Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, September 10, 2012

Historia yaandikwa Haydom: Haydom Cultural Festivals yatia Fora

 • Maelfu ya wananchi wahudhuria, yafunguliwa na DC Mbulu na kufungwa na RAS Manyara
 • Makampuni na taasisi zaidi ya 15 zashiriki, NMB na Ensol watoa udhamini
 • Mashindano ya Ngoma na riadha yafana sana
 • RAS Manyara aagiza Mlima Haydom uhifadhiwe

Baada ya maandalizi na subira ya muda mrefu hatimaye lile Tamasha lililokuwa likisubiriwa kwa Hamu kubwa na wananchi mbalimbali wa Haydom na Maeneo ya jirani limefanyika katika viwanja vya kituo cha utamaduni Haydom (4CCP). Tamasha hilo yaani Haydom Cultural Festivals 2012 lilifunguliwa rasmi tarehe 6 September 2012 na mkuu wa wilaya ya Mbulu mheshimiwa Anatoly Choya aliyekuwa anamwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara mheshimiwa Elaston Mbwilo.

Tamasha hilo la siku tatu lilifikia kilele siku ya Jumamosi tarehe 8, na kufungwa rasmi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara (RAS) kwa niaba ya mkuu wa mkoa, ambaye baada ya kukagua shughuli za 4CCP na mabanda ya washiriki wa maonesho kutoka taasisi na makampuni mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Manyara ambapo wananchi mbalimbali walipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii zinazofanywa na taasisi hizo.

Makampuni na Taasisi hizo ni Benki ya NMB ambao walilidhamini Tamasha hili kwa kutoa fedha za kitanzania shilingi Milioni 5, Kampuni ya Ensol (T) Ltd inayotoa huduma za vifaa vya Solar, Hifadhi za Taifa Tanzania kupitia Tarangire National Park, Idara ya mambo ya kale na Makumbusho ya Mwalimu Nyerere chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Tanzania Cultural Tourism Programme iliyo chini ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Red Cross Tanzania, Engaj (ubuyu-Dodoma), African Designers Arusha, Barbaig Traditional Wear-Katesh, Kikundi cha Wanawake Uvumilivu Kankanala, Haydom Lutheran Hospital kupitia Idara za Kisukari, Maabara, Amani Ward na CTC, Chuo cha Ufundi na Ujasiriamali Haydom, Bustani ya Miti Sighis Endaharghadatk, Wahunzi Injur, Best Food Market, Camp Davis Hotel Haydom na kikundi cha wanawake Ng'wandakw.

Aidha katika tamasha hilo, kikundi cha ngoma cha Wadatooga Qandach kiliibuka kidedea katika mashindano ya ngoma na kujinyakulia shilingi 100,000, nafasi ya pili ilichukuliwa na ngoma ya Hadzabe Kipamba waliojitwalia 75,000 na ngoma ya kina mama Mazangiri walijinyakulia 50,000.

"Kwa niaba ya Timu nzima ya Maandalizi, 4CCP na jumuiya nzima ya Haydom tunapenda kuwashukuru wote walioshiriki katika kulifanya tamasha hili kuwa na mafanikio ya hali ya juu" alisema Eliminata Awet ambaye ni mratibu msaidizi wa 4CCP.

NIPO KWA SABABU UPO!

2 comments:

 1. Hongereni sana wadau woooooooooote mliofanikisha hilo tamasha ya Haydom. Nimelifuatilia .... nimependezwa sana.

  NAAMINI FUTURE ITAENDELEA KUNG'AA ZAIDI!!!

  ReplyDelete
 2. Mkuu weka na Picha...

  Ras Manyara ni Cheo kumbe!

  Hongera Sana kwa Kufanikisha hilo Tamasha...

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda