Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, September 26, 2012

Papaa On Tuesday......Kama Wengine Wanaweza Kwanini Mimi Nisiweze?

Wapenzi wasomaji wa Ohayoda tunawaomba radhi kwa kuchelewa kuwaletea Papaa On Tuesday jana kama ilivyo ada kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Lakini hakijaharibika kitu, Samuel Sasali a.k.a Papaa anasema Kama Wengine Wanaweza Kwanini Mimi Nisiweze? Ungana naye ujue kwa undani kwa nini anasema hayo maneno


Nimefarijika sana Marafiki zangu wanaonipigia simu, wanao sms, wanaoniandikia kwenye facebook wanaoniandikia email kunitia moyo na wengine kunisahihisha na wengine Kuniombea. Sina Cha Kuwalipa Mungu wangu na awabariki sana kwa kunitia kwenu Moyo katika Kuandika Papaa On Tuesday. Sio Kitu rahisi kila Jumanne kuwa na Jambo la Kuongea ni Kama Mchungaji ama Padri ama Imam ambaye kila siku ya Ibada lazima awe na neno. Tuko pamoja sana.

Leo nataka nifanye muendelezo wa Papaa On Tuesday niliyoiandika tarehe 12 October, 2010. Hii ni wiki ya tatu mimi pamoja na Swahiba nambari one Prosper Mwakitalima tunafundisha vijana katika "Kujitambua" katika Kanisa la Full Victory Maeneo ya Kurasini ambapo Ijumaa hii tutakuwa tunahitimisha Semina Ya mwezi Mzima. Papaa On Tuesday hii ni kasehemu ya Yale ambayo nimefundushisa Ijumaa Mbili Katikati Ya Vijana.
Kuna watu wengi sana wanaogopa kujifunza kwa walioshindwa. Nimewahi sikia hata muimbaji mmoja wa nyimbo za Injili anaeleza kuwa "Usijifunze Kwa Walioshindwa". Maana Walioshindwa hawana Msaada. Kwa Mtazamo wake na watu wengine wenye kuwaza kama yeye nakubaliana nae kabisa. Lakini lazima tujiulize swali ni kweli hatuna cha kujufunza kwa walioshindwa??Hivi katika kushindwa kwako katika maisha hakuna mtu anayeweza kujifunza??. Kwenye semina niliwaambia ndani ya Miaka Kumi Ijayo kati wengi wetu tutakapokuwa wazee tayari tutajilaumu sana kwa mambo ambayo hatujayafanya mpaka wakati huo kuliko yale ambayo tutakuwa tumefanya. Wiki hii Jumapili nikisoma gazeti nilisoma habari inayoeleza mwanafunzi wa Darasa la Saba aliyejifungua Kwenye mitihani ya juzi ya darasa la Saba. Katika maelezo yake anaeleza kuwa anasikitika sana sana kwa ndoto yake ya Udaktari kupotea. Alijiingiza kwenye mapenzi sababu ya ugumu wa maisha na mbaya zaidi akajiingiza kwenye ngono isiyo salama na kupata mtoto ghafla ameshindwa kuhitimu darasa la saba na amekuhitimu kuwa mzazi. Kwake anaona maisha yameisha ndoto imepeperuka. Wengi wetu mpaka sasa tunajilaumu kuwa nuna mambo kadha wa kadha pengine tungeyasikiliza siku za nyuma tusingekuwa hapa tulipo. Wengu tumebakiwa Kama isingekuwa..............ningekuwa mbali sana sasa hivi, Kama Sio.............ningekuwa ni mtu mwingine kabisa, Kukosa kukutana na .................ningekuwa sijui nani, Kukosa Kusomea................ningekuwa mbali. Lipo Somo la Kujifunza kwa walioshindwa katika maisha.
Tangu nikiwa mdogo nilifundishwa kuwa kukosea sio sehemu ya kujifunza, nilitumia muda mwingi kujikita katika kupatia kuliko kukosea. Na kama ilitokea nimekosea kitu nilikuwa najisikia vibaya sana na wakati mwingine nashindwa hata kula pengine kulia kabisa. Tangu nikiwa mdogo nikajifunza upande mmoja wa jambo kuwa katika kila jambo ni sharti ufanye vema, tafuta namna ya kufanya vema, Nikajikuta najifunza sana sana kuto kuanguka kuliko nikianguka nitasimamaje. Shuleni kama nimekosea hesabu ama Kiingereza ama somo lolote tulikuwa tunachapwa hali hii inakifanya niamini nikitaka kuwa na raha na furaha kwenye maisha ni lazima uwe sambamba na mawazo ya Yule anayekuelekeza hata Mwalimu wangu hakuwa anatafuta logic ya kukosea kwangu. Au hujui katika kukosea tunapata kujifunza na kupata mambo mengine mapya katika makosa?nikaanza kukariri kila ninachoambiwa ili nisikosee..akili yangu haikuweza kujifunza kujitegemea, ilikuwa imeumbiwa kutokujiamini kwa maana ya kwamba nikifanya mwenyewe nitakosea. Ndio maana leo hata vyuo vikuu watu bado wanagezea watu bado wanakula chabo sababu gani??hakuna mtu anayeamini kuna uzuri wa kukosea ingawa tunakosea.

Kwenye maisha kila mtu hataki kukosea ndo maana kuna wataalam wa kushauri watu wasifanye makosa. Kuna Makampuni na Watu ambao kwa kubaini kuwa akili za wengi wetu zimelala wameanzisha Program mbali mbali za kuwajenga watu kiakili. Watu wanapenda kuambiwa namna gani unaweza pata “Mume Mwema”, namna gani unaweza kupata “Faida, Pasipo Hasara”, watu wanapenda kuambiwa Tuma neno Mkoko upate gari. Wengi wetu ni kama Vibao Vya Kanisa kazi ni kuelekeza watu kufanya mema wakati mema yenyewe yanawashinda. Juzi kati nilisikia mwezeshaji wa Semina Ya Ukimwi baada ya Somo la Ukimwi akaanza mtongoza Mwanasemina akisema "anaogopa kulala peke yake". Sasa huyu anayeongea mbele kufunza watu kumbe nae ni mgonjwa. Kweli Mpera hauwezi kuzaa Nyanya Chungu.  kuna watu wanatumia advantage ya ujinga wetu kunufaika bila ya sisi kujua.
Kwenye maisha ni lazima tunuie kufanya tena kufanya kwa ajili yako mwenyewe no one responsible with your success. Ndio maana wiki iliyopita niliandika Lini utayaangalia mambo yako mwenyewe??. Kila mtu Mungu amempa uwezo wa kufanya kitu kwenye maisha. Maisha ni zaidi ya kuwa na gari, maisha ni zaidi ya kuwa na familia, swali ninalojiuliza Familia yako imefaidika nini na wewe kuwa miongoni mwa wanafamilia, Kanisa lako limefaidika na nini wewe kuwa mwanafamilia, Taifa letu la Tanzania linafaidika na nini wewe kuwa Mtanzania. Lazima kwenye Maisha kuwe kuna Purpose yaani Kusudi. Kila tunachokuwa nacho kwa kukimiliki ama vyovyote lazima vituelekeze kwenye kusudi. Je gari ulilonalo linakupeleka katika kusudi?mke ama mume au mchumba uliye naye anakupeleka kwenye destiny?mtu yeyote au kitu chochote kisikutaabishe kama hakikupeleki kwenye future yako. It doesn’t matter how much will cost you lazima uwe na strategy. Kwanini upo hapo ulipo na upo mpaka lini?je umefika ama unapita?kama unapita unaenda wapi?je hiyo ni njia ama uko chaka?kama uko chaka mbona unalipalilia chaka?

Huu si wakati wa kuongea ni wakati wa kufanya kwa maisha yetu, God has given us talents and Gifts, wengine kuongea, wengine kuimba,wengine kukimbia, wengine kuandika, wengine kuwaza, wengine kuona yasiyoonekana, wengine kuomba, wengine kuchekesha wengine kufundisha, wengine kushauri. Kuna Tofauti Kubwa sana kufanya Kile Ulichosomea ada na kulipiwa na familia yako na kufanya kile ulichoumbiwa kufanya duniani. Kwanini usijipe malengo wewe mwenyewe ukayatekeleza?Una Njozi??go for that. Mimi na Swahiba Prosper tumewahi mara kadhaa kufuatwa na watu wa Network Marketing, Wakiamini Kuwa Kwa kuwa tuna Network ya watu itakuwa pouwa sana kuuza products. Mwanzoni sana tulijaribu hizi mambo tukahudhuria semina kadhaa tukatoa hela kuuza Products. Mungu ni shahidi iliishia tu kugawa hizo products. Kila tukijaribu watu kuwashawishi watumie Products mioyo yetu inakosa amani, mioyo yetu inakosa kuthubutu kuuza. Ndipo tukakaa tukaulizana Mbona tunatumia nguvu kubwa kuuza hizi kitu???mwisho wa siku tuligundua hatukuumbiwa kufanya hayo mambo. Hata kama wengine wanatengeneza hela kila kukicha, hata kama wengine wanapata faida kupitia hiyo biashara. Kama Moyo wako haupo hapo utafanya utapata hela na utakosa raha. Ukifanya kile ulichoumbiwa kwenye eneo lako hata kama hautapata fedha lakini utakuwa na utosherevu wa ndani kabisa ndani ya maisha yako. Kuna watu wana struggle sana katika kazi wanazofanya na hawana raha sababu tu walisomea kazi hizo mjomba alilipa ada. Hivi umewahi jiuliza kwanini wabongo wengi “Hawajatoka” ingawa wanafanya Business Marketing?umeahi jiuliza unapata raha gani unapokuwa unafanya cha kwako?kwanini usifanye?unasubiri nani akuhesabie moja, mbili, tatu ili uanze kukimbia?anza kufanya kwenye maisha mbona wengine wanafanya unachodhani hakina faida?aaaaaah kumbe unaogopa kukosea?Kukosea ni Mwalimu Mzuri kuliko kupatia, we should learn to take risks. Mwaka huu utakapokuwa unaisha jiulize umefanya impact gani kwenye Jamii inayokuzunguka. Ukianza kufanya maboresho yatakukuta juu kwa juu.Kama wengine wanaweza Kwanini wewe usiweze. Utalala njaa siku chache, utapata tabu siku chache lakini if ur destiny haiko kwenye Biashara ama Ajira basi iko kwenye Kipaji.
Usidharau wazo lako, usidharau kile ambacho moyo wako unasukumwa kufanya hata kama hakina faida kwa sasa lakini kama Biblia inavyosema katika Muhubiri “Tupa Mkate Wako Kwenye Uso wa Maji Nawe utaukuta baada ya Siku Nyingi” its very fun inawezekanaje Mkate ukawa kwenye maji then ukaukuta baada ya siku nyingi??Is not linking but it links. Sometimes in life ni kama tunapoteza lakini ndo njia nzuri ya kujifunza, Mwalimu mzuri kwangu amekuwa kufanya makosa kwenye maisha. Nilipopata wazo la kuanzisha Blog yangu sikuwa nimeona impact ya moja kwa moja by that time. Kwa kadri siku zinavyozidi kwenda naona kile ambacho kilikusudiwa kupitia blog. Nilipoanza kuandika Papaa On Tuesday sikujua kama itakuwa na wasomaji wanaosaidika namba hii. Blog haikuanza hivi wale wanaoijua wengine walibeza lakini leo hii Blog imeajiri mtu mwingine ukiacha mimi mwenyewe. Kukosea ni njia ya kujifunza. Don’t wait mpaka uweze kupatia Kila Kituuuuuuuu anza pale ulipo. My friend Mbunge Mtarajiwa Martin Kaswahili kaandika “Start With Nothing Finish With Everything”. Anza na kile ulichokuwa nacho huwezi jua. Mungu ataku connect na watu wenye mawazo bora zaidi unapokuwa umeanza kufanya. I feel very comfortable mtu anapotaka nimwambie namna gani my Blog inaweza kuwa na Impact kwenye Jamii kuliko kuuza Product ya mtu mwingine. Ninajisikia raha sana kumwambia Mtu Mimi na Prosper na wadau wengine tuliwahi kuwa na Magazine ya Gospel Today Ikafa, Kuna vitu vingi sana niliwahi kuanzisha kwenye maisha vikafa lakini sijawahi kukata tamaa kwenye maisha. Life is how you make it. Aonavyo mtu nafsini mwake ndiyo alivyo.
Watanzania tunapenda kufanya kwa ku-organize. Utasikia tu yaani angekuwepo mtu wa kutu-organize tungefanya 1,2 and 3. Anza kufanya mwenyewe mbona wengine wanaweza?Mwalimu wangu Kibasa alimaarufu Baba Xtina kwenye facebook aliwa sema Siku moja nenda shule ya Msingi Uliyosoma nunua hata vitabu vya shilingi laki moja visaidie ile shule…Shule zile ni kati ya zilizotusababisha tuwe hivi tulivyo. Ndani yangu nina dhamiri ya kufanya kwa ajili ya shule yangu japo kakitu kadogo lakini kama ishara ya kusaidia elimu Tanzania.  Don’t wait to be organized…Organize Yourself …au ndo ulivyoumbwa? Kama wengine wote wanaweza kwanini wewe usiweze?

Seat down weka nafsi yako pembeni, weka roho yako pembeni weka na mwili wako pembeni kaeni Kikao. Be yourself, be honesty be open to yourself. Jiulize maswali. Imenisaidia sana kwenye maisha yangu. Najiwekaga vikao mara kadhaa. Najiuliza watu wanasema Papaa hutaki kuoa sababu unachagua sana, hutaki kuoa sababu ……………., mwingine nae ………………………, then najiweka Kikao. Hivi kwanini Sijaoa mpaka sasa. Am honesty to myself naandika. Then najiuliza mbona rafiki yangu kaoa sababu hiyo hiyo inaweza isiwe kweli, naandika nyingine then nagundua Fulani kaoa sababu hiyo hiyo…naandika nyingine nagundua    Mbona huyu nae ameoa??then nakuja nyingine nyingine nagundua fulani anaoa kesho kutwa kwa sababu hiyo hiyo?at last nagundua baadhi ya vitu vingine then naanza kutendea kazi. Kama hawa wote wanafanya kwanini mimi nisiweze. Kama Tshirts ndizo zinamuweka Prosper Mjini kwanini wewe usiweze?Kama Taa za Mionzi ya Jua  ndo zinamuweka Andrew Mnzava mjini kwanini wewe usiweze?Kama Kuchekesha ndo kuna Muweka Masanja mjini Kwanini wewe Usiweze. Hujaamua kuthubutu kufanya.

Ukiwa umeajiriwai jiulize sentensi hii. Siku Management ya hapo unapofanya kazi ikiamua tu uachishwe kazi yaani kwa wema tu uache. Je utafanyaje?utalia?utachukualia kama ipo ipo?utapotezea?Je kama Mume ama Mke uliyenaye atakufa ghafla utarudi kwenu uanze moja, utaoa ama Olewa tena au??Jiulize Kile ambacho unakitegemea kukusitiri na tabasamu hapo ulipo kisipokuwepo utafanya nini?/Usisibiri Ustaafu ndo uanze kufuga kuku, Usisibiri hela ya NSSF ndo ufanye mtaji. Linalowezekana leo lisingoje Kesho. Kama wengine wanaweza kwanini wewe Usiweze??

Think Differently and Make a Difference.

Papaa
0713 494110
samuel_sasali@yahoo.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda