Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, August 7, 2012

Sikitiko Langu Jumanne Hii....Kwanini Baadhi ya Watu wakiwa Katika Nafasi Nzuri Hujisahau na kuwaona wengine wooote hawana maana?

Na Nelson Faustin Nd. Meku

Kila Mtu Lazima aheshimu UTU wa mwenzake sehemu ya Kazi.
Salaam viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vikundi mbalimbali, maboss maofisini, wenye nyumba za kukodisha na wengine wote wenye nyadhifa mbalimbali ambao kwa bahati nzuri umepewa nafasi katika sehemu fulani kama kiongozi iwe ni yako binafsi au umeajiriwa au ni ya serikali na ya una watu ambao wapo chini yako makala hii inakuhusu sana.

Kwa kuwa kazi ya OHAYODA ni kuitengeza jamii na kumfanya kila mtu auheshimu UTU uliopo ndani ya mtu mwingine? Leo Jumanne sawasawa na Jumanne nyingine zote nitakuwa ninatoa masikitiko yangu kutokana na mambo ya kawaida kabisa yanayoendelea kwenye jamii, najua yapo mengi ya kisiasa na burudani lakini haya nitakayokuwa nayasema yanasikitisaha sana, UTU wa MTU mwingine lazima uheshimiwe.

Nataka nitoe masikitiko yangu kwako/kwenu, Ila mtanisamehe kwa kweli kwani leo itabidi tu tusaidiane kwani kuna miungu watu katikati ya wanadamu. Do not hate me for this. Kwa kuwa blog hii inasomwa na watu wa kila kada basi hata wewe unayesoma hapa upo sehemu sahihi kabisa na kama ishu hii haikuhusu basi we fahamu tu yupo ambaye inamhusu na unamfahamu.

Tunajua kuwa si wote tunaweza kuwa viongozi, lakini hii si sababu ya baadhi yetu kujiona kuwa wao ndio mwisho wa kila kitu kama vile kwa kuwa katika nafasi walizonazo basi wana kila sababu ya kuwafanyia kila baya wanalolitaka kwa wale wanaowaongoza.

Lakini pia, njia zilizotumika kwa wewe kufika katika nafasi uliyonayo zinaweza zikawa ndo sababu ya kuwanyanyasa wengine kwani wengine wamepachikwa tu na ndungu zao, wenginie rushwa, wengine uchawi, wengine ubabe tu, samahani ila wengine elimu mlizo nazo hamkustahili kuwa katika nafasi hizo bali ni kama zali tu, wengine kwa kuwa wana uchu wa madaraka, na hata wale wanaoingia kazini kwa kustahili pia wapo wenye tabia kama hizi tutakazoongelea.

Mbaya zaidi unakuta kiongozi ana umri mdogo kuliko wa wale ano waongoza lakini vituko na vimbwanga unavyowafanyia si vya kawaida. Ndugu wanajamii, baadhi ya maboss wetu wamekuwa na lugha za kutunyanyasa sana na baadhi yetu waemishia kuacha kazi, kunywa pombe au kuvuta sigara kabla hajaenda kazini ilimradi tu ajitoe ufahamu pindi anapokutana na boss kichomi. Wengine japo wanashida ila wameamua kuacha kazi na kuacha hata haki zao za msingi, hapa si kwamba wanajikomoa lakini wanaona ni afadhali waachane na watu wasiojali utu wao.

Kuna dada mmoja alipatwa na stress kutokana na masengenyo ya boss wake aliyekuwa mwanamke hadi akapata miscarriage (imagine....), mwingine aliamua kumdunda ngumi boss wake, mwingine aliamua kumwekea boss wake upupu kwenye maji ya kuoga (housegirl), mwingine aliamua kumnywea pombe na akamtukana mbele za watu, najua ipo mifano mingi sana lakini cha kujiuliza ni kwa nini watu hawa wafanyiwe hivi? Jibu tu ni kwamba tabia zao na matendo yao kwa jinsi wanavyowafanyia wengine ndio sababu ya wao kupatwa na haya yote. Wengine huishia hata kulaaniwa na wafanyakazi wao kutokana na dhuluma na masengenyo yasiyoisha, Boss gani usiyeridhika? Wewe kila wafanyakazi wakifanya huoni, unadhani hao ni mashine? Ungelijua majina wanayokupa.......usingetamani kuishi tena wamekupa majina mengi kama vile, gobore, jinamizi, nyambizi, mpausho, mnoko, kimeo, nyoka, sumu, ngozi ya kenge, bwana pima, bibi kihere na mengine meeeeeeeeengi ambayo hapo ofisini kwenu mnayafahamu ilimradi tu wakuchafue na kukushusha thamani...

Maswali ya Msingi.
Je, Wewe unadhani hiyo nafasi wewe tu ndo unastahili kuwa nayo? Na Je, unadhani maisha ndo yanaishia hapo kwa kuwa wewe ni boss? Hivi tuulizane, Unaona ugumu gani kuwa na mahusiano mazuri na unao waongoza? Au unafurahia sana unapoongea kwenye kikao mwenyewe bila ya hata mmoja kukujibu wala kuchangia chochote? Unadhani wewe na hao wendawazimu wako wachache ndo mmeshikilia muimili wa dunia kwa nafasi mlizo nazo? Mtoto wako/mkeo/mumeo akifanyiwa unavyo wafanyia wengine utajisikiaje? Leo na kesho huna hiyo nafasi, unadhani utakuwa na idadi gani ya wanafiki katika dunia yako? Hivi una habari kuwa una maadui wengi sana wanakuzunguka? (ukitaka kujua kumbuka ulivyopata tatizo nani alikusaidia) Utajisikiaje siku ukifunuliwa moyo wa kila unayemwongoza na ukaona fundo la chuki aliyokuwekea au aina ya maombi wanayokufanyia na ambacho labda angeweza kukufanyia kukudhuru? na Je nyingi sana.......

Kwa nini kila binadamu asione thamani ya UTU ulioko ndani ya mwenzake? Si kwamba maboss msiwe serious na kazi,,,No..Simamia misingi ya kazi ipasavyo lakini pia utambue kuwa unaofanya nao kazi ni wanadamu kama wewe na miongoni mwao kuna kina SANGWINI, MELANKOLI, KOLERIKI NA KINA FLEGMATIKI, ukitaka kuwafahamu hawa fuatilia makala zetu za kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.

Kabla hatujashauriana, ngoja nikupe kisa hapa, Leo ni tarehe 7 August 2012, kuna rafiki zangu wanafanya kazi maeno fulani karibia na Mkoa wa Shinyanga hivi.....sasa hadi leo hawajapata mshara na mhasibu wao kakaa kimya na si mara ya kwanza na ana majibu ya mkato ile mbaya, jamani,,,hata kama kuna tatizo kwenye benki, si uwaambie tu bandugu kwamba kuna tatizo na mishahara itachelewa? Au kwa kuwa unajua kuwa woote wanakutegemea ndio wapate mahitaji yao unataka wakuone kama kamungu mtu? Hao pia ni binadamu nao pia wanahitaji kutiwa moyo wa matumaini...Je kwa stahili hii...chuki zitaisha? Kazi zitaenda? Tutauaga umasikini?

Wakati ninajifunza management, nilijifunza kutoka kwa Mary Parker Follett (1868–1933) kuwa management ni "the art of getting things done through people". Lakini pia  Douglas Murray McGregor (1906, Detroit–1 October 1964, Massachusetts) ambaye pia ni Management Professor alisema kuwa "Theory X and Theory Y relates to Maslow's hierarchy of needs in how human behavior and motivation is the main priority in the workplace in order to maximize output. In relations to Theory Y the organization is trying to create the most symbiotic relationship between the managers and workers which relates to Maslow's hierarchy of needs of Self Actualization and Esteem. For Self Actualization the manager needs to promote the optimum workplace through morality, creativity, spontaneity, problem solving, lack of prejudice, and acceptance of facts. It can relate to Esteem when the manager is trying to promote self esteem, confidence, achievement, respect of others, and respect by others". Naamini umeelewa hapa hata kama hukusoma waombe wakusaidie. Hata ufanyeje, this applies from managing simple to complex organizations. HIZO ZA KWAKO ULITOA WAPI? AU SHULE KWAKO ILIKUWA NI MADESA/MAKARATASI TU?

Ngoja nipunguze hasira..................kwa kuwa uafahamu wajibu wako, utekeleze bila ya kuwatesa wengine kwani hata wao ni wanadamu kama wewe, wana mwili, nafsi, moyo na roho kama wewe, usitumie cheo kama fimbo ya kumchapia mwingine. Leo kwake kesho kwako, kwa jinsi gani hata mimi siju...

Mfanyakazi mwenzangu, najua hii ndo kazi ambayo kwa sasa lazima uifanye, na huna ujanja lazima upate mahali pa kuanzia, ni lazima uvumilie ndugu yangu lakini fanya kazi kwa malengo, timiza wajibu wako hata kama boss wako ni mtu asiyeridhika usimpe nafasi ya kukutesa, acha kujipendekeza kwake kwani kisaikolojia anapata mwanya wa kukumiliki kimawazo, acha kujichekeshachekesha kwani mshahara na maslahi yako hayapimwi katika hilo, have the respectable but smooth relationship with him/her, ila siku unaoondoka hasa kwaajili yake, mwambie kwa hekima na busara ili kumsaidia asije akafa vibaya, na mbingu akaikosa. Muda wako ukiisha ondoka kitaeleweka tu, maisha ni popote, dunia ina watu bilioni saba ujue.

Ndugu zangu, katika haya maisha kila mtu namhitaji mwingine, heshimu kila mtu Mungu anayekupa, kadunia haka ni kadogo sana, tuache kudharauliana katika maeneo ya kazi iwe ni ofisini,Nyumba za kupanga, nyumbani, dukani, sokoni, kanisani, misikitini, kambini, shuleni, vyuoni, na popote pale ambapo kiongozi lazima awepo. Tujitahidi kupendana na kila mmoja aheshimu kazi, taaluma na hitaji la mwenzake kwani sisi sote ni binadamu kinachotutofautisha ni ile tu kuwa wewe umewahi kufanikiwa kabla ya wenzako. Kama ulikuwa hujui, Duniani ni kwa zamu.

Desa hili kama hutapenda kujifunza mwenyewe, utafunzwa na ulimwengu.

Asante japo najua kimukuuma japo kidogo, kama umeguswa please fanyia kazi kama hujaguswa, Jitathmini....

Ni jukumu la OHAYODA kuona kuwa, kazi zinaleta tija kwa mtu binafsi na kwa taifa kwa ujumla.

We remain little Beings, trying to give You the little we have, Receive it please.

(Sorry for this, Lakini kama Katika unaloona hapo
 kwenye picha sote tupo sawa...Ni Kwa nini Tusithaminiane?)

2 comments:

  1. Kaka hongera na punguza hasira yote kwa yote ulicho sema ni sahihi kabisa hata kwa picha za nyumba zetu za milele zina tukumbusha kuwa binadamu wote tuko sawa japo kweli wengine wana jiwehusha nandiyo maana tunafanyiana makusudi katika nafasi zetu za kikazi hata kimaisha,Mungu ameweka fumbo kubwa ndani ya upeo aliotupa na ndiyo maana tunaona pale macho yetu yanapo fikia kikomo laiti kila mmoja wetu angeweza kufunguliwa na kuonyeshwa la kesho au sekunde moja mbele basi Amini Mungu hakuna tajiri wala masikini sote level yetu kimaisha ni moja sema tunazidiana katika katafuta urahisi wa kuyaendesha haya maisha yetu ya kila siku, Namalizia kwa kusema jitihada zenu OHAYODA ni njema sana kwetu na hata kwenu pia so Mungu asimame ili sote tujengane na isiwe tunakasoro za ndani @ Nelson Faustin love you kaka be blessssssssssssssssssss

    ReplyDelete
  2. Kaka ila usisahau kuwa wengine wanajengewa kwa marumaru hakuna udongo unao ingia zaidi ya ule wa Mchungaji

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda