Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, September 3, 2012

Baada ya Sangwine, Melankoli na Koleriki sasa ni Flegmatiki, Mwanadamu anayefahamika kwa "Unyofu wake wa Moyo" (Know Your Personality)


Katika hali tusiyoifahamu wanadamu, Mungu ametupa nafasi ya kuwa na hulka za tofauti sana na akahakikisha kuwa kila mmoja anakuwa kama alivyo lakini zaidi sana wote wana sifan njema na mapungufu japo kuna wengine ambao wana ubora kuliko wengine na wengine wana "mapungufu mengi kuliko ubora", na wengine wana "ubora wa kiasi kikubwa kuliko mapungufu yao". Hizi zote ni sifa za Mungu aliyekuumba wewe na mimi.

Japo kwa tofauti hizi bado Mungu antupenda na anatupa njia mbalimbali za kujitambua na kuweza kuishi na kila mmoja wetu. Ndo maana kuna masomo kama haya ya na yanatupatia mwelekeo wa namna ya kuenenda na kuvumiliana ili tu dunia iwe mahali pema pa kuishi. Tulijifunza sana kuhusu Sangwini, Melankoli na Koleriki, sasa tunapata tena nafasi ya kujifunza kuhusu Flegmatiki.

Baada ya kujifunza tabia za makundi mbalimbali katika kuwafahamu wanadamu na hulka zao mbalimbali tangu tuanze safari hii kwa kuwaangalia wote katika tofaurti zao mbalimvbali, sasa tuwaangalie wanadamu waliopo katika kundi la Flegmatiki.

Kwa asaili anafahamika kama “mtu mnyoofu”, tabia yake na mwenendo wake huonesha kuwa yeye ni mtu asiyependa makuu, mwenye kukubaliana na kila jambo na kadhalika. Mwanadamu ambaye si wa kundi hili hutokea kuona kama vile wao ni watakatifu sana na hakika hawakose lolote katika utendaji wao.

Kwa utangulizi tu ni kwamba, kuna watu ambao mara nyingi hawa si wasemaji sana, si wepesi kujibu, kwa nnje huonekana ni waoga sana, wanaonekana kuwa hawana mahangaiko ya moyo, wanaopenda sana kujifunza, wanautulivu wa ndani na wa nnje, wanauwezo mkubwa sana wa kuwa wanadiplomasia wazuri, wanahuruma sana pindi wanapokuwa wanadili na wanadamu wa makundi mengine, uwezo wake wa kuishi na watu vizuri humfanya awe na marafiki wengi sana. 

Baada ya kupata utangulizi huu, kipindi kijacho tutajifunza dondoo za sifa njema za Flegmatiki, na zaidi sana tutajua kuwa kwa kuziangalia tabia zake ni rahisi sana kufahamu huyu ni mtu ni wa namna gani na anatofauti gani na watu wengine.

Maswali ya msingi ambayo tunapaswa kujiuliza:-
  1. Je, watu wote wapole ni maflegmatiki?
  2. Je, watu wote wakali ni makoleriki?
  3. Je, watu wote wanaochecheka marakwamara ni masangwini?
  4. Je, watu wote walio "serious" ni mamelankoli?
Stay tuned.........................B: Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA au JINA LA HAIBA/TABIA FULANI kama vile Koleriki, Melankoli au Sangwini" kwenye search engine yetu ili kupata tulipoanzia hadi tulipo. 
 
Namailizi kwa kusema......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu, ni zawadi ya KUJITAMBUA (A point of self-Actualization) katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili 
 ya sifa na utukufu wake YEYE mwenyewe.
Unajitambua? Au Unaishi tu kwa sababu siku zinaenda?


KAMA KAWA,, MUNGU AKUTUNZE...0753-038005
sonnelly06@gmail.com 
(We are little Beings, trying to give you the little we have)

Tuonane Ijumaa...............................No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda