Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, September 5, 2012

Power Mangwana? "Toka Ujambazi Sugu" hadi kuwa "Muhubiri Mashuhuri". Wakazi wengi Mjini Haydom Wafurika kumwona.

Na Nelson Faustin Nd.
Mtumishi wa Mungu-Power Mangwana.
Ni siku nyingine nzuri ya kupendeza ambayo tunapata kufahamu yaliyojiri huku kwetu Haydom. Mungu anawatu wake na katika hili utajua kweli Mungu ni mkuu sifa na utukufu kwake kwa yale ayatendayo.

Kwa wale ambao ni wafuatiliaji wa mechi za mpira wa miguu ligi kuu ya Uingereza na Ligi kuu Tanzania Bara kupita radio free Afrika na Kiss Fm mtakubaliana na mimi kuwa, kuna mtu anaitwa Power Mangwana. Nilikuwa namsikia sikia tu bila ya kujua alitokea wapi kwani kuna kahistoria ambacho kichwani mwangu bado kalikuwa kanatawala, kwani nilimfahamu kama Jamabazi la kutisha sana lakini nilipomwona jana nilimtukuza Mungu kwa kweli.

Leo alhamisi Mtumishi wa Mungu Pawa Mangwana aliyekuwa Mtumishi wa Ibilisi kwa muda wa mika kumi na tano bila likizo atakuwa na semina ya Neno la Mungu hadi Jumapili hapa mjini Haydom-Manyara. Historia yake inatisha kidogo kama wengi mnavyofahamu lakini nitawapa kidogo na zaidi sana utapata wiki ijayo tutakapoweka makala (documentary) ya mahojiano yake na OHAYODA ili jamii ifahamu kazi hasa Mungu anayomwezesha kuifanya kwa Taifa la Tanzania.

Mtumishi akipokelewa madhabahuni na mdhamini wa Semina hii.
Kama ilivyokuwa kwa mtume Paulo enzi zake alipokuwa akiitwa Sauli, Clemence a.k.a Power Mangwana ni muha wa Kigoma anayeishi na kufanya kazi zake katika mkoa wa Mwanza. Kwa miaka kumi na tano amekuwa akiusumbua sana ulimwengu katiaka mataifa kumi na mbili kutokana na shuguli yake ya Ujambazi sugu, hapa alitoa madaraja ya wahalifu wa aina hii akasema kuna mdokozi, kibaka, dongo na mwisho Jambazi ili kuonesha hatua gani ambazo watu huanzia tabia hii.Dhahama na chanzo cha yeye kuingia atika dimbwi hili la ujangili lilianza pale alipokuwa darasa tano "alimbaka mwalimu wake" akatoroka na kukimbilia Uganda akakutana na mwajeshi aliye staf toka katika jeshi la Idd Amin ambaye aliahdi kumsomesha kumbe "Somo" alilompa ni somo la "Ujambazi" na akaifanya kazi hii kwa moyo wote huku akimtumikia Ibilisi kwa miaka kumi na tano. Yapo mengi sana sana kaitika maisha yake lakini tukiwa tunasubiri kupata "The Documentary about Power Mangwana in Ohayoda Blog" tunajifunza nini?

Kumbe kubadilika na kuwa wanadamu wa kutegemewa inawezekana kwa msaada wa Mungu. Uwe ni jambazi sugu, malaya wa kutupa, mwongo, msengenyaji, mlevi, fisadi, nk bado Yesu anaweza kukupokea ulivyo na ukawa mpya tena na tena. Injili inapigwa, Watu wanaokoka na wagonjwa wanapona, miujiza kila kona chini ya mtumishi wa Mungu Power Mangwana. Mimi na wewe tusihukumu wala kubeza ila tujivunie hatua za watu kama hawa.

Watu wakisikiliza Neno la Mungu kwa makini lilitoka Mdo 3
Mkutano unaendelea hapa Haydom hadi Jumapili septemba 9......

Gari la mfadhili wake kanda ya kaskazini..

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda