Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, August 22, 2012

Wafahamu Makoleriki ili Ujue ni Njia gani Utazitumia Katika Kuishi naye bila kusababisha Migogoro kwenye jamii. (Become a Blessing By knowing the Best way to live with Them)Na Nelson Faustin.
Tulipata nafasi ya kuwafahamu japo kwa kifupi wanadamu wenye tabia za kundi la Koleriki na nikashauri kuwa kama hujui tunaandika kuhusu kitu gani jaribu kuandika neno "Haiba" kwenye serch engine hapo juu ili ujifunze zaidi au uangalie upande wa kulia wa blog hii utaona mtiririko wa masomo haya na lengo la kuandaa masomo haya kwenye blog hii.

Leo tunajifunza juu ya dondoo za muhimu zitakazo tusaidia kuishi na mwnadamu mwenye tabia za Koleriki, ni muhimu sana kufahamu tabia zake na zadi sana kufahamu mapngufu yake mambo ambayo tayari tumeshajifunza.

Jambo ambalo limebaki sasa ni kujifunza kuishi nae, kwani tutakutana naye mahofisini, majumbani, misikitini, kanisani na duniani kwa ujumla ila kazi ngumu inakuwa kwenye njia bora za kuweza kuishi naye kwani kwaasili hawa ni watu ambao wanatumia nguvu sana na ni kama vile hawana huruma hivi lakini hatuna budi kuishi nao.

Dondoo zenyewe ni kama vile:-
 •  Pasipo unafiki, jaribu kumuonesha kuwa unautambua uwepo wake kwa kumpongeza au kumkaripia pale anapofanya jambo ili ajue kuwa na wewe upo makini na matendo yake.
 • Kama inawezekana, mpe nafasi ya kuwa kiongozi sehemu ambayo umeona kuwa anaihitaji sana ili kutimiza hitaji lao la uongozi ila kama umempita umri na nafasi jitahidi kumpa uangalizi hata kama hataki.
 • Kama unafanya naye kazi jitahidi sana kufanya kazi yenye manufaa na matunda mazuri kwani kwa kufanya hivyo utamfanya akupe nafasi kwenye moyo wake na kwa hili unaweza kumpa ushauri au kumkosoa bila ya yeye kukasirika.
 • Wasaidie kuona hasara wanayoisababisha kwa kufanya kazi pasipo kuzingatia mpangilio na uhalisia wa kazi zenyewe.
 • Fanya kazi yako kwa ufanisi ili asipate nafasi ya "kukuburuza". Hawa wajamaa hawana "appreciation" kutokana na hili usisononeke pale unapoona umefanya vizuri lakini bado haridhiki na anaendelea kukuburuza.
 • Jitahidi kuwa mtiifu na si mnyonge.
 • Wakati mwingi ni watu wa kugomba sana, usimjibu katika kugomba kwake, mwache akimaliza ndo useme tena kwa uchache. Lakini pia ukimya au kujibu kwa sauti ya upole ni bora kuliko vyote.
 • Usitafute mashindano na Koleriki. Ukitaka kufanikiwa kuishi na Koleriki, basi usimpe nafasi ya kushindana naye, fanya kama vile unakubali kila kitu lakini kutokana na muda ataelewa kuwa si kwamba umemsikiliza bali umemgundua kuwa anapenda vyakwake tu ndo vipewe kipaumbele.
 • Kuwa na msimamo katika kile unacho kiamini kama  ni chema/sahihi.
 • Simaimia ukweli ili uwe huru lakin pia ongea mambo kwa ushahidi na mifano hai ili asipate pa kukukosolea tena kwa ukali, ukiruhusu hali hii itakufanya ukate tamaa na kumchukia Koleriki.
 • Mpe changmoto pale unapoona inasthili na itazaa matunda kwani si watu wa kupokea changamoto kwa urahisi.
 • Akikunesha kuwa huwezi, basi upatapo nafasi jitahidi sana kufanya kwa ufanisi ili aone aibu na hatimaye ataanza kujenga imani juu yako.
 • Kama unajifahamu kuwa wewe si Koleriki nataka nikuhakikishie kuwa kama ilivyo kwa watu wa haiba nyingine Koleriki kwa Koleriki huwa wanafahamiana vizuri na hii huwafanya waweke watu wengine kando, Usijilaumu kwa hili na wala usibadili haiba yako kwaajili hii, fanya kile ambacho unapaswa kufanya kwa usahihi wake.
 • Usiwe mtu wa longolongo unapotaka kumweleza jambo, "be straight foward".
Mpaka  hapo, naamini umepata kitu cha kukusaidia, ungana nasi tena wakati ujao,, 
 
 Kama hukupata fursa ya kuanza nasi katika somo hili la Haiba, andika neno "HAIBA" kwenye search engine yetu ili kupata tulipoanzia hadi tulipo leo, tumeshajifunza HAIBA kuu mbili.


Namailizi kwa kusema.......Kati ya Zawadi Kubwa Ambazo Mungu Amempa Mwanadamu ni zawadi ya KUJITAMBUA (A point of self-Actualization) katika madhaifu na mazuri aliyotuumbia kwaajili 
 ya sifa na utukufu wake YEYE mwenyewe.
Unajitambua? Au Unaishi tu kwa sababu siku zinaenda?
No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda