Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, September 2, 2012

Maisha Yangu Yamekosa Tumaini, Lakini bado nina Matumaini na ninajua unaweza KUNISHAURI, Tafadhali, nisaidie japo kwa Neno moja tu......


Na Nelson Faustin Nd.
Wapenzi wasomaji wa Blog hii ya OHAYODA, tuliamua kuwa na makala pekee ya kuwashauri watu wenye matatizo mbalimballi, leo ni siku nyingine ambayo tutpata kusikia kisa kingine na wewe kama mdau wa blog hii utapata nafasi ya kumshauri ndugu yetu huyu japo kwa neno moja ili aweze kusonga mbele. Majina na taarifa za wahusika zitatunzwa kwa sababu maalumu".

"Niliwahi kufahamu kuwa kuna kila sababu ya kumjua Mungu na kufuata mafundisho ambayo yataniweka karibu sana na Mungu. Lakini baadaye nikafundishwa kuwa baba na mama ni miungu wa dunia na hivyo ikanilazimu sana kuwaheshimu na vyote ambavyo walikuwa wakinifundisha na kunieleza kutokana na uzito wa kuwa wao wana nafasi kubwa sana katika maisha yangu.

Maisha yaliendelea vizuri sana ila mwaka 2006 baba alitangulia mbele ya haki,..........iliniumiza sana ila sikuwa na budi ya kumwachia Mungu, na kuendelea kuamini kuwa Mungu alikuwa na sababu kwa nini baba yangu aniache nikiwa na umri wa miaka 18 nikiwa kama mtoto wa kwanza na wadogo zangu wanne ambao mimi ndo kama kiongozi wao.......................

Kwa sasa mama yangu anaumwa na wiki mbili zilizopita mama aliniita akaniuliza,....."Je upo katika hali ya kujiamini nikueleze haya ambayo ninataka kukueleza?"...........Nikamwambia mama, mbona unaniweka mashakani?.... Kuna nini?.... Akaniambia, kama unakumbuka,,,hadi sasa haujui ni kitu gani ambacho kilimuua baba yako, na zaidi sana mdogo wako wa mwisho hataki shule anaokenana kama vile anachanganyikiwa hivi....... na anayekufuata anaonekana kama vile ni mjamzito na ndo kwanza  yupo kidato cha nne yani ni matatizo kila upande, familiya imepoteza ustawi wake na baba ametuachia madeni mengi sana na miradi yote imefilisika...................

Mama aliendelea,,,,,,"Na sasa, ninaona nakaribia kufariki na wewe kama mtoto wa kwanza sina budi kukueleza na kukukabidhi suala hili la muhimu"........ Nilishtuka kidogo nikamwambia aseme tu ili nijue mapema. Mama yetu alifanikiwa kuwa na asilimia kubwa sana ya kuchangia pato la familiya zaidi ya baba. Jambo hili hatukuwahi kulielewa na mama hakuwahi kutueleza chochote kuhusu usitawi wa baba kiuchumi......Mama aliendelea kusema kuwa, kuna dawa nilipewa na mganga nikaitumia vibaya na matokeo yake ndo chanzo cha kumuua baba yenu na zaidi sana mdogo wako wa mwisho kuwa kama vile amechanganyikiwa. Maneno haya yalinifanya nicheke kwani nilidhani mama kapatwa na "cerebral Malaria". Lakini kunihakikishia siyo, alirudia tena kwa ufasaha.............................................................hii ilinifanya nizimie kwa muda....Kumbe mama yangu allikuwa "MCHAWI" na lengo lake mimi nirithi huo uchawi kwani alisema yeye alirithi kwa bibi yangu na ni lazima mimi kama mototo wa kwanza niurithi la sivyo "NITAFARIKI BAADA YA YEYE KUFARIKI na FAMILIYA NZIMA ITAPOTEA KABISA".

Ndugu zangu, nampenda sana mama na familiya yangu lakini pia namwogopa Mungu sana, nina mengi ya kurekebisha katika familiya yangu. Ninaomaba ushauri wako wa dhati kabisa ili nitoke hapa nilipo. Mama yangu amelazwa ICU-Bugando na ana  hali mbaya sana.........................nitafanyaje? kabla hajatangulia mbele ya haki? Na kila siku  anasisitiza kuwa lazima nipokee 'hirizi" iliyomuua baba yangu na kutuletea matatizo yasiyoisha?.............

Ni mimi nduguyo..

Godson- Nyamagana-Mwanza.

NB; Mpenzi msomaji, baada ya kusoma kisa hiki...usiache kutuma "USHAURI" wako kupitia blog hii kwenye comment box au kwenye e-mail hii sonnelly06@gmail.com 

Usikose safu hii kila Jumapili, karibu tushauriane..........................

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda