Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, August 21, 2012

Sikitiko Langu Jumanne Hii, Je, Ni Kwa nini Baadhi yetu sisi vijana Hatuwakumbuki wazee wetu vijijini? Je, Thamani yao kwetu ilitoweka Baada ya sisi kwenda kuishi Mijini?


Na Nelson Faustin Ndelemo.
Mimi kama wewe, nimepata nafasi ya kuishi mjini na hata sasa nipo mjini ila kwa wiki mbili mfululizo nilipata fursa ya kufika kijijini kwetu na baadhi ya vijiji huku nilipo sipataji kwa jina na hii ikanipasa kusikikitika sana nikasena nikushirikishe na wewe haya masikitiko yangu kwani tunajidai hatuoni kumbe tunayaona.

Ni kweli wengi tumesoma na tunafanya kazi mijini popote Tanzania, na wengi hawapendi sana kurudi vijijini kwao kufanya kazi lakini si hivyo tu, hata wengine kwenda walau kusalimia ni kazi, zaidi sana ninasikitika kwani kwa familiya nyingi nilizotembelea zinasitikisha sana. Nimekutana na wazee ambao wanasema watoto na wajukuu wao wapo mijini lakini   kwa ufupi ni kwamba maisha yao ni duni sana. Malazi yao, chakula wanachokula na hata mahitaji mengine yote ni duni sana ukilinganisha na jinsi wewe unavyokula bata mjini huku sisi wenzako tukikuona wa thamani kumbe wa nyumbani kwenu wanaangamia kwa umasikini na njaa kama vile hawakuwahi kuwa na kizazi kilichofanikiwa kuwa na maisha bora nmijini.

Wengi wetu hata kama huwa tunaenda, huwa ni kwa siku moja au mbili, hata kama tupo busy na maisha lakini kwa siku zinavyoenda mbele kuna hatari ya hawa wazee kusahaulika kabisa mpaka hapo tutakapojikuta tunaenda kuwauguza dakika za mwisho huku tukijua fika kuwa wapo mbioni kukata roho. Hii kwa upande mmoja tunaona ni sahihi kwani wengine walidhiriki kusema kuwa "wanamaliza pumzi afadhali wafe wakapumzike", ni sawa ila nafikiri upande mwingine wa shilingi ni kwamba, kuna baraka kubwa na nyingi sana ambazo tunazipoteza kwa kuwatupa wazee hawa.

Haya si mageni sana kwetu ila wewe na mimi tujiulize kila mara Je, wazee hawa wanathamani gani kwangu? Tunafahamu kuwa wazee ni wale ambao kwa Neema ya Mungu wamefanikiwa kufikisha umri wa miaka 65+ ambao mimi na wewe tunaweza kuwaita baba, mama, babu au bibi na kwa umri wao kwa namna fulani wanategemea sana uwepo wetu, Je, umefanya mangapi kwaajili yao? Tufahamu kuwa mahitaji yao huongezeka siku baada ya siku kutokana na umri na mahitaji yao ya msingi ni kama vile afya bora kwa kula vizuri, mahitaji ya kiroho, ulinzi, wasaidizi wa kazi na mengine kama hayo. 

Najua kuna baadhi ya sababu ambazo zinatufanya tuone kuwa hatuwezi kwenda kijijini kuwasalimu wazee na kuwapatia yale mahitaji yao ya msingi, na sababu hizo ni kama vile hakuna umeme, ni mbali sana toka mjini, hakuna baathi ya mahitaji ya muhimu kama yale yaliyopo mjini, wengine wanasema kuna vumbi sana na baridi, wengine wanasema kuna wachawi nitalogwa, wengine watakwambia Nelly wazee wanalewa sana halafu inakuwa kero na wengine wanakwambia wazee wengine wana imani za kishirikina sana, wengine wanasema meengi wanayoweza kusema lakini hakuna sababu hata moja inayotengua ukweli kuwa, "Wazee ni Hazina"

Ni vizuri tukakumbushana ili kwanza tupate miaka mingi na heri duniani lakini pia tusisahau kwa wale wenzangu wenye matumaini kama yangu ya kuishi miaka zaidi ya 70 tukumbuke kuwa tutazeeka, Je, ni nani atatuhudumia? Kwani utamaduni tulionao ndio tunaowarithisha watoto wetu..., Itakuwaje na wao wakirithi yale ambayo tunawafanyia wazee wetu leo?  Usisingizie umeolwa au unaishi mbali, hapa hakuna cha kujitetea cha msingi ni kuwa kila mtu anatakiwa kuhakikisha kuwa anaishi maisha ambayo atakumbukwa na jamii lakini pia siku moja atapata fadhila hapa duniani na mbinguni kutokana na kazi njema aliyoifanya kwa taifa la Mungu.

Mnisamehe sana kwa hili ila kila atakayepata ujumbe huu, akumbuke wazee wake popote pale walipo hata kama hujaenda kwa miaka mingi ila ni vyema ukaenda kuwaona hata kama utafika kwa muda mfupi lakini usiwaache waondoke duniani kama vile hawakuacha kizazi, kwa Mungu lazima tutalipa. Biblia yangu inaniambia hivi, asiyejali wa nyumbani mwake ni mbaya kuliko muuaji, Je, wewe unawajali wa nyumbani mwako? Au unafurahia kufanya vitu vinavyoifanya jamii ikuone wa maana sana kama vile kutoa michango mikubwa mikubwa ya harusi, kupanga au kujenga nyumba za gharama ya juu, kutembelea magari mazuri, kula vya bei ya juu na kuwa na matumizi ya juu ili hali wa nyumbani mwako hasa kule ambako ndo asili yako wanataabika kwa kula miogo na viazi, wanaishi gizani, huduma duni za maji na afya wakati wewe unakula bata town kwa kisingizio eti " I am very busy"...hii ni mbaya sana....................................


As Simple as That. 
(We remain little Beings, trying to give You the little we have, Receive it Please.)


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda