Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Saturday, September 1, 2012

SAKATA LA UTEKAJI HAYDOM LACHUKUA SURA MPYA


  • Kikao chavunjika asema yupo salama watu wasiwe na wasiwasi
  • Aongea kwa simu na mke wake na watu wengine, asema yupo Tabora
  • Alitoa hela kupitia ATM Mwanza, na kuweka hela Shinyanga
  • Hali ya SINTOFAHAMU yazidi kutanda Haydom na vitongoji vyake

Hhando Samo anayesemekana ametekwa na watu wasiojulikana
Hali ya SINTOFAHAMU inazidi kutanda kwa wananchi wa Haydom baada ya taarifa mbalimbali kuzidi kuwachanganya wananchi hasa ukweli wa sakata hili. Tukio hili ambalo limegusa hisia za watu wengi na kukusanya maelfu ya wananchi kutoka vijiji zaidi ya 11 katika tarafa ya Haydom na maeneo ya jirani lilitokea usiku wa kuamkia jumanne tarehe 28 Agosti ambapo mfanyabiashara maarufu Hhando Samo mwenye makazi yake Haydarer na Haydom alipotoweka katika mazingira ya kutatanisha huku ikiaminika akiwa na kiasi kikubwa cha fedha.

Taarifa zilizoifikia Ohayoda zinasema kuwa, mfanyabiashara huyo alikuwa akitokea Singida  pamoja na wafanyabiashara wengine wanne wakiwa katika gari dogo aina ya SUZUKI escudo mali ya Bw. Samo na walifika Haydom jioni. Inasemekana kuwa alipokuwa Singida Samo alitoa fedha benki na kumkabidhi Korneli kiasi cha shilingi milioni moja na laki mbili kwa ajili ya kununua pikipiki. Baada ya kununua pikipiki Korneli alitangulia kwa pikipiki hadi walipokutana Haydom. Habari zaidi zinasema kuwa waliachana hapo haydom na Hhando Samo aliondoka kwenda nyumbani kwake Haydarer na ndipo alipotekwa katika eneo la Qorong'ayda.

Katika hali ya kushangaza Hhando Samo alimtumia mke wake ujumbe wa simu kupitia simu yake ujumbe unaosema kuwa "Nimetekwa na gari langu tumeliacha Ilongero (Singida) nikiwa na shilingi milioni 84, sasa hivi sijui twaenda wapi ila tumepita Itigi", ujumbe ambao ulizua maswali mengi kuwa inakuwaje atekwe halafu aweze kutuma ujumbe huo? Wakati bado hali hiyo ya SINTOFAHAMU ikiendelea, wananchi wa Haydom kwa kushirikiana na Polisi walienda hadi msitu wa Ilongero na kulikuta gari likiwa lipo salama, limefungwa na funguo zikiwa ndani na kisha gari hilo kupelekwa kituo cha polisi Haydom.

Wakati wananchi wakiwa katika harakati za kutafuta na vikao vikiendelea katika eneo la Qorong'ayda, wananchi walipiga kura ya siri kwa watu wanaoshakiwa na mshukiwa moja ambaye ni dalali maarufu wa mazao anayeitwa Kasi alipata kura zaidi ya 15 na wakati anahojiwa maelezo yake yalizidi kumweka matatani mbele ya wananchi hao wenye hasira hali iliyopelekea polisi kuingilia kati.

Aidha taarifa za kuchanganya zaidi zinaeleza kuwa siku ya Jumatano, fedha zilitolewa katika akaunti yake kupitia ATM ya Mwanza na picha za CCTV zikaonesha kuwa aliyetoa fedha hizo ni Hhando samo mwenyewe na kisha kesho yake fedha zikaingizwa benki Shinyanga.

Wakati wananchi wakiwa wamekata tamaa ya kupatikana kwa Bwana Samo, usiku wa kuamkia leo alimpgia simu mke wake na watu wengine akieleza kuwa yupo Tabora anaumwa na kuwa Mke wake auze kila kitu akamchukue. Lakini utata zaidi unakuja zaidi kuwa simu hiyo inakuwa hewani anapoitumia yeye tu.

Hali ya taharuki inazidi kutanda na kukiwa hakujulikani kama ni katekwa na kajambazi kweli au kuna lingine la zaidi, na bado wananchi wanaendelea na kusaka kama kuna wahusika katika tukio hilo huku maswali yakiwa mengi kuliko majibu.

Tukio hili kama ni tamthilia basi imetengenezwa Hollywood maana visa, mikasa na vituko katika sakata hili havieleweki na mkasa moja huishia hewani na kisa kingine huibuka, ila kinachowachanganya zaidi wananchi ni jumbe na mawasiliano anayoyafanya na familia yake na utata juu ya usalama wake.

Katika hatua nyingine, kikao kilichokuwa kinaendelea kimevunjika muda mfupi uliopita kimevunjika baada ya Hhando Samo kuongea na mke wake na watu wengine kwa njia ya simu na kudai kuwa yupo Singida na kuongeza kuwa mtu yeyote asitiwe nguvuni kuhusiana naye kwani yupo salama huko Tabora na kuwa watu waliomteka wamemwachia na anaendelea na shughuli zake na baada ya siku mbili ataeleza alipo. Kufuatia taarifa hiyo kikao hicho kimevunjika hadi taarifa zaidi zitakapopatikana huku wadau wengi wakihoji kama kweli ni yeye au hata kama ni yeye kama je alitoa hizo taarifa pengine kwa kushurutishwa baada ya washukiwa kuwekwa kikaangoni.

Ohayoda itazidi kukujuza juu ya sakata hili kadiri moda utakavyoruhusu ila kwa sasa hiyo ndiyo picha kamili...katekwa kweli? au Kajiteka?

Nikiripoti kutoka viwanja vya CCM Haydom ambako vikao vya upelelezi vikiendelea kukiwa na makundi matatu ya vijana, wazee na kina Mama....mimi ni Amani Paul


Usikose kuhudhuria Tamasha la Utamaduni Haydom kuanzia tarehe 6 mpaka 8 Septemba 2012 katika viwanja vya 4CCP Haydom. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda