Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, September 20, 2012

Hongera sana Haydom Safaris: Kampuni ya kwanza ya Utalii Haydom

Kwa niaba ya Ohayoda na wanaHaydom kwa ujumla tunapenda kutoa pongezi zetu za dhati kabisa kwa Kampuni mpya kabisa ya Utalii na ya kwanza kuwepo Haydom yaaniKampuni ya Haydom Safaris. Kwa muda mrefu sasa wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakifika Haydom kwa shughuli mbalimbali hasa kuja kujionea tamaduni za jamii za huku, lakini hakukuwa na Kampuni yoyote hapa Haydom ambayo imekuwa ikijishughulisha na kuwahudumia wageni hao badala yake wamekuwa wakiletwa na makampuni hasa yaliyoko Arusha na hivyo mapato hayo kutokuwa na faida yoyote kwa jamii ya Haydom
Uwepo wa Haydom Safaris utaongeza idadi ya taasisi zinazotoa huduma hapa Haydom na kuzidi kuchochea maendeleo na kuongeza wigo wa kiuchumi siyo tu Haydom bali pia katika wilaya ya Mbulu na Mkoa wa Manyara kwa Ujumla.
Ohayoda ilipata fursa ya kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Haydom Safaris bwana Clemence Paresso ambaye alikuwa na haya ya kueleza

Blogger: Ngrrrrrrrrrrrrrrrr ngrrrrrrrrrrrrrrrrr ngrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Clemence: Hallo Amani mambo vipi mwana?

Blogger: Shwari kaka hakuna shari
Clemence: Upo Haydom hii hii au umesafiri?

Blogger: Nipo tele kiongozi...kaka kwanza Hongera kwa kuanzisha Kampuni ya Utalii Haydom
Clemence: Nashukuru Mkuu

Blogger: Haydom Safaris imepata usajili lini? na inatoa huduma zipi?
Clemence: Haydom Safaris imepata usajili rasmi wa BRELA tarehe 10 Agosti 2012 na tuatoa huduma za safari hasa Utalii wa Kiutamaduni yaani Cultural Tourism katika maeneo ya Haydom ambako kuna vivutio vingi sana ambavyo wageni hupenda kutembelea mfano michoro ya kwenye mapango yaliyopo Murkuchida, Qamatananat na Mkalama, kuna mlima Hanang ambao ni wa tatu kwa urefu nchini Tanzania ukiwa na mita 3418 juu ya usawa wa bahari, kuna ziwa Basotu ambalo limezungukwa na "crater lakes" zipatazo tatu na kuna "Asteroid" yaani kimondo kilichopo maeneo ya ziwa hilo. Vile vile kuna bonde la Yaeda chini ambako unaweza kujifunza kuhusu utamaduni wa wahadzabe na mambo mengine lukuki.

Blogger: Wateja wenu haswa wanatoka wapi?
Clemence: Kwa sasa wateja wetu ni wageni wa Haydom hasa wanaokuja Hospitali ya Haydom kama Volunteers, wataalamu na wanafunzi hasa kutoka Norway. Lakini tunatoa pia huduma za utalii wa ndani hasa kwa shule, hospitali na watu binafsi wanaopenda kwenda kwenye hifadhi za taifa na hata katika maeneo hayo niliyoyataja

Blogger: Haydom Safaris ni kampuni ya kwanza kabisa ya Utalii hapa Haydom, je Uwepo wa Haydom Safaris utainufaisha vipi jamii ya Haydom?
Clemence: Haydom Safaris itafungua fursa nyingi  hasa kwa vijana wa Haydom ambao ndio watakaokuwa waongoza watalii yaani "tour guides" na hivyo kutoa ajira kwa vijana. Mfano tuna vijana kama Elifadhili na wengineo ambao watanufaika moja kwa moja. Pili Haydom Safaris itakodisha magari kutoka kwa wadau mbalimbali hapa Haydom mfano bwana Mangi na watoa huduma za malazi na chakula nao watafaidika na Haydom Safaris.

Blogger: Una wito gani kwa watoa huduma hasa Chakula na Malazi hapa Haydom?
Clemence: Bado ubora haurudhishi japo wanajitahidi mfano Ndorobo Guest House, Bajuta Guest House, Jimbo Guest House, Gidabiyonga, IM Hotel na Guest House ya Hospitali kwa ujumla wanajitahidi lakini bado havitoshelezi na kwa upande wa chakula jitihada zaidi zahitajika.

Blogger: Tunashukuru sana kwa kutupa muda wa kufanya mahojiano nasi
Clemence: Mimi nashukuru zaidi, muda wowote tuwasiliane

Unaweza kufahamu zaidi kuhusu Haydom Safaris kwa kutembelea ukurasa wao wa Facebook unaoitwa Haydom safaris au https://www.facebook.com/HaydomSafaris au kwa njia ya Simu 0783711615

Ohayoda inaitakia Haydom Safaris mafanikio mema na pia tunatoa wito kwa wadau mbalimbali hasa wanaotoka Haydom na Hata maeneo mengine kuja kuwekeza Haydom kwani kuna fursa nyingi sana za uwekezaji na kuleta mabadiliko katika jamii ya huku.No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda