Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, September 24, 2012

FLATEI GREGORY MASSAY: Ajitokeza kugombea Ujumbe wa NEC Taifa kutoka Mbulu

 • Adai Yeye ni Jembe la kung'oa sangari lililoingia ndani ya CCM

  Asema anavigezo vyote na amebobea kwenye chama kwa miaka zaidi ya 27

  Wakati joto la kuwania nafasi ya mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi NEC kupitia wilaya ya Mbulu likizidi kupanda, mwanasiasa kijana na maarufu wilayani Mbulu Bwana Flatei Gregory Masay amejitosa kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa katika kutunga sera na itikadi za chama hicho tawala nchini.
  Flatei Gregory Massay, kada maarufu wa CCM

  Flatei ambaye kwa sasa ni katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Mbulu na pia Mkoa wa Manyara, ameiambia Ohayoda mjini Haydom wakati wa uchaguzi wa CCM tawi la Haydom kuwa amepata uzoefu wa kutosha kwani amekulia katika chama toka akiwa mdogo na anakijua vizuri chama na anauchungu na chama tofauti na watu aliowaita "Sangari" ambao wameingia ndani ya chama na kuchafua hali ya kisiasa katika wilaya ya Mbulu huku wakitumia fedha kupata madaraka pasipo kuwajali wananchi na maslahi ya Chama

  "Nilianza kuwa chipukizi wa chama cha Mapinduzi mwaka 1985 wakati Mwalimu Nyerere anakuja Mbulu kufungua Jengo la Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbulu na Uwanja wa Mpira wa Nyerere Stadium ambapo nilikuwa "right marker" katika gwaride la chipukizi, mwaka 2002 nikachaguliwa kuwa katibu mwenezi wa chama wilaya ya Mbulu na mwaka 2007 nikachaguliwa kuwa katibu mwenezi wa mkoa nafasi ambazo nazishikilia mpaka leo" alisema Flatei

  "Nimekitumikia chama kwa hali na mali hasa katika kueneza itikadi za CCM na nimekuwa kama jogoo ambaye huwaamsha watu asubuhi lakini hawezi kufungua mlango, lakini najiona mimi Jembe la kutoa sangari ambalo limeingia katika ardhi ya Mbulu kisiasa, kiuchumi na hata kiutamaduni, kuliko kila siku kupiga debe lisilofika mahali nieona bora niitumikie Mbulu kwa kuiwakilisha ndani ya NEc kwa kuwa NEC ndicho chombo kinachotunga sera na Ilani ya CCM na kueneza itikadi ya CCM, nafasi ambayo ninaimudu" Aliongeza Flatei ambaye pia ni mwanzilishi wa kikundi maarufu cha sanaa kinachoitw Tumaini Sanaa Group ambacho kimetoa ajira kwa vijana wengi na kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi.

  Flatei Gregory aliongeza kuwa kutokana na utumishi wake uliotukuka ndani ya chama na mchango wake kutambulika, aliteuliwa kuwa moja wa vijana sita walioukimbiza mwenge wa Uhuru nchi nzima mwaka 2010 na kuukabidhi mwenge huo kwa mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ukiwa salama huku wakitekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi na kutunukiwa vyeti na nishani ya utumishi uliotukuka kwa zoezi hilo.

  Flatei ambaye alikuwa akiongea kwa hisia kali aliongeza kuwa ni wakati muafaka kwa viongozi wa CCM kuteuliwa kwa uwezo na vigezo na si kwa kuangalia uwezo wa fedha kama ambavyo baadhi ya wagombea wenzake wanavyotumia nguvu zao kifedha ili kupata nafasi za uongozi na hivyo kuliweka jimbo rehani kwa wapinzani

  Aidha Ohayoda ilitaka kujua analizungumiaje suala la CCM kupoteza jimbo la Mbulu wakati yeye akiwa katibu Mwenezi, Flatei alifunguka kwa maneno haya
  "Ni kweli tulipoteza jimbo mwaka 2012 na sababu zinajulikana, pia ikumbukwe kuwa ni wakati huo nilikuwa katika jukumu la kitaifa la kuukimbiza mwenge na hivyo kutokushiriki kikamilifu katika kampeni. Lakini nilifika katika hatua za mwisho na kuipa ushindi CCM katika kata ya Endagikoti ambayo kama ingeenda upinzani basi CCM ingepoteza Halmashauri lakini nilipewa hilo jukumu na kulitekeleza kikamilifu na kuiwezesha CCM kupata nafasi ya diwani wa viti maalum na kuipa uwingi wa madiwani katika Halmashauri"

  "Ninawaomba wanachama wa CCM kuwa kama jina langu likirudi wanipe nafasi niwatumikie kwani uwezo ninao na nina nafasi ya kuwatumikia kama kijana na ninaubunifu, nimewawezesha vijana wengi kupata ajira na ninaamini kuna mengi ambayo kama kijana ka kushirikiana na vijana wenzangu tunauwezo wa kuyafanya na kuleta mabadiliko Mbulu" Alimaza kuongea Flatei

  Flatei Gregory Massay alizaliwa mwaka 1972 wilayani Mbulu na mwaka 1986 akiwa na umri wa miaka 14 tu alianzisha kikundi cha sanaa cha Tumaini Group, kikundi ambacho kimejizolea umaarufu mkubwa siyo tu wilayani Mbulu na nchini kwa ujumla bali pia nje ya nchi na kimetoa ajira kwa vijana zaidi ya 50, kikundi ambacho ohayoda iliwahi kuandika katika moja ya makala zake huko nyuma (bofya hapa http://ohayoda.blogspot.com/2012/05/shujaa-wa-wetu-flatei-gregory-massay-wa.html)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda