Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, September 18, 2012

Papaa On Tuesday......Lini Nitayaangalia Mambo Yangu Mwenyewe???

Sitaacha Kumshukuru Mungu Kwa kila siku inayoitwa leo kwa ajili ya uweza wake na fadhili zake za kila siku kwenye Maisha Yangu. Nikusalimu wewe Msomaji wa Papaa On Tuesday kwa kutumia dakika hizi 10-15 kuweza kusoma article hii. Niwashukuru wale ambao wamekuwa na moyo wa kuwatumia na kuwa printia wengine ujumbe huu ili uweze kuwafikia. Niwashukuru sana wale walioni sms na kunipigia simu na kuni email kuhusu Papaa On Tuesday na Kunishauri. Mwisho nikushukuru wewe uliyeamua seriously kutendea kazi yale uliyoyasoma na kuona yatakusaidia. Kama hayatakusaidia leo yatakusaidia kesho. Tuzidi kuombeana sana maana kazi ya kupanda kwenye hii madhabahu kila Jumanne kuongea na nafsi za watu sio ina changamoto lakini pia ina vita vyake.

Wakati siku ya Jana Madaktari waliokuwa wanagoma nchini Tanzania kuomba Msamaha na habari kuonesha kuwa wameongezwa Mshahara kimya kimya basi linalofuata nahisi sasa ni kushtakiwa kwao na ndugu ambao waliathirika na mgomo ule kwa namna moja ama nyingine. Kuomba msamaha ni dalili ya kuwa ulikosea na Kama ulikosea basi kuna madhara ambayo uliyasababisha kwa kukusudia ama kuto kukusudia. Twende Kazi sio hasa ninachotaka kuongea leo nakamilisha taarifa kadha wa kadha kabla sijaja na Papaa On Tuesday ambayo nimeanza kuandika inayohusiana na mambo yanayoendelea Tanzania. Alikuwepo yule Waziri aliyesema aliwekewa Sumu mpaka mwili ukafanya nini sijui akongeaaaaa ghafla kanyamaza, Akaja yule baba wa TUCTA sijui akaongeaaaaaa ghafla Kanyamaza, Akaja Yule waliyempeleka Mabwe Pande madaktari wakaongeaaaa weee jana wameomba msamaha, Kesi Ya yule anayesadikika kama sio hisiwa anahusika na mauaji ya yule Mcheza Filamu nambari One bongo, imeeenda jana imerudishwa Mahakama ya Kisutu mwisho wa siku. Hata Hili Nalo Litapita, dont plan to Miss Kusoma hiyo ya Article nimechukua tu mifano ya Kisiasa lakini individually kuna issue zilikuja Zikatikisa maisha yetuuuu, Zikaja Zikapita, Kuna Watu walitesekaaaaa, Mateso yakaja yakapita, Kuna watu walipopata Ujauzito walitelekezwa lakini hiyo hali ikaja ikapita, Hata unalopitia sasa hivi na lenyewe Litapita, alikuja Ukweli Na Uwazi Facebook akaharibuuuuu amekuja nae amepita...Nothing Will Stay Forever.

Leo Nataka tuitazame Papaa On Tuesday kutoka katika Kitabu Cha Biblia katika Kitabu Cha Mwanzo Sura Ya 30:27 mpaka Wa 30. Biblia Inasema hivi....."Ikawa Raheli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, Nipe ruhusa niende kwetu, na kwenye nchi yangu.  Nipe wake zangu na watoto wangu, niliokutumikia, niende zangu, maana umejua utumishi wangu niliokutumikia. Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba Bwana amenibariki kwa ajili yako. 28 Akasema, Sema mshahara wako utakao, nami nitatoa.29 Akamwambia, Umejua jinsi nilivyokutumikia, na jinsi wanyama wako walivyokuwa kwangu.30 Maana mali yako ilikuwa haba kabla sijaja, nayo imezidi kuwa nyingi, Bwana akakubariki kila nilikokwenda. Basi sasa, lini nitayaangalia mambo ya nyumba yangu mwenyewe?".

Ukisoma hiyo Mistari kuna Papaa On Tuesday Kama 3 ndani yake ambayo nitayaongea siku nyingine. Unaweza kujiuliza kwanini baada ya Kuzaliwa Yusufu ndipo Mgogoro wa Mwajiri na Mwajiriwa ukaanza. Wengi Mnajua Story ya Yusufu ambaye baadae alikuja kuwa Waziri Mkuu Misri sasa ajabu baada ya yeye kuzaliwa Mwajiriwa ambaye ni Yakobo akaanzisha Mgogoro na Mwajiri. Ukisoma Story pia utaona Mwajiriwa anaamua ku resign kutoka kwenye ajira ili awe Mjasiriamali ndipo Mwajiri ambaye ni Labani anakataa kisha anamwambia "Jipangie Mshahara Wowote nitakulipa" umewahi jiuliza kwanini Mwajiri aliomba Kumuongezea Mshahara ila Yakobo akaomba apewe "shares"??Nitakuja kuongea siku nyingine tofauti ya ku own Mshahara na Ku-own shares. Lakini leo nataka tuutazame kwa Makini Mstari wa Mwisho kabisa Yakobo akasema "Lini Nitayatazama Mambo Ya Nyumba Yangu Mwenyewe???.
Inawezekana kuna maswali kadha kadha tumejiuliza kama Yakobo tuliyemsoma na kukosa majibu kuwa ni lini nitaachana na habari ya kuajiriwa na Ajira Yangu Mwenyewe??Ni Lini Nitaachana na Nyumba za Kupanga na Kuwa na Nyumba yangu Mwenyewe??Ni Lini nitaachana na Uvivu nilionao??Ni Nili Nitaachana na Tabia mbaya niliyonayo??Ni Lini nitabadirika na tabia ya kutegemea Mshahara??Ni Nili Nitakuwa na Familia yangu Mwenyewe??Ni Lini na Mimi nitakuwa mtu mwenye kusimamia Maisha yangu mwenyewe??Ni Nilini nitaachana na Tabia ya kuwa mmbeya, ni Nili nitaachana na hiki kinachonifanya mpaka sasa kuwa hivi ni livyo, Ni mpaka lini nitaendelea Kuwa na Maisha niliyonayo??umewahi Kujiuliza Mpaka Lini utaendelea kuwa hivyo ulivyo???

Kubadilika na Kuamua kuishi katika mabadiliko sio jambo jepesi. Mara ngapi tumekuwa tukisema Kuanzia leo mimi basiiiiiii nimebadilika baada ya siku umekuwa yule yule. Mara ngapi umewekwa kikao na boss wako ama familia yako ama mumeo ama mkeo ukajisikia vibaya sana kisha ukasema kuanzia leo nimebadilika baada ya muda umerudia yale yale. Mara ngapi umejilaumu kwa kutumia vibaya fedha zako unazozipata kwa kununua vitu vizivyo na msingi kwenye maisha lakini pamoja na kujilaumu na kujiapia kubadilika umeendelea kuwa mtu yule yule. Mara ngapi umefanya maamuzi ya kupunguza unene kwa kufanya diet na mazoezi??unafanya wiki 2 mwisho wa siku umerudi maisha yale yale. Mara ngapi umekaa kusuruhisha matatizo ya mahusiano yako na mumeo na mkakubaliana kubadilika mwisho wa siku yale yale. Hivi umewahi jiuliza Mpaka lini hali hiyo utaendelea nayo??

Story tuliyosoma ni mtu anaitwa Yakobo alikuwa ameajiriwa, Mwajiri wake alikuwa anaongeza faida kupitia Yeye, Kama ni Profit ilikuwa inakuwa kuliko maelezo. Huyu Mwajiri alikuwa anafaidika kupitia Yakobo. alikuwa anasifika Kupitia jasho la mtu mwingine. Wakati Yakobo anazidi kupoteza Muda na Kuzeeka. Huyu Mwajiri amezidi kustawi. Ndipo Yakobo akajiuliza swali Mpaka Lini Nitaendelea Kunufaisha Wengine Mimi nikiendelea na maisha haya??Mpaka lini Nitaendelea Kuwa Mwajiriwa wa huyu Jamaa??Waajiri wanatupenda pale tunapowaletea faida kwenye kampuni. Kama wewe umeajiriwa kama Mimi jiulize swali. Lini utaanza kufanya mambo yako ukisha staafu??Ukishafukuzwa??. Kama wewe ni Mwanandoa jiulize Lini Utaanza kuyaangalia mambo yako mwenyewe??Ukiwa Ni Mwanafunzi jiulize swali lini utaanza kuyaangalia mambo yako mwenyewe??Kama Unakaa kwa dada yako, Shemeji Yako, Ndugu yako jiulize swali lini utaanza kuyaangalia mambo yako mwenyewe???Utazeekea kwa watu??.

Watanzania wengi sana tumedhani kuna mtu anawajibika na maisha yetu. Waajiriwa wanadhani Mwajiri anawajibika na Maisha yao, Mke au Mume anadhani Mwenzake anawajibika na Maisha yake, Mtoto anadhani Wazazi Wanawajibika na maisha yao, ndugu wanadhani ndugu wengine wanawajibika na maisha yao ndio maana lawama na migogoro kila siku. Utasikia Kakaangu wala hanisaidii kutafuta kazi, Utasikia Mume wangu wala haangaiki na issue zangu, utasikia Mwaajiri hajishughulishi na maisha yangu, sijui shemeji wala hanitafutii biashara, utasikia Wazazi hawajanipa Mtaji, Kila mtu anajitune kuwa Kuna Mtu Mwingine anawajibika kwa Well Being yake. Kila mtu anawajibika kwa faida na maisha yake mwenyewe. Kwenye Kiswahili tunasema Mgaa Gaa na Upwa, Hali Wali Mkavu na Kwenye Nia Pana njia. Ukweli ni kwamba tumewalaumu watu wengine tukidhani wanahusika na maisha yetu. Ukiwa na Mawazo haya kila siku utaendelea kuwa mtumwa wa maisha yako mwenyewe. Kuna Watu kazi yao kuagizia wengine majukumu. Utasikia Nitafutie kazi, nitafutie Biashara, Nitafutie Nyumba, Nitafutie sijui nini na nini. Mwisho wako utakuja kuwa mbaya kupita maelezo. Lini Utaanza kuyaangalia Mambo yako Mwenyewe???
Ukiona kila siku unarudie hali yako ya kwanza ujue bado haujachoka hali uliyonayo. Ukichoshwa na hali uliyonayo siku zote utakuwa na maswali "watu watanionaje" Itakuwa vipi kama haikukaa pouwa, Itakuwa vipi kama nitakaa miezi mitatu bila ajira, itakuwa vipi kama haitakuwa sawa ukifika Kikomo cha kuchoshwa na hali uliyonayo utasema Liwalo Na Liwe. Ukifukuzwa nyumba unayokaa hautalala nje Milele kuna akili utaipata, Ukikaa na Njaa Siku 3 utajua namna ya kutafuta pesa, Ukikaa Bila Ajira ndipo Utakuwa na akili ya  Kujiajiri yeyote naye ona aibu kujiletea maendeleo yake mwenyewe ujue ametosheka na afadhari. Umewahi waona wale wanaookoka taka taka nyumba hadi nyumba umewahi muona mtu ameajiriwa lakini kutwa kucha kutembeza vinguo nguo, umewahi muona mtu na profession yake anashika mic kufanya kazi ya u-mc, umewahi ona mtu na cheo chake anafanya kazi kufuga kuku???Unless umechoshwa na hali uliyonayo ndipo mshipa wa aibu utakatika. Usiridhike na afadhari uliyonayo wakati una uwezo wa kufanya zaidi ya hicho unachofanya. Mshahara unadanganya, Mshahara una utamu wake ukiupata ila mshahara haukupi uhuru wa kutimiza ndoto zako zaidi ya kutimiza ndoto ya mwajiri. Mtu yeyote mwenye mshahara pasipo kuwa na shares (ownership) mahali pengine huendelea kuwa na mawazo ya kujionea huruma.
Nimalize kwa Kusema Kila mmoja wetu anaweza kwenda extra mile katika yale anayoyafanya. Ijumaa hii nikiwa na Swahiba Prosper Mwakitalima Tutaendelea na Live Teachings Pale Maeneo Ya Kurasini. Kuanzia saa 3 Usiku Mpaka Saa 9 Usiku. Hii itakuwa ni Wiki Ya 3. Wiki iliyopita Swahiba alikuwa anaongea Namna gani Talent Uliyonayo Inavyoweza Kukufikisha Mbali na Mimi Niliongea "How You Can Translate Your Dreams To Reality" ambapo tulitazama Kwanini kwa Bongo ni Changamoto kutimiza ndoto Zetu, Pia nikaeleza Unawezaje kugundua Talent or Gift ambayo Mungu amekupa ambapo hata ukipewa shilingi ngapi hautasikia raha kuliko ukafanya kile kitu ambacho Mungu amekupa hata kama umefanya bure. Wiki hii Usiku tutaendelea Kuongea Mpaka Kieleweke kwenye "Changing Mind Set Za Watanzania".


Jiulize swali hili nani yuko accountable na maisha yako??Ni Lini utabadilika kutokana na hali uliyo nayo??Think Differently and Make a difference.

Papaa Ze Blogger.
0713 494110.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda