Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, August 7, 2012

Wahdzabe Watishia kugomea Zoezi la Sensa

Na Amani Paul
Zikiwa zimebakia siku chache kabla halijanyika lile zoezi kubwa kuliko zote za kitakwimu nchini yaani Sensa ya Watu na Makazi baadaye mwezi huu, jamii ya Wahadzabe iliyoko katika bonde la Yaeda katika wilaya za Mbulu, Iramba na Karatu wamelalamikia kutokupata fursa sawa katika zoezi la usimamizi wa shughuli hiyo.
Wahadzabe maeneo ya Mongo wa Mono

Akizungumza na Ohayoda mratibu wa shirika la Hadzabe Survival linalojihusisha na kutetea na kulinda ustawi wa jamii ya Wahadzabe lililoko mjini Mbulu ndugu Edward C. Endeko alisema kuwa zoezi hilo limewabagua wahadzabe kwa kutokushirikishwa kwatika zoezi hilo na hivyo wao kama jamii wanaona hawajafanyiwa haki hali inayoweza kupelekea kususia zoezi hilo.

"Tangazo lilitoka kuwa watu wenye sifa watume maombi kuhusu usimamizi wa sensa kama makarani, kwa upande wa jamii ya Wahadza vijana wengi ambao walikuwa na hizo sifa walifanya hivyo lakini cha kushangaza walipigwa chini kitu ambacho kwa kweli iliwafanya vijana hao wakate tamaa kabisa ya kutuma maombi yoyote yatakayowataka wao waombe serikalini ili kupata shughuli hata kama ni ya muda mfupi.Wengine waliambiwa eti hawawezi kufanya kazi kwa kuwa ni wanywa pombe,hiyo kama siyo kashfa ni nini? Wengine pia waliambiwa hawana uzoefu na mbaya zaidi watu waliowekwa kuwa makarani wanazidiwa elimu na vijana hawa" alisema kwa mratibu huyo.

"Kuna vijana ambao wamefika kidato cha sita lakini walipita na baadaye kukatwa bila sababu zozote.Sisi ni Watanzania,na kwa mfano mtu kama huyu akikataa kuhesabiwa atakuwa amefanya kosa? na ni nini faida ya hawa vijana kwenye jamii yao? Hongo bado ipo,lakini kwa kuwa sisi hatukuwa na pesa za kuhonga ndiyo maana walizokuwa na hizo pesa walipewa nafasi hizo. Isije kuonekana vibaya kama kashfa hizi zikifika kwa jamii ya Wahadzabe wakakataa kuhesabiwa maana si vizuri.mimi mwenyewe imeniuma sana kwa kuwa aliyetupiga chini ni jamaa yetu wa karibu sana alafu anajisikia sana.Hatutaki mazoea naye na yeye asituzoeeee" aliongeza bwana Endeko aliyeonekana kukerwa na kitendo hicho.


Katika hatua nyingine, Endeko alieleza kuwa baada ya kupata malalamiko hayo kutoka kwa hao vijana wa Kihadzabe juu ya kitendo hicho, alimtafuta afisa ustawi wa jamii wilaya ya Mbulu ndugu Ezekiel Asecheck ambaye ndiye anayehusika na zoezi hilo, lakini afisa huyo alimjibu vibaya na kupelekea yeye (Endeko) ambaye awali aliomba kusimamia zoezi hilo na kupata lakini baadaye yeye pia jina lake liliondolewa.


"Majina yalishatoka, mimi siyo crazy (mwendawazimu) natetea nafasi za Wahadzabe kwa nini wasiwepo? Hao waswahili aliowaweka watafika Mapomba, Bashana, Sililiako na Maeneo mengine ambayo wahadzabe wapo? Ndiyo maana idadi ya wahadzabe bado ni ndogo kwa kuwa hawahesabiwi wote" alisema bwana Endeko kwa ukali

"Huu niuonevu mkubwa sana tena wa makusudi na kwa hili sisi wahadzabe hatutakaa kimya, katika maeneo yote ya wahadzabe wamewekwa watu wengine na ni mhadzabe moja tu anayeitwa Pili Gudo ndiye amechaguliwa naye sijui hatima yake, anasingizia zoezi litafanywa na walimu lakini si kweli kwani kuna watu wamechaguliwa wameishia kidato cha nne tena walifeli" alimaliza kuongea bwana Endeko


Aidha Ohayoda ilimtafuta Ezekiel Asecheck ambaye anatuhumiwa kwa "kuwafanyia fitna" wahadzabe alikanusha madai hayo

"Malalamiko hayo hayana msingi wowote kwani mpaka dakika hii majina ya waliochaguliwa hayajatoka bado, na hata na hivyo wahadzabe wengi hawana vigezo" Alisema ndugu Asecheck
Aidha Ohayoda ilipotaka kujua vigezo vinavyohitajika kuwapata makarani kwa ajili ya sensa ndugu Asecheck alisema vipo kwenye mtandao lakini akataja kimoja kuwa "kidato cha nne" hawatachaguliwa.

Na kuhusu madai ya Endeko kuwa ameondolewa kwenye zoezi hilo alisema "Kwanza mimi ni mkufunzi tu na sihusiki na kuchagua majina, ila kuhusu Endeko ni kweli aliomba na anavigezo lakini nilimshauri kuwa hataweza kufanya hili zoezi kwa kuwa yeye ni mlemavu wa mguu na zoezi hili litambidi atembelee nyumba nyingi, na japo Endeko anadai kuwa anatumia pikipiki lakini kule ni porini, lakini hata na hivyo mimi sihusiki anayehusika ni DCC  (mtakwimu wa Wilaya).


Kwa muda mrefu jamii ya Wahadzabe ambao idadi yao inafikia watu 2300 tu imekuwa ikilalamikia uvamizi wa ardhi yao kutoka kwa makabila yanayowazunguka na hivyo kutishia ustawi wao kama jamii kwani wao hutegemea uwindaji na ukusanyaji wa matunda, mizizi na asali kama njia ya kujipatia riziki. Endapo watasusia zoezi hilo serikali haitaweza kujua idadi kamili ya wahadzabe hivyo kushindwa kupeleka huduma kwa jamii hiyo kama inavyopaswa

Wakati huo huo mafunzo kwa makarani wa sensa katika wilaya ya Mbulu yanatarajiwa kuanza Alhamisi ya tarehe 9 Agosti na ikiwa imebaki siku moja tu mafunzo hayo kuanza bado waliochaguliwa hawafahamiki hivyo kutia mashaka kama mafunzo hayo yatafanyika kama ilivyopangwa.


Mafunzo hayo hayo yatafanyika kikanda (kitarafa), na Ohayoda itawajulisha yanayojiri katika zoezi hili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda