Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, August 7, 2012

Papaa On Tuesday....Wenye Akili Zao HunyamazaNinakila sababu Za Kumshukuru Mungu Kwa ajili ya Siku hii Ya leo kutupa tena uzima. Ni Matumaini yangu kuwa mgogoro wa Kidiplomasia Baina ya Tanzania na Malawi Utamalizwa kwa Njia Za Kidiplomasia Zaidi Kuliko nguvu.

Mwaka 2010 tarehe 14, September niliandika Papaa On Tuesday yenye Kichwa cha 'Wenye Akili Zao Kimyaa". Nilipokuwa ninasoma Papaa On Tuesday hiyo nikapata Ufunuo Mwingine wa Wakati huu kupitia Ujumbe ule wa Mwaka 2010 uliokuwa unafanana na Mwaka huo.

Kunyamaza ni Silaha mojawapo inayotumika kwenye maisha na style hii haikuanza jana wala juzi. Ukisoma Biblia utaona wakati Yesu amezongwa na Wayahudi wakitaka kumsulubisha na wakimbeza na kumzomea na kuuliza kama kweli ni Mfalme wa Wayahudi, Yesu alikuwa hawajibu chochote alikuwa anajinyamazia Kimyaaaaa. Hata walipomuuliza wale wakuu wa Makuhani kama yeye ni Mwana Wa Mungu...Yesu na akili zake akijianyamazia Kimya.
Si Yesu tu, tazama Rais Mstaafu Mkapa, watu walisema mengi wakasema alifanya biashara Ikulu, yeye ni Fisadi Mkubwa, tulimbeza tukamwambia aibu yake ama aibu yetu, lakini Rai Mkapa alinyamaza Kimyaaaaaaa, Leo hii Mkapa anaonekana ni mtu muhimu kuliko Kiongozi kama Makamba alikuwa anaeongea kila kitu na kila siku akiwa CCM leo yuko wapi Kimyaaaaaa, yule yule tuliyembeza jana leo amegeuka kuwa rafiki, huyu alitumia akili zake kunyamaza kimyaaaa mwingine akatumia kuropoka.
Aliyekuwa Waziri Mkuu Mhe. Lowassa, mara baada ya kupata Kashfa ya Richmond Silaha pekee aliyotumia ni kunyamaza kimyaa, pasipo kujibu chochote. Kwa kunyamaza kwake imeanza kumuonesha yeye ni mtu mwenye akili na uwezo wa namna gani katika kupambana na wale waliokuwa wakimcheka na kumdharau. Leo Watu wale wale waliokuwa wanamuambia ametutia aibu tunasema Bora Lowassa Kuliko Mtoto wa Mkulima.

Hakuna Silaha kali na pengine mbaya kuliko mtu akunyamazie tena akunyamazie ukiwa hujui kwanini Kanyamaza. Kunyamaza ni Ishara ya kudharau, ukitaka kujua unadharauliwa ama lah basi mtu akunyamazie unamuuliza kitu anakutazama tu pengine juu mpaka chini, Unaweza kujiua kabisa. Assume umeolewa, pengine kutokana na matatizo ya ndoa ama shetani kupata nafasi katika ndoa, mwanamke akasaliti ndoa yake yaani aka cheat, uzuri ama ubaya mumeo siku akakukuta live live kabisa na huyo mwingine. Then Mume anaamua kulinyamazia hilo jambo kama halijatokea. Unamuomba msamaha ye anasema its ok na yameisha, ila hakusemeshi, hakuulizi wala hakusalimu. Kama unaroho nyepesi unabeba kilichochako unaenda nyumbani. Walio wanandoa wanajua ingawa wanadai sina experiance hahahaha afadhari unayamaziwe na Mchungaji wa Kanisa lako kuliko unyamaziwe na mpenzio ama mwenzi wako wa Maisha.

Huwezi ipotezea kirahisi inauma sana kunyamaziwa bila kujua hukumu ya Kosa lako bora mtu akuchape akuseme kiishe kuliko akupotezeee.
Kunyamaza wakati mwingine kwenye maisha inakupa sababu ya kujipanga ki-hoja zaidi katika makosa, wenye akili zao huwa wanatulia mambo yanapokuwa yanaenda mrama, kuna msemo unasema watasema mchana na usiku watalala, wenye akilizao wanapokuwa na wakati mgumu hunyamaza,kunyamaza kunamfanya adui yako amalize upesi kuongea kuliko ukijibizana nae, mkijibizana nae inampa nafasi ya kusema na mambo mengine lakini mtu akiongea na akatukana we unajinyamazia mwisho asimaye huamua kunyamaza na yeye.
 

Biblia inasema Mpumbavu akinyamaza huonekana anahekima. Ni heri kuna wakati unyamaze kimyaaaa utakuwa salama zaidi kuliko ukitaka kuongea ukajikuta umeharibu reputation yako uliyoijenga miaka mingi. Kuna Wakati Mwingine tabia ya Kukimbilia Kuongea Kama Yule Baba Wa Jeshi la Polisi, Jambo Kidogo tu anaita Media anavyoongea issue akapigwa na Maswali huwa naona inamdhihirisha  kwa kumuonesha “Real Him” ambayo kwangu naona ni vema akaitunza hiyo personality kwa kunyamaza...hapo wenye akili zao hujinyamazia. 
Nimalize kwa kusema, huwezi wazuia watu kuongea juu ya wewe, wengine wataongea mambo makubwa na mabaya kuhusu wewe, kila ukitaka kujibizana nao ndo inaonesha wewe ulivyo. Kabla hujajibizana nae kumbuka wenye akili zao hutulia kwanza na kijipanga ki-hoja kabla hawajakurupuka. Ukikurupuka tu basi aibu yako inaweza kuwa kubwa zaidi, Kunyamaza ni hekima ndo maana Biblia inasema Mpumbavu akinyamaza anaonekana ana hekima. Biblia kama ilivyosema kila jambo na Wakati Wake kuna wakati Wa Kusema na Kuna wakati Wa Kunyamaza. Usinyamaze tu unapokuwa Umelala, Ila hata pale ulipopaswa wakati mwingine kusema wewe nyamaza.

Kunyamza inakufanya kuelewa wapi ujipange na watu wanakuonaje pia. Huwezi wazuia watu kuongea kuna wanaoongea kwa kuzusha na kuna wanaoongea kwa kuongeza chumvi, lakini kunyamaza inakupa nafasi ya kujipanga. Leo ukifanya makosa either ukateleza katika maisha huwezi wazuia watu kuongea watasema sana aibu yako aibu yetuuu..lakini wenye akili zao?hapo wanayamaza. Kunyamaza kunakufanya ujipange na kuelewa nani yupo nawe na nani hayupo nawe kuna kujitia nguvu pale unapo nyamaza. Ukisoma Bible kuna wakati Daudi aligeukwa na rafiki zake, askari wenzake baada ya kukuta kila kitu chao kimeteketezwa ukisoma bible pamoja na shutuma zote But David Strengthern himself in the Lord. Kwenye maisha kuna wakati wa kunyamaza. Mtu mmoja alisema “There is a voice in every Silence” ukikaa mahali kimyaaaa just alone, wengine ndo tunapataga madesa ya kuongea na watu. Kama mtu mwenye akili timamu lazima kuna wakati wa kunyamaza.
Wakati mwingine kwenye maisha ni vema ukajinyamazia kuliko ukaongea, utakuwa na akili zaidi ukatunza personality kuliko ukasema neno moja likaharibu. Ukitaka kutunza heshima yako sio kila saa na kila kitu lazima uongee, jinyamazie kimyaaaaaa. Kwenye ndoa na mahusiano kumekuwa na kuto kuelewana sababu tu kila mtu hataki kuonewa, huyu akiongea na huyu anaongea, tujifunze kunywa maji na kutoyameza mtu anapokuweka kiti moto. Kukubali kosa ama makosa si kuonesha mapungufu kuliko ukiendelea kuongea ndo kuonesha hayo mapungufu uliyonayo kwa wenye akili zao huwa wanakunyamazia tu then wanaongea pembeni. Wanaume tumekuwa na ubabe wa kubeba maamuzi, wengine kutokana na vipaji vyetu vya kuongea kila Kosa tunataka Kujustfy kuwa ni a,b,c kwanini tusijifunze kunyamaza kama wenye akili?

Kuna Watu wanaongea sana, Wanaongea Kwa Maandishi Wanaongea na Maneno, sembuse siku hizi kuna facebook na Tweeter na zingine basi jambo lolote la kwake mtajua, akipata hela mtajua, akipata mchumba mtajua, akiachwa mtajua, akilala njaa mtajua, yaani chochote Cha Kwake Mtajua sababu ya Kuongea sana.

...//Papaa
0713 494110

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda