Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, September 2, 2012

BREAKING NEWS: ALIYEDAIWA KUTEKWA AREJEA SALAMA SALIMINI

 Na Amani Paul-Haydarer
Kama ni filamu au tamthilia basi mwandishi na muongozaji wake wameicha hadhira katika hali ya "suspense" yaani hawaelewi kinachoendelea. Filamu ilianza kwa mbwembwe sana, ikaamsha hisia za hadhira maelfu kwa maelfu wakanunua nakala za filamu hiyo, kujua hatma ya starring wa filamu hiyo ambayo ilianza kwa nyota huyo kutekwa na kulitelekeza gari lake porini.

Hatimaye Hhando Samo amerejea nyumbani kwake baada ya kupotea kwa takribani siku 5 baada ya kile alichokieleza kupitia ujumbe mfupi wa maneno kuwa ametekwa akiwa na zaidi ya shilingi milioni 84 na kuwa gari lake lipo Ilongero. Ohayoda iliandika mkasa mzima bofya hapa http://ohayoda.blogspot.com/2012/09/sakata-la-utekaji-haydom-lachukua-sura.html

Swali kubwa ni je ni kweli alitekwa? Imekuwaje arudi salama bila hata jeraha? Na kama hakutekwa, ni kwa nini azushe suala zito namna hii? Wajuzi wa mambo wanadai kuwa inawezekana alikuwa anadaiwa na akaona mbino ya kuyaepuka madeni hayo ni kupika utekaji huo.

Mpaka ninapoandika habari hii, watu wamekusanyika kwa uwingi sana nyumbani kwake Haydarer, ni halaiki kubwa sana pengine hata zaidi ya wale waliojitokeza kwenda kumtafuta.......

Ohayoda itawajuza yanayoendelea kujiri........Jumapili njema

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda