Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, September 11, 2012

Papaa On Tuesday.....Kujionea Huruma Kufanya Maamuzi Magumu Kuna Zuia MafanikioNa Samuel Sasali
www.samsasali.bogspot.com
Ikiwa leo ndugu zetu wa America wanakumbuka mauaji September 11 siku ya leo Tanzania Waandishi wa Habari Wanafanya Maandamano ya Kimya Kimya Kulaani Mauaji Ya Mwandishi David Mwangosi yaliyotokea Wiki Moja Iliyopita Kwa Ujumla Wake September 11 ni Siku Ya Majonzi kwenye nchi hizi mbili yamkini na nchi zingine pia. Mungu awe Mfariji wa wenye huzuni kipindi hiki.

Mara Kadhaa nimemsikia aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa akisema kuwa nchi hii imefika hapa sababu Serikali imeshindwa Kufanya maamuzi Magumu. Mbunge wa Jimbo langu Mhe. Mnyika aliwahi sema Serikali Yetu ni dhaifu ndio maana inashindwa kufanya maamuzi magumu. Hatujapiga hatua sababu tunashindwa kuamua.

Kwa waliosoma issue za Management kuna Topic Ya Decision Making ambayo wanasoma watu lakini subutu yake nani anakumbuka majibu ya Mtihani kwenye issue za Kuamua. Kila siku unapoamka unatakiwa uamue, unegotiate between the two or more. Mwalimu wangu Kibasa aliwahi sema kila siku unapoamka hata kabla ya Kuamka unaanza ku negotiate uamke saa 12 ama 12 na nusu, Ukiamka unaanza ku negotiate tena Uoge maji ya moto ama Ya baridi, Uanze kuoga ma kunyosha, upande daladala ama bajaj. Ukifika Ofisini unaanza Uanze kusoma Papaa On Tuesday ama Kazi, Ufungue email ya Ofisi ama Facebook. Hakuna dakika itapita hujaamua kitu cha Kufanya ndipo utagundua upo hivyo ulivyo kutokana na Maamuzi.
Kwenye maisha ili tuweze kupiga hatua kuna wakati lazima ifike mahali tusijionee huruma katika baadhi ya mambo. Assume uko mahali pengine kwa mwajiri wako, au kwenye mahusiano lakini kikweliii moyo wako haupo hapo unakuta mtu analalamika tu Mshahara mdogo, unanyanyaswa sijui kutoka hatoki ndani aingii amesimama tu mlangoni kuzibia wengine, nadhani ipo haja ya kupiga hatua pasipo kujionea huruma. Hapa inaitwa kupiga Moyo konde.
Huruma ninayoongelea hapa sio kujiumiza kwa maana ya mwili hapana ni ile nafsi yako ku-scicrifice wakati mwngine hata utu wako, assume unadumu katika dhambi, mtumishi wa Mungu akaita watu wa dizaini ya dhambi uliyonayo watoke mbele wewe ukapotezea, unajionea huruma status yako itashuka, au unaona watu watakuelewaje, cha kujiuliza kwanini uendelee kuteseka huku ukilinda ujinga?hapo hakuna sababu ya kukaa kimya kama vipi jilipue kieleweke.

Unajikuta una hali hiyo hiyo inajirudia mpaka unakasirika, Kila mwezi wewe ni mtu wa kukopa, mshahara wako unaishia kwenye madeni, ukitazama hakuna cha maana unachofanya na hela zako. Ukipata tu Mshahara unakuwa na tabia za ajabu mpaka wewe mwenyewe unajishangaa. Hela zikiisha unajisikia vibaya huna furaha hali uliyonayo je umewahi fanya uamuzi mgumu kuhusu hali yako??.

Huwa nashangaa sana wale ambao wako majumbani wanatazama TV halafu wana waagizia watu wa Ofisini kuwa "Nitafutie Kazi". Ukweli ni Kwamba tulio Maofisini hatutafutii watu kazi. Ila tukisikia kuna nafasi tutakutaarifu lazima ujifunze kuacha kutazama TV na kusaka ajira kwa ajili ya kujinusuru na Maisha yako mwenyewe. No one is responsible with your life except wewe mwenyewe. Niliwahi andika kwneye Papaa On Tuesday...Kifaranga Kilichovunjiwa yai kutoka hubaki kuwa goi goi. Jifunze kuvunja yai wewe mwenyewe. Maisha sio kutafutiana Maisha ni Kutafuta na Kushirikiana.

Kuna watu wengine wako kama walivyo sababu wanashindwa nini cha kuamua kufanya. Mwingine anateseka na kupenda na anashindwa kusema kwanini usifunguke??kwanini usiseme ulilonalo moyoni. Kuna watu wanateseka na hali walizonazo wengine mpaka wamekuwa watumwa kwa watu wengine sababu mbali mbali. Kuna Jamaa mmoja alikuwa sio mwaminifu kwa Mkewe, akawa ana cheat, yule jamaa alipotaka kuachana na yule mdada akageuka kuwa mtumwa maana kila siku yule mdada anamwambia ukiniacha tu naweka mambo yote hadharani namwambia Mkeo kila kitu. Huyu Jamaa sababu ya kulinda heshima katika Jamii na Kwa familia yake akafanyika kuwa mtumwa kwa huyu kahaba. Huyu Kahaba akitaka fedha anamwambia Jamaa ninashida na laki 5 jamaa akisema sina, kahaba anamtishia Nitamwambia Mkeo, jamaa kulinda heshima akawa anatafuta anampa, hali hiyo ilienda mwaka mzima huyu Kahaba akawa anamgeuza huyu Baba wa watu mtaji. Siku Moja huyu Baba akiwa amezingatia moyoni mwake akawaza sana hii hali itaendelea mpaka lini??Mpaka lini nitakuwa Mtumwa wa huyu Kahaba??huyu Baba akaamua Liwalo Na Liwe akaazimia moyoni Mwake kwenda Kumueleza Mkewe, kama kusamehewa ama ugomvi bora amalizane na Mkewe yaishe. Akafunga safari akaenda kujieleza MWAMWI (mwanzo Mwisho) kwa mkewe. Wakaongea sana mwisho wa siku Wakaamua kusameheana waendelee na maisha yao. Siku tatu baadae yule kahaba akatuma sms kuwa anataka Milioni 5 aongezee anunue gari. Yule Baba akamwambia HATOI TENA HELA, yule mdada akamwambia nitamweleza Mkeo Kila Kitu Tulichofanya, yule baba akasema "tena niko na Mke wangu hapa nikupe simu uongee nae"??yule kahaba akakata simu akajiuliza "amepata wapi confidence". Yule Kahaba akajitutumua akapiga tena simu kwa Jamaa, akapokea Mke wake akamwambia yule kahaba "Mume wangu amenieleza mambo yote mliyoyafanya sababu hiyo usipate tena tabu ya kuniambia" akakata simu. Tangu siku hiyo huyu baba akawa huru. Akajilaani sana kwanini asingefanya huo uamuzi zamani angekuwa na furaha kuliko kuwa mtumwa. Swali alilojiuliza ndilo ambalo nataka kukukuuliza "Utaendelea kuwa Mtumwa wa hali uliyonayo Mpaka Lini"??  
Watu wengi waliofanikiwa katika maisha ni wale walioamua ku take risk kwa ajili ya kitu, hata kuoa wengine walishauriwa wasioe ama kuolewa na Fulani sababu ya “ukimeo” wa mtu lakini watu wakaamua kujiripua kwa ajili ya “focus” ya maisha. Leo hii wale tuliowahi wakataa ama wadharau wakati wakifanya maamuzi magumu tumebaki kuwapigia makofi kimoyo moyo kuwa wanaendelea vizuri. Ni lini utaendelea kusikiliza shuhuda za wenzako?Siku Moja nikiwa nimeamka usiku kusoma soma neno moja likanijia "To Love is to Choose, and to Marry is to Decide" Kupenda ni kuchagua, Kuoa ni Kuamua.Hakuna kitu kibaya kwenye Mafanikio Kama Kuamua Kuto Kuamua.

Kama Mtu anakusumbua na hupendi usumbufu wake kwanini usimwambie??kunyamaza haita saidia zaidi kumuhamasisha wengine hawaelewi kwa kunyamaziwa ila kwa kuambiwa. Unless You Speak It out ndo itakuwa nafuu yako.


Usijiripue sababu wengine wamejiripua jilipue sababu umefanya mchakato kwenye ubongo ila unaogopa ku take action. Amua leo kufanya maamuzi magumu. Poul anasema katika Biblia kujizoeza katika mema, hata kufanya maamuzi magumu inahitaji kujizoeza ili kuweza kupiga hatua. KUlalamikia Mwajiri, Kulalamikia Mshahara na huku bado upo hapo hapo ni kujidanganya.

Jiulize baada ya kuacha kufanya maamuzi magumu kwa ajili ya maisha yako, umepiga hatua ama upo pale pale?diriki leo kufanya maamuzi magumu.


Think Differently and Make a Difference.

Papaa Ze Blogger.
0713 494110. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda