ngumu ili watu wajipange na lingine?, au unamkuta fundi anajua kabisa kitu fulani kwa leo hakiwezekani lakini bado anasisitiza tu eti...subiri dakika sifuri nitafanya..au unamkuta mtu ambaye umempa dili afanye na bado ana mengine ya watu kibao kapokea lakini katika trend hiyohiyo anakwambia usijali kabisa lazima nitafanya, mwisho wa siku anaanza kukuzungusha..ukimuuliza anajing'atang'ata...kwa nini usiseme sintaweza kuliko kusumbuana? au unajua kabisa huna hela afu anakuja swahiba wako na anashida sana badala ya kumwambia kuwa kwa sasa huna,,,unamwambia ngoja niangalie...unaangalia nini wakati milango yote imefungwa? au mwanafunzi mwenzako anataka umpige tafu kwenye pepa na wewe unajifahamu huwezi au huna huo uwezo, unamwambia hakuna shida mtasaidiana..mjamaa hasomi akisubiri kusaidiwa a.k.a "kudesa" lakini mkiingia kwenye pepa unamchunia..siungemwambia tu haiwezekani ili ajipange kivingine? Kama unajua huna mchango wa harusi au harambee, ya nini uwafanye watu waaamini kitu ambacho hakipo? unawakwamisha wengine bhana,,,,,,,

Japo kuna saa inakuwa ngumu lakini kuuona ukweli na kuutendea kazi ni jambo la maana sana kwani utapata faida kama vile:-
 • Inakupa Neema ya kuwa karibu na Mungu.
 • Inakupunguzia idadi ya maadui.
 • Inaongeza thamani hata kama huna kitu.
 • Inakuweka katika nafasi ya kukaa mbali na wababaishaji.
 • Inakupa uhuru wa kuwa huru na mambo yako na hii si kuwa mbinafsi kwani unafanya kile unachokiweza.
 • Unapata fursa ya kuwa wewe kama wewe na si mtu mwingine. nk
Ninaishia hapa.....cha msingi kila mtu ajitahidi kuwa "realistic" hata kama watakutemea mate na kukuona hufai lakini usiahidi kitu ambacho unajua hakiwezekani. Si lazima udanganye au utoe matumaini kwenye ktitu ambacho hakina uhalisia. 

Dondoo za kukusaidia:-
 • Fikiri sana kabla ya kusema.
 • Mwombe Mungu akupe njia rahisi ya kulisema jambo fulani hata kama halitakuwa basi Mungu atafunika.
 • Angalia unasema nini na kwa nani..ili wasije wakakutatisha tamaa badaye.
 • Usiongozwe na hisia bali uhalisia (stop being emotional)
 • Kama huna uhakika...usiseme kumridhisha mtu bali Funga mdogo.
 • Sema machache tenda mengi..hii inajenga heshima.
 • Acha kuweka siasa katika maisha ya kawaida.
 • Kama huna au huwezi basi yaache yalivyo usije kwama mahali ambapo hutaweza kutoka baadaye.
 • Soma kitabu cha mithali kitakusaidia.
NB: Kundi lingine lijiandae Jumatano ijayo............

UKWELI NA UHALISIA UTAKUWEKA HURU nawe UTAKUWA HURU KWELI KWELI KAMA UNABISHA, KUWA MBABAISHAJI UONE.
Hatimaye Historia ikaandikwa katika mkoa wa Manyara...kuwakusanya watu wote hawa si kazi rahisi...ndo mana tunasema Sifa na Utukufu kwa Mungu...Nipo kwa sababu Upo. 


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda