Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, August 28, 2012

Sikitiko langu Jumanne hii...kama hizi ni "Political Propaganda" Basi Hatujengi bali Tunabomoa na inaweza kutugharimu kujenga Upya.


 
Na Nelson Faustin.
Siongelei swala la Polisi na wafuasi wa CHADEMA Morogoro na wala siongelei siasa hapa bali kuna jambo ambalo kwa kweli linakera sana na kama tusipolifanyia kazi mapema kama watanzania basi litatugharimu sana kwa siku za usoni.

Sina mengi sana leo ila tu kama raia wa kawaida kabisa kuna kauli ambayo inaendelea na ninaisema kama nilivyo isikia tarehe 25/08/2012 ambapo katibu wa CCM wilaya ya Mbulu kuna kauli aliyoitoa katibu wa CCM wilaya Bw. Shekue Pashua alipokuwa akitoa rai kwa vijana kwamba, vyama viwili ambavyo ni CUF na CHADEMA vina lengo la kuhakikisha kuwa "DAMU" inamwagika. Eti kisa bendera zao zina rangi nyekundu. Kauli hii sidhani kama ni kwaajili "Propaganda za kisiasa tu" lakini sisi tunaona kuwa inaathari kubwa sana kwa baadhi ya wananchi na usalama wa taifa kwa ujumla jambo ambalo si vyema likaendelea kusemwa hovyo hovyo kutokana na madhara yake baadaye.

Mbali na hapo, nilienda Moshi vijijini nikakutana na wazee fulani wakaniambia kuwa, Mwanangu Nelson, hatutaki kuona chama chenye bendera yenye rangi nyekundu kwani ni ishara ya umwagaji damu. Dah, ilinishtua sana kwani ni idadi kubwa ya watanzania ambayo wamelishwa sumu hii, kwa baadhi ya viongozi wa chama fulani wanadhani wanaweza kuwapata wafuasi wengi, Kwa kauli hii mtafanikiwa kwani watanzania ni waoga sana lakini kwa upande mwingine wa shilingi "mnawaandalia watanzia shimo ambalo watatumbukia humo na nyie mbaki juu mmekaa"

Tuwe makini na kauli zetu, siasa si kumwaga damu, na wala sidhani kama hizo ni kauli za kuueleza umma kama viongozi na kama raia wazalendo,  kisaikolojia tunawapoteza kabisa. Si vizuri, narudia tena jamani si vizuri, siasa za kistaarabu ndo jambo la msingi kwa Tanzania ya leo na ya baadaye.

Tuendelee kumwomba Mungu atusimamie, Kwa mtazamo wangu, nasikia sikia maswala ya dini yakisemwa semwa, sawa tu semeni ila msiende kiasi cha kutupoteza jamani. Bado sisi ni masikini sana, tuna matatizo kibao jamani, bado tena siasa inatusumbua, wengine hawataki kuhesabiwa, wengine mafisadi, wengine wanauana kwa imani za ajabu ajabu, wengine majambazi, wengine manabii wa uongo, bado mnaongeleal swala la bendera na kumwaga damu?  kah.....Tutafika? Embu angalia kauli kama hii hapa ,"‎'kama wao wamejifunza kuua watu, basi sisi tutajifunza kufa.." hao ni wafuasi wa CHADEMA nimeaona leo kupitia ITV baada ya mwenzao kuuawa na Polisi. ...

"Mwenye macho haambiwi tazama"

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda