Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, September 27, 2012

KUUNGUA KWA ZAHANATI AYALABE TUNAKULA MATUNDA YA UJINGA WETU

Na Henry Msuya
Ayalabe-Karatu
Ijumaa ya tarehe 21 September 2012 zahanati ya Ayalabe iliyopo Karatu iliungua na kuteketea kwa moto kitendo kilichogusa hisia za wadau mbalimbali. Mmoja wa wadau hao ndugu Henry Msuya G alieleza hisia zake kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook "alifunguka" kuhusu kile anachokiamini kuhusu ajali hiyo ya moto. Endelea...."Naandika makala hii nikiwa na masikitiko makubwa kwani kwa kipindi sasa itanibidi nipigwe na vumbi kwenda kutibiwa kwenye zahanati za foleni ndefu katika mji wetu wa Karatu masikini nilizoea naenda nachukua dawa nasepa mh ila acha niseme kuungua/kuunguzwa kwa zahanati hii ni matunda ya UJINGA wetu
KWANINI?

1. Mida ile ya saa 9 usiku wananchi tulifika pale badala yakuonyesha jitihada kuzima eti tunashangaa moto(aibu kwetu) wengine wanasema maji hayakuwepo kweli ila udongo nao haukuwepo?? Majembe hayakuwepo? Au beleshi? Mmbona tuliweza kutoa meza kabati nk

2. Narusha lawama kwa KAVIWASU moja kwa moja kwani wananchi walipiga simu mara kadhaa kuomba maji yafunguliwe wakatia ngumu YES si wamazoea ubabe wanafungua maji dakika 5 wanafunga e
eenh eti ukame weeeee 2006 hakukuwa na ukame? Mbona tulipata maji japo mgawo wa umeme ulikuwepo??? Acheni sound semeni watumiaji wameongezeka vyazo vimebaki vilevile unategemea nini

3. Hivi huyu mlinzi tumefika pale anasema chanzo ni Gesi nikauliza Mbona chumba chenye Mtungi hakijaungua???? Haiiingii akilini gesi ilipuke chumba kisidhuriwe ghafla wanageuka eti ni SOLAR mmmmmh sijawahi sikia sola inaunguza nyumba itabidi hii iiingizwe kwnye kitabu cha Maajabu ya DUNIA

4. Kama kweli ni sola Huyu Fundi aliyefanya wiring alifanyaje lazama tuulize ila kwa mimi niliyesoma umeme it is not possible nakataa; umeme usingewaka au nasema sio mtu alijifanya analeta za kuleta akafanya Short circuit ikasababisha moto siju labda ila mmmmmmmm

5. Nauliza lile gari jekundu nalolionaga limeandikwa fire linazima Moto upi? Au ni urembo kama ni urembo Halmashauri itarajie kuaibika maana sasa Karatu imekua na matatizo ya moto yanaweza kutokea tena na tena juzi tu nyumba ya mfanyakazi wa halmashauri imeungua yote

6. Viongozi wetu hivi wao wanaweza kuhamasisha watu katika kampeni tuuuu? SIKU ILE YA MOTO hakuna hata kiongozi mmoja aliyehamasisha watu kuzima moto ule jamani bado elimu ya maafa inahitajika kwa wote

7. Mwisho zifanyike jitihada za haraka kureja ujenzi wa zahanati hii maana ni msaada mkubwa kwa wakazi wa NMC, MARERA, KINIHE, AYALABE YOTE KWA UJUMLA

8. Haya ni matunda ya ujinga wetu ila mmmh lazima tujiangalie kwa upya
Tahadari yangu huu ni mtazamo wangu tu ufanyike uchunguzi huru kujua ni nini? Na ni nani? Aliyesababisha moto huu mwisho wa siku ajulikane hata kwa yale maombi ya wazee wetu MUNGU IBARIKI AYALABE MUNGU IBARIKI TANZANIA NAWAPENDA WOTE
;;;;;;;; makala hii imeandikwa na Henry Msuya;;;;;;; anapatikana kwa henry.msuya@yahoo.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda